Mitandao mipya ni hatari sana

Mitandao mipya ni hatari sana

Joined
Mar 14, 2014
Posts
90
Reaction score
6
Baada ya muda mrefu tangu tahadhari zitolewe kuhusu wale waliojiunga na mtandao wa Telex free kuwa ni "illegal" na Benki Kuu ya Tanzania haitambui mtandao huo wa "online marketing", sasa yametimia maana mtandao wa Telex Free UMEFUNGWA rasmi.
Watanzania zaidi ya 20,000 wadaiwa kupata hasara kubwa ya kifedha na mpaka sasa hawajui namna ya kukomboa fedha zao.
Itakumbukwa kuwa ili uweze kufungua "account" Telex Free ni lazima ulipie kiingilio ambacho kilikuwa kinaanzia 600,000 TZS na kuendelea. Hivyo, hatua ya kufungwa kwa mtandao huo kumepoteza fedha zote za kiingilio na faida zote ambazo wanachama wa Telex Free walijipatia pindi walipokuwa wakifanya kazi na mtandao huo.
Poleni sana Watanzania wenzangu mliopatwa na janga hili. Hakika Pasaka imekuja vibaya sana
Kua makini na kampuni za mitandaoni hasa unapoamua kujiunga nazo.
Pasaka njema
for more inf 0766789288
masternyari@gmail.com
 
tatzo watu wanapenda mteremko. maisha hayapo hivo.
 
poleni mliofikwa na majanga jamani!!

Sikukuu njema pia kwenu!!
 
Hapo haipo tena sikukuu njema kwa waliotapeliwa. Kwa nini lakini wabongo hawajifunzi kwa mapato ya jasho? Decci haikuwapa funzo?.
 
serikal nayo ilaumiwe wanaona hvi vitu vya kijinga vinaendlea wanafumbia macho bdae wanafungua kesi kimagumashi,, halaf znayeyukia hewani kama deci,wakati mwingne nashindwa kuacha kusema kuna mikono ya wanene humo,kwanin wakubali vitu kama hvyo?
 
Serikali haihusiki,huo ni upumbafu wa mtu mwenyewe,watu wanapenda urahisi rahisi tuu. Wangeibiwa hata 50m kila mtu ingekua poa maana wametaka wenyewe.
serikal nayo ilaumiwe wanaona hvi vitu vya kijinga vinaendlea wanafumbia macho bdae wanafungua kesi kimagumashi,, halaf znayeyukia hewani kama deci,wakati mwingne nashindwa kuacha kusema kuna mikono ya wanene humo,kwanin wakubali vitu kama hvyo?
 
Polenii mlotapeliwa pesa zenu, ila siku nyingine muwe makini na mkiambiwa ni hatar chunguzeni kwa umakini. Na wale mlioshawishiwa na masupastaa kamma JOYCE KIRIA kawadaini sasa......teh teh
 
serikal nayo ilaumiwe wanaona hvi vitu vya kijinga vinaendlea wanafumbia macho bdae wanafungua kesi kimagumashi,, halaf znayeyukia hewani kama deci,wakati mwingne nashindwa kuacha kusema kuna mikono ya wanene humo,kwanin wakubali vitu kama hvyo?
Benki kuu ilishakemea,wewe ulitaka hadi nani aseme?
 
serikal nayo ilaumiwe wanaona hvi vitu vya kijinga vinaendlea wanafumbia macho bdae wanafungua kesi kimagumashi,, halaf znayeyukia hewani kama deci,wakati mwingne nashindwa kuacha kusema kuna mikono ya wanene humo,kwanin wakubali vitu kama hvyo?

Nani alikubali?serikali gani iliidhinisha huo mtandao?
 
Kuna mkono wa kigogo hapo, sio bure jiulize kama haikutambuliwa na bank kuu ilipataje kibali cha kuendesha shughuli zake? imefungwa na nani na kwanini? naomba serikali ya JK ifatilie hili suala, maana haiwezekani kampuni kuwaibia wananchi wakati serikali yao ipo!
 
Tatizo hizi iSsue zinakuwaga Online, halafu Sirikali yetu huwa inachelewa kutoa taarifa hukuwengi wakiwa tayar imesha athirika. Let's go back to DECI, serikali ilikuja kutoa taarifa kuwa hawaitambui DECI after two years in Operation. It was too late kwa kweli. Ndo Maana unakuta wengi washaangukia pua tayari.

Ila, We must understand that, No easy Money. We must work hard. Don't let anyone deceit/fool you in any how.
Be yourSelf and have critical thinking. No one will deceive you.
 
serikal nayo ilaumiwe wanaona hvi vitu vya kijinga vinaendlea wanafumbia macho bdae wanafungua kesi kimagumashi,, halaf znayeyukia hewani kama deci,wakati mwingne nashindwa kuacha kusema kuna mikono ya wanene humo,kwanin wakubali vitu kama hvyo?

Mbona serikali ikishatoa tamko kuwa haiitambui hiyo Telex free na yatakaemkuta asilalamike!!
 
Back
Top Bottom