Mitambo ya IPTL yazimwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo ya IPTL yazimwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Jul 18, 2011.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mitambo ya IPTL yazimwa [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 17 July 2011 20:43 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Ramadhan Semtawa
  MATUMAINI ya kupungua kwa makali ya mgawo wa umeme nchini, yamezidi kutoweka baada ya mitambo ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), inayozalisha megawati 100 kuzimwa kabisa kutokana na ukosefu wa mafuta.

  Hatua hiyo imekuja wakati wabunge leo wakitarajiwa kuendelea kujadili hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini, Willliam Ngeleja, iliyowasilishwa Bungeni Ijumaa iliyopita na kupingwa na wabunge wengi wa CCM na upinzani.

  Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana, zilisema mitambo hiyo sasa haizalishi umeme, ingawa serikali imekuwa ikieleza kuwa kiwango cha uzalishaji kimepungua kutoka megawati 100 hadi kufikia 10.

  Kwa majibu wa habari hizo, kupungua kwa uzalishaji wa umeme kwa kiwango cha mgewati 100 katika IPTL kunatokeza katika kipindi ambacho, tayari nchi imeshatikiswa na makali ya mgawo huo ambao sasa hivi umeonekana kukosa ratiba maalumu.Habari za uhakika na zilizothibitishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, jana zilisema tatizo hilo limetokana na uhaba wa mafuta.

  "Kulikuwa na tatizo la ukosefu wa mafuta ambalo limekuwa likishughulikiwa na nadhani, litakuwa limepatiwa ufumbuzi, lakini taarifa zaidi mtafute mtu wetu wa mawasiliano," alisema Malima.

  Wakati Malima akisema hayo, vyanzo huru vimeiarifu Mwananchi kuwa tayari IPTL imesimamisha uzalishaji na hatua hiyo imezusha hofu kwa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

  Mmoja wa wakurugenzi wa CTI ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuna hatari ya uzalishaji viwandani ukaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na kupungua kwa umeme.Alisema kupungua uzalishaji wa megawati 100 za umeme katika IPTL ni hatari kwa uchumi wa nchi ambao kila mara umekuwa ukipigwa na mawimbi mazito ya mgawo wa umeme.

  "Serikali haitaki kusema ukweli, lakini hizo megawati zinazozalishwa kidogo kidogo na IPTL nazo sasa hivi hazipo tena. Hali ya umeme ni mbaya kweli kwa sasa," alieleza kigogo huyo wa CTI.

  Mkurugenzi huyo alisema, hata upatikanaji wa gesi asilia kwa ajili ya uzalishaji umeme nchini kwa sasam ni jambo ambalo haliwekwi wazi, lakini nako kuna tatizo kubwa linaloweza kuitikisa nchi kiuchumi.

  Kwa mujibu wa habari kutoka CTI, gesi ambayo hutumika kuzalisha umeme katika mitambo mikubwa nayo inapatikana kwa shida.Alipoulizwa kuhusu IPTL kuzima mitambo, Msemaji Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Aloyce Tesha, alikiri , lakini alisema tayari kibali cha kupata Sh17 bilioni kutoka serikalini kimepatikana.

  Kwa mujibu wa Tesha, , kinachofanyika sasa ni kuweka utaratibu wa kununua mafuta na kuyapakia kwenye malori.

  Alifafanua kwamba matarajio ni kuona kuwa hadi Jumatano uzalishaji umeme katika kituo hicho, unarudi katika kiwango chote cha asilimia 100 kama hakutakuwa na tatizo lolote la kiufundi.
  Hata hivyo, Tesha alisema uzalishaji haukusimama kwa asilimia 100 na kwamba ulikuwa ukiendelea kwa kiwango kidogo cha hadi asilimia 10.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  His position is hanging by thread!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,956
  Trophy Points: 280
  He should be fired as soon as possible :(
   
 4. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wana JF hivi anayetakiwa kununua mafuta ni TANESCO au ni IPTL? ufahamu wangu ni kuwa IPTL wameingia mkataba kuiuzia TANESCO umeme wa megawati 100 ambao huingizwa kwenye gridi ya taifa. je?
  1. IPTL hailipwi pesa na TANESCO kiasi kushindwa kununua mafuta? (kama wananunua wenyewe)
  2. Je TANESCO wameingi mkataba tata tena na IPTL wa wao kununua mafuta ilihali IPTL wanalipwa pesa kwa uzalishaji?
  3. Je kipindi hiki cha IPTL ambapo hawaproduce umeme whose fault? who is paying who? tafadhali naomba kuwasili
   
 5. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Si kuna habari humu kuwa IPTL imetolewa amri ya kufirisiwa? Au mimi lugha imenipita kulia kwenye hiyo thread au sina info zaidi?
   
 6. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Asante ccm dhamira yenu ya dhati umeiona,shida,umasikini,mahangaiko kwa kila mtanzania.giza lainyemelea nchi then utasikia leo lingeleja linasema tunasambaza umeme vijijini,ujuha huu
   
 7. L

  Losemo Senior Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazime kila kitu tujue moja. Mimi nataka waendelee kutuudhi mpaka tuchukie tuamue la kufanya kama Watanzania. Itakapofikia hapo watashika adabu yao. Iweje serikali inunue mafuta na wao waiuzie TANESCO umeme. Sielewi hata kidogo. Kwani huo ni mtambo wa serikali? Iweje uinunulie gari mafuta na wakati wa kusafiri ulipe nauli. Haingiiakilini samahani
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Losemo unajua mwisho wa ubaya ni aibu sasa tunaanza kujua mengi kupitia hii mikataba yao mibovu !
   
 9. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nadhani watanzania tunatendewa yote haya kutokana na upole wetu na wao wanatembea kifua mbele wakitangaza tanzania kuna amani ... je huu uonevu wa umeme ndo tuendelee kukaa kimya???
   
Loading...