Mitambo ya Nyuklia ya Irani Kubomolewa ndani ya Masaa Machache

Mitambo ya Nyuklia ya Irani Kubomolewa ndani ya Masaa Machache

Mlaleo

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
16,376
Reaction score
13,196
Waziri: Nyuklia ya Irani Inawezekana kuharibiwa Ndani ya 'Masaa' tu

2013/08/09, 11:45

Waziri wa mambo ya nje nchini Israel anasema 'masaa machache tu ya mashambulizi ya angani' yatakuwa ndio mwisho wa matarajio ya nyuklia nchini Irani endapo mashinikizo ya jumuiya ya kimataifa yatashindwa.

jumuiya ya kimataifa lazima iwe wazi kwa Iran kuwa ina chaguzi mbili tu: kumaliza mpango wake wa nyuklia kwa hiari, au "kuona ikiharibiwa kwa nguvu za Kinyama," Waziri wa Mambo ya Mkakati Yuval Steinitz amesema, akizungumza na gazeti la Washington post.

Kuibomoa mpango wa nguvu za kinyuklia wa Irani inawezekana kabisa, alisema, kukadiria kuwa itachukua "masaa machache ya Mashambulizi ya Angani, hakuna la zaidi."

Yeye hakusema yote juu ya wasiwasi na uwezekano wa Iran kwamba inaweza kujibu mashambulizi kwa makombora yake yatue nchini Israeli katika kukabiliana na mashambulizi ya kimataifa juu ya mitambo yake. Mashambulizi ya Irani yakitumwa kwetu yatasababisha "uharibifu mdogo sana," alisema, akielezea kuwa Israeli itakuwa na uwezo wa kuyazuia zaidi makombora ya Irani kwa Mitambo yao maarumu ya kuzuia Makombora.

Rais mpya wa Irani, Hassan Rouhani, ameelezea nia ya kujadili na jumuiya ya kimataifa juu ya mpango wa nchi yake na mipango yake ya nguvu za kinyuklia.

Hata hivyo, viongozi wa Israel wameonya dhidi ya ulimwengu kuwa wanaamini kuwa kauli Rouhani ya umma. "Bila shaka anataka mazungumzo zaidi. Yeye anataka kuzungumza na kuzungumza na kuzungumza. Na wakati kila mtu anapokuwa bize kuzungumza naye, yeye atakuwa bize kurutubisha madini ya uranium yakisharutubishwa yanaweza kutengeneza Bomu la maangamizi, "Waziri Mkuu Binyamin Netanyahu alionya wiki hii katika mkutano na wabunge nchini Marekani.

"Hii si siri. Rais mpya wa Iran anajivunia kwamba ni mkakati wake, "aliongeza.

Steinitz alikubali. "Rouhani hana haiba, yeye ni mjanja, na yeye kutabasamu njia yote ya bomu," aliiambia Post.

Netanyahu ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kukabiliana na kudumisha shinikizo juu ya Iran.

"Rais wa Iran alisema kwamba mashinikizo hayawezi kusaidia kumzuia kuendeleza mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia. Lakini tunaona kwamba zaidi ya miongo miwili iliyopita, Njia pekee ambayo imesaidia imekuwa ni shinikizo tu, "alisema.

378189.jpg
Dege la Kivita la Israel...

iron_dome_156425619_620x350.jpg

Mitambo ya Kuzuia Makombora ya Israel... jinsi inavyofanya kazi
Kampuni ya Rafael

Katika miaka ya karibuni kimekuwa kikifanya kazi ya kutengeneza mtambo ambao utakuwa na uwezo wa kufanya kazi barabara kwa kila aina ya misimu ya hewa ambao Unaitwa Ghuba ya chuma ya Majira yote (All-Weather Iron Dome

2039097592.jpg

ujenzi wa kituo cha Fordow ambacho kipo ndani ya mlima kipo juu ya maili 20 kaskazini kaskazini wa Qom, Iran. Picha na AP
 
hata huyo rais mpya wa iran ana msimamo mkali kama Nejad?
 
Acha kuandika kishabiki. Kwani Irani hawana silaha? Israel anategemea USA wakati Muirani ana tengeneza mwenyewe

Unachekesha.... Irani hana Akili ya kutengeneza kifaa chochote zaidi ya Ndala na Birika la Kahawa.... fuatilia ujue... wale ni wezi tu na vifaa vyote vinatoka ulaya marekani na Israel pia wanatumia pesa ya mafuta tu kununua na kuiba tech karibu kila kitu wanatumia maengeneer wa Kizungu Germany Russia na mayahudi... Ushabiki upi soma upate elmu kwanza wacha nikale Mpunga nitarejea na data za wezi wanaotumwa na Serikali ya Iran kuiba tech na kushawishi Mafundi wahamie Iran kwa Pesa Nzuri.
 
kama hivo ndivyo basi wana mpango mzuri, muda tu wataanza kujitegemea.
 
Israel inaweza kuiangamiza mitambo ya Iran ndani ya Masaa ni kweli lakini Iran inaweza kuifuta Israel ktk uso wa Dunia ndani ya nusu saa...Israel ilivilipua vinu vya nyuklia vya sadam miaka ya 80 na baadae Syria 2006 lakini imeshindwa na inapiga kelele ili US ndo awe wa kwanza na US intellegecia kwenye vyombo vya Israel vinasema US hana ata hamu ya kuivamia Iran zaid waibinye kiuchumi na wachochee vikundi vya ndani viipindue serikali kama Syria..Iran is only superpower in middle east with No nukes
 
Unachekesha.... Irani hana Akili ya kutengeneza kifaa chochote zaidi ya Ndala na Birika la Kahawa.... fuatilia ujue... wale ni wezi tu na vifaa vyote vinatoka ulaya!
Dah kweli jamaa unachuki sana! Iran sio level zetu ata kwa nchi nyingi za ulaya ! Jaribu kugoogle MADE IN IRAN ndo utajidharau..jamaa wana export mpaka Ulaya vitu kibao tu! Iran ina home grown aircraft, helicopter and figherjet Israel hana anatumia F15,F16 za US na ana order ya F22 raptor or fifth generation z
 
Unachekesha.... Irani hana Akili ya kutengeneza kifaa chochote zaidi ya Ndala na Birika la Kahawa.... fuatilia ujue... wale ni wezi tu na vifaa vyote vinatoka ulaya marekani na Israel pia wanatumia pesa ya mafuta tu kununua na kuiba tech karibu kila kitu wanatumia maengeneer wa Kizungu Germany Russia na mayahudi... Ushabiki upi soma upate elmu kwanza wacha nikale Mpunga nitarejea na data za wezi wanaotumwa na Serikali ya Iran kuiba tech na kushawishi Mafundi wahamie Iran kwa Pesa Nzuri.
Wezi?!! siamini.

Ninakubaliana na maoni yako kuwa kwa kiasi fulani Irani ina ushirikiano wa nyuma ya pazia kati yake na Mayahudi(wa kidugu),Germany, Russia umesahau na Marekani.

...Muirani aliyekuwa akipiga kelele kutwa kuchwa kuwa Marekani ni Shetani alipata nafasi ya kumuadhibu Mmarekani aliyejileta mwenyewe mlangoni (Iraq)! kwa nini asiitumie nafasi ile?

Msijihangaishe na kusumbua vichwa vyenu Iran haitashambuliwa na America wala Israel.

America na Israel nazo hazitashambuliwa na Iran kamwe! ukiondolea ubabaishaji wa Wairani "kuwasidia" Hizbollah kurusha vijiroketi viwili vitatu ndani ya Israel halafu Mayahudi nao wanakuja kulipiza kisasi kwa kuwaua maelfu ya Waislamu Sunni kwa sababu ya "kuwasaka" na "kuwashikisha adabu" Hizbollah.

Ni gemu kubwa linaloendelea...
 
Acha kuandika kishabiki. Kwani Irani hawana silaha? Israel anategemea USA wakati Muirani ana tengeneza mwenyewe

Muulize ile drone ya Hisbollah iliyopita juu ya Fordow na kupiga picha...ikajakustikiwa inataka kuvuka mpaka ...muda huo mtambo ulikuwa haujakamilika !?
 
Acha kuandika kishabiki. Kwani Irani hawana silaha? Israel anategemea USA wakati Muirani ana tengeneza mwenyewe
USA inamtegemea sana Mu Israel.. kama si Israeli kutia mguu kwa Sadam, USA angeumua vilivyo
 
Israel hawezi kuishambulia Iran kwa sababu anafahamu nguvu ya Iran katika messile ambazo zinaweza kuiharibu Tel Aviv Yof.Angekuwa anauwezo angefanya tangu zamani kama alivyofanya Iraq,Syria na Sudan.
 
Unachekesha.... Irani hana Akili ya kutengeneza kifaa chochote zaidi ya Ndala na Birika la Kahawa.... fuatilia ujue... wale ni wezi tu na vifaa vyote vinatoka ulaya marekani na Israel pia wanatumia pesa ya mafuta tu kununua na kuiba tech karibu kila kitu wanatumia maengeneer wa Kizungu Germany Russia na mayahudi... Ushabiki upi soma upate elmu kwanza wacha nikale Mpunga nitarejea na data za wezi wanaotumwa na Serikali ya Iran kuiba tech na kushawishi Mafundi wahamie Iran kwa Pesa Nzuri.

wewe ntakujib baadae maana nakuona unaropoka tu biladata,utachekwa ndugu.
 
Israel hawezi kuishambulia Iran kwa sababu anafahamu nguvu ya Iran katika messile ambazo zinaweza kuiharibu Tel Aviv Yof.Angekuwa anauwezo angefanya tangu zamani kama alivyofanya Iraq,Syria na Sudan.

Wenzio huko Irani wananchi hawataki kabisa Ugomvi na Israel wanaishi kwa hofu kwani wakati wowote kinaweza kikanuka Maisha ya Irani yapo chini sana nina mshikaji wangu alienda wanatia huruma sana wana mawazo ya kukimbia nchi tu wengi kwa sasa wanakimbilia Australia wanaenda Indonesia kisha wanakula bot za njia ya panya kufika pwani za Australia... Makombora ya Irani yote yanazuilika Israel kesha yaona na kupima na Ujue Iran na Israel wapo Mbali sana Israel anaweza kuifikia Iran kwa Urahisi sababu anauwezo mkubwa zaidi ila iran ni Shida tu anamtegemea Russia kwa Vifaa... Fuatilia kinu cha Nuclear cha Fordow kililipuka na nani alihisiwa....

http://www.youtube.com/watch?v=06GbQQQbP30
 
Back
Top Bottom