Mitambo ya Umeme ya Kampuni ya Symbion Power kupigwa mnada

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,224
12,944
Mitambo ya Kampuni ya kufua umeme nchini "Symbion" imeshindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara takribani miaka mitatu sasa hivyo kupelekea kampuni hiyo kushtakiwa mahakama ya kazi na hatimae tangazo rasmi limebandikwa la kupigwa minada mitambo yake.

Ikumbukwe mitambo hiyo ilizulinduliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Dr. Kikwete sambamba na Mh Barack Obama aliyekuwa Rais wa Marekani kwapamoja, Mitambo hii iliwahi kuingiwa na kashfa ya ufisadi huku link yake ikitoka katika kampuni ya Richmond zote kutoka nchini Marekani.

=====

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, imeamuru Kampuni ya kufua umeme Symbion Power Tanzania Limited, kuwalipa waliokuwa wafanyakazi wake zaidi ya Sh. bilioni 12 ambazo ni malimbikizo ya mishahara yao.

Wafanyakazi hao 43, wanaidai kampuni hiyo Sh. 12,249,890,439 tangu mwajiri huyo aliposimama kuwalipa mwaka 2016 baada ya serikali kupitia Shirika la Umeme (TANESCO) kusitisha mkataba.

 
Mitambo ya Kampuni ya kufua umeme nchini "Symbion" imeshindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara takribani miaka mitatu sasa hivo kupelekea kampuni hiyo kushtakiwa mahakama ya kazi, na hatimae tangazo lasmi limebadikwa la kupigwa minada mitambo yake...
Kwa utawala huu hakuna atakayejitosa kununua mitambo hii! Nashauri wanunuzi wa vyuma chakavu wauziwe hayo mavyuma.
 
Mzee kampuni kwa kasha zake zile za kuwauzia umeme Tanesco bei kubwa na kuwatoza service cherge! Sina hakika kama inauwauzia umeme mpaka leo katika kipindi hiki cha Magu! Hizi kampuni zikijiendesha kiwizi sana, wametupiga mno

Wote waliohusika na hii mikataba isiyo na tija wapo wengi ni CCM.

Ndiyo maana mimi uwa siwakubali CCM sababu wamelitia hasara sana Taifa
 
Mitambo ya Kampuni ya kufua umeme nchini "Symbion" imeshindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara takribani miaka mitatu sasa hivo kupelekea kampuni hiyo kushtakiwa mahakama ya kazi, na hatimae tangazo lasmi limebadikwa la kupigwa minada mitambo yake...
Wafanyakazi 48 wanadai mishahara ya Bilion 12 kwa miaka 3. Kuna watu wanalipwa kipande kirefu nchi hii..
Jarib kuweka wastani ni kama sh ngap kwa mwezi.

Sawa na milion 141 kwa miaka 3.
 
Back
Top Bottom