SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,280
Ninafahamu kwamba mitandao karibu yote ya simu imeanika sokoni vifurushi vya intaneti.Ninachotumia mimi ni vodacom BOMBA7. Kifurushi hiki kiko hivi: kinanunuliwa kwa sh 10,000 na unapata MB 750 kwa wiki. Wao Hawasubiri hizo mb ziishe ila wanahesabu siku tu! Siku saba zikiisha hata kama una akiba ya mb, kwa mfano 200, zinakufa ndani. Hii naona kama ni uonevu na wizi.Ninataka kuhamia penye unafuu. Sasa nawauliza wanajf, je, ni mtandao upi wenye vifurushi nafuu kwa mlalahoi kama mimi?
NINAWATAKIENI HERI YA MWAKA MPYA! MWAKA 2012 BILA BAN INAWEZEKANA!
NINAWATAKIENI HERI YA MWAKA MPYA! MWAKA 2012 BILA BAN INAWEZEKANA!