Mitandao ya simu wanatuibia, tena Wizi mkubwa, wateja tunajua??

Mitandao ya simu wanatuibia, tena Wizi mkubwa, wateja tunajua??

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
233
Reaction score
418
Hii imenitokea Mara kadhaa pale ninapoweka salio , huwa napenda kununua salio kupitia Mpesa au Tigo pesa , lakini ukinunua salio bila kujiunga kifurushi unakuta tayr wamekata pesa kidogo kuanzia sh 100, 200 au 250,

Nikasema labda kuna huduma nimejiunga , nikapiga simu kwa wateja na kuuliza wakanambia hakuna huduma yoyote niliyojiunga , sasa najiuliza pesa yangu imeenda Wap? Baada ya kuuliza nikaona na watu wengine wanalalamika vile vile duh!

Nasema huu ni wizi acheni
 
Niliwahi kununua kifurushi cha dakika tiGo wakanipa MB ilihali natumia nokia ya tochi, hili nililipita. Hatari ni pale nilijichanganya baada ya kutuma TZS 50,000 nikanunua muda wa maongezi elf50 yaan walikuwa wanakata wanavyojisikia. Toka asubuhi hadi jion unaweza kuta wanakata 400
 
Yaaan haya makampuni wanatufanyia vitu vya ajabu Sana, nimeongea nao wanasema pesa imekatwa sema matumiz yake bado hayajajulikana duh
 
Hiyo imetokea mara kadhaa kwangu,

Unaweka salio unaendelea na kazi utajiunga baadae,

Unazima kabisa na habari za data,

Nikijaribu kujiunga baadae inagoma

Ukicheki salio unakuta 50 hakuna au 100
 
Hiyo imetokea mara kadhaa kwangu,

Unaweka salio unaendelea na kazi utajiunga baadae,

Unazima kabisa na habari za data,

Nikijaribu kujiunga baadae inagoma

Ukicheki salio unakuta 50 hakuna au 100
Huu ni wizi kabsaa
 
Hawawezi sababu wanamaslahi humo
Unajua makampuni huwa yanafanya lobbying za training of new products ngoma inapigwa Hyatt regency au Ramada courtesy ya Voda,Tigo plus per diems na maposho misosi labda Oriental cuisine.

Kama ni mtendaji lazima upagawe kutenda kazi.
 
Ulipouliza 200 imeenda wapi ulijibiwa nini? Isije ikawa uliacha data on na automatic updates zikala pesa..
 
Ulipouliza kama una huduma ukajibiwa huna huduma yoyote, sasa salio langu limeenda wapi? Ukajibiwa nini?
 
Huo wiz haujaanza leo ni mda mrefu wananikata salio hata nikiwapigia hawatoi majibu ya kueleweka tcra wapo kimya.
 
Lasway.Jr

kabla ya kununua muda wa hewani kwa mpesa/tigopesa au vocha hakikisha KWANZA unazima DATA. HALAFU endelea kufuatilia kama wanaendelea kukata.

lkn kwa ujumla usanii upo. utakuta wakati mwingine mimi nina full airtime za mitandao yote, lkn utakuta ukipiga simu wanakwambia huna salio la kutosha. nashindwa kuelewa.
 
Airtel tu,kidogo hawa jamaa wapo vizuri ila kwenye suala la internet ni bure kabisa utasema tupo zama za mawe.
 
Weird sana na ni mitandao yote,uzime data usizime ila 50-100 watakuibia tu na kwao ni hela nyingi sana wanaiba!!
Tigo wanakadiriwa kuwa na customers 5mln+

Kwa mwezi waibie mara moja tu customers 2mln shs 100 tu= 2,000,000 x 200 tusaidiane jibu!!

Huu wizi hawawezi kuacha bila ya wateja kulindwa na haya makampuni kushitakiwa /kkupigwa fine!!
 
Hivi kwamfano watanzania woote kwa ujumla wenu mkaamua kususia matumizi ya mitandao mnayoona inawaibia wazi wazi mnafikiri hawatopata akili?

Yani kama ni tigo mnaamua kuihama woote, mnazira mbona watabadilika tu.

Tatizo watanzania wameshazoea kukubaliana na kuonewa na kufanya kama ni hali ya kawaida baada ya muda!
 
Hawawezi sababu wanamaslahi humo
Naungana mkono na mtoa hoja,tcra wana masilahi mapana au lasivyo wangekuwa wamefanyia kazi hili jambo.
Mtu anaomba muda wa maongezi unakuta wakuwekea SMS,MB, sijui nini ilmradi wafyeke hela ya mteja.
Kwa nini kila huduma isijitegemee?

Wezi wa mchana kweupe.
 
Kiukweli TCRA wamelala sana katika hii industry ya mawasiliano, lakini pia sisi wateja wa haya makampuni kwa ujumla wetu hatutambui haki zetu na tumeridhika na huu wizi wa rejareja,,, yaani tumezoea kuonewa na sisi kukaa kimya!!

Laiti kama wateja tungekuwa tunafungua kesi mahakamani juu ya huu wizi wallahi haya makampuni yangestop hii dhulma, lakini tumejinyamazia kimya..!!

Nawapongeza sana wanamuziki wetu kina AY na MwanaFA kwa kuifikisha Tigo mahakamani kudai fidia ya dhulma iliyofanyika, sasa wakipatikana wadau wengine kwenda kufungua mashtaka na haya mambo yakaanikwa mitandaoni basi nna uhakika huu ujinga watauacha maana hawatakubali kuona kampuni ikiloose trust kwa jamii!!!
 
Lasway.Jr

kabla ya kununua muda wa hewani kwa mpesa/tigopesa au vocha hakikisha KWANZA unazima DATA. HALAFU endelea kufuatilia kama wanaendelea kukata.

lkn kwa ujumla usanii upo. utakuta wakati mwingine mimi nina full airtime za mitandao yote, lkn utakuta ukipiga simu wanakwambia huna salio la kutosha. nashindwa kuelewa.
hakuna cha data on..wanaiba na ukipiga hawapokei
 
Lasway.Jr

kabla ya kununua muda wa hewani kwa mpesa/tigopesa au vocha hakikisha KWANZA unazima DATA. HALAFU endelea kufuatilia kama wanaendelea kukata.

lkn kwa ujumla usanii upo. utakuta wakati mwingine mimi nina full airtime za mitandao yote, lkn utakuta ukipiga simu wanakwambia huna salio la kutosha. nashindwa kuelewa.
Naelewa ninachokisema mkuu, hawa jamaa ni wezi.
 
Back
Top Bottom