Mitambo ya nyuklia balaa!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo ya nyuklia balaa!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kadogoo, Mar 15, 2011.

 1. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nchi zilizoendela kwa kutegemea msaada wa nguvu za Nyuklia ziko hatarini kurudi nyuma kimaendeleo na hata kuhatarisha Afya za raia wao baada ya kugundua kuwa Mitambo yao haiko salama kutokana na Tetemeko la ardhi la Japan ambalo limeitikisa mitambo yake ya nguvu za nyuklia!!!!

  Hivi sasa viongozi wa nchi zinazojiita Tajiri sana duniani wako Ufaransa kwa mkutano maalum na mada kuu inahusu mitambo hiyo huku Mawaziri wa Nishati wa nchi za EU wakikutana Ubelgiji kuzungumzia Tetemeko hilo na hatari ya kuisambaratisha mitambo yao ya Nyuklia!!

  Tayari Serikali ya Ujerumani imeamua kudurusu mitambo yake na kuhakiki uwezekano wa kuathiriwa na majanga kama ya Japan!!

  Hali hii imesababisha Hisa ktk Ulaya, Asia na USA kuporomoka kwa kasi tangu mkasa huu utokee Japan na kuna hatari ya uchumi wa Dunia kutikisika tena na kusababisha maafa na umaskini zaidi ktk Dunia yetu hii!!
  Sasa nchi Tajiri zikiwa zinajiandaa na mikakati ya kujinusuru na maafa na majanga ya Mitambo yao Nyuklia sijui sisi Walala hoi wa Dunia ya 3 tunajiandaaje???

  Habari zaidi gonga hapa: BBC News - Japan earthquake: Radiation levels fall at Fukushima
   
 2. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,086
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  Unajua tatizo la haya madude ni mionzi yake kwahiyo hasara yake ni kubwa mno. Huku kwetu wala wasijaribu kuyaleta hayo kwasababu hatuna utamaduni wa kuwa makini. Tunaleta mizaha sana katika mambo muhimu sasa hii teknologia ya nyuklia haiitaji upuuzi hata kidogo.
   
 3. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  ukimchimbia shimo mwenzio ili adumbukie,basi utaanza kudumbukia wewe kwanza.
   
Loading...