Mita 200: Jicho la kisheria (Tafsiri yangu binafsi)

Mita 200: Jicho la kisheria (Tafsiri yangu binafsi)

Na sisi ambao nyumba zetu zipo ndani ya mita 100 distance ya kituo cha kupigia kura tuhame majumbani? maana mkumbuke hivyo vituo vimetukuta sisi tumeshajenga.

Naomba ufafanuzi wa kisheria hapa.

Kwako swala la umbali linajifia kifo cha mende ama sisiemu, isipokuwa zingatia yale yote yaliyokatazwa na sheria hii. WALAKINI ni ruhusa kuchungulia kupitia dirishani kwako kuona kinachoendelea ndani ya chumba cha kuhesabia kura. Ukiona fisiemu wanachakachua mawakala, unakinukisha kwa wale walio nje ya mita mia 200.
 
Nimepima mita 200 kutoka kituo changu, nimejikuta kituo cha polisi

Pole mkuu, itabidi uisaidie polisi kwa kazi za kaunta ama ulinzi kituoni, maana hakuna jinsi nyingine.
 
Kuna mvutano kuhusu mita 200 siku ya uchaguzi na tafsiri yake. Nami najitokeza jamvini kuweka kifungu cha sheria husika pamoja na kuchambua kwa tafsiri kifungu husika. Naweka jambo hili katika jukwaa hili kwakuwa ndilo Jukwaa linalotembelewa na wanaJF wengi kuliko mengine. Nawaomba wakuu moderators mnivumilie kwa hili. Nia yangu ni kuchangia na ikiwezekana kuelimisha.

Sheria husika katika jambo hili ni Sheria ya Uchaguzi wa Kitaifa ( the National Elections Act), Sura Nambari 343 ya Sheria za Tanzania. Kifungu husika ni kifungu cha 104 cha Sheria tajwa. Nakiweka kama kilivyo, katika lugha ya kiingereza, ili ituongoze kuunga mkono au kukosoa tafsiri yangu juu ya kifungu husika. Kifungu cha 104 kinasomeka hivi:

104.-(1) No person shall hold a meeting on election day or within any building where voting in an election is in progress, or at any place within the radius of two hundred metres of such building wear or display any card photograph, favour or other emblem indicating support for a particular candidate in the election.


(2) Any person acting in contravention of this section commits an offence and shall be on conviction to a fine of not less than fifty thousand shillings and not exceeding one hundred thousand shillings.

Sasa twende taratibu. Kifungu cha 104 (1) kinamkataza mtu yeyote kufanya mkutano katika siku ya kupiga kura au kwenye jengo lolote ambamo upigaji kura unaendelea au katika sehemu yoyote ya umbali wa mita 200 kutokea jengo la kupigia kura kuvaa au kuonyesha picha, ushawishi au nembo zozote zinazoonyesha kumuunga mkono mgombea fulani kwenye uchaguzi husika.

Kifungu cha 104 (2) kinatoa adhabu kwa mtu atakayekiuka kifungu cha 104 (1). Adhabu husika, baada ya kukutwa na hatia mahakamani, ni faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na kuzidi shilingi laki moja. Kimsingi, kosa lililoainishwa katika kifungu cha 104 (1) halina adhabu ya kifungo jela.

Kwanza, kifungu cha 104 (1) kinakataza nini? Kinakataza kufanyika kwa mkutano katika siku ya kupiga kura. Pia, kinakataza kuvaa au kuonyesha picha au nembo inayoonyesha kumuunga mkono mgombea fulani kwenye uchaguzi ambao unakuwa unafanyika. Mkutano, uvaaji au uonyeshaji unakatazwa kwenye jengo la kupigia kura na kwenye sehemu yoyote au jengo lililo kwenye umbali wa mita 200 kutoka jengo la kupigia kura.

Kwanini vitu hivyo vinakatazwa? Mosi, kwakuwa muda wa kampeni ulikwisha. Mambo hayo yalisharuhusiwa na kufanyika. Pili, ni kwa ajili ya kulinda amani. Wananchi wanaweza kuvurugana sehemu ya kupigia kura kama watatambuana kiushabiki wa vyama au wagombea wao. Tatu, siku ya uchaguzi, mambo hayo huwa ya kitaifa zaidi. Nne, utulivu. Mikutano ikiruhusiwa siku hiyo na mahali pa kupigiakura, ukimya utapotea.

Iko wazi hadi hapo kuwa, kama wananchi hawatafanya mkutano, kuvaa au kuonyesha picha au nembo zinazoonyesha kumuunga mkono mgombea fulani kwenye uchaguzi husika baada ya mita 200 wanaruhusiwa kuwepo. Wanaruhusiwa kuwepo kuendelea na shughuli zao ikiwa tu hawapo ndani ya mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura. Ingawa adhabu ya kukiuka Sheria ninayoizungumzia hap si kubwa, kinachoogofya ni jinsi ya kukamatwa kwa watuhumiwa.

Nasisitiza kuwa hii ni tafsiri yangu binafsi ya kifungu cha 104 cha the National Elections Act, Chapter 343. Nawashukuru wanaJF. Karibuni kwa mjadala.

Learned fellow kumekuwa na tatizo.kwa watu wanaokitafsiri kifungu hiki wanatoa maana ambayo si halisi kwa makusudi ama kwa kutumia njia ambayo si sahihi kutafsiri kifungu hicho cha 104, ukitumia literal rule of statutory interpretation unapata maana potofu juu ya kifungu hicho.
hivyo ni lazima uende kwenye kitu tunachoita the golden rule of statutory interpretation inayozingatia intention of the framers of that section.

kwa mantiki hiyo lengo la katazo hilo kwa mambo yaliyotajwa hapo juu na kifungu husika ni kama ulivyotaja hapo juu.

lakini kifungu hicho kiko kimya juu ya mambo mengine yote kufanyika nje ya radius ya mita 200 ya kituo cha kupigia kura kwa mfano watu kukusanyika kusubiri matokeo ni jambo halali kisheria, watu kukaa kulinda kura zao ni haki yao kwa sababu haijazuiwa kufanya hivyo.

hebu tujiulize kitu kimoja wasimamizi wakishamaliza zoezi la kuhesabu kura wanatakiwa kutangaza matokeo on the spot sasa kama wapiga kura wameenda kulala majumbani kwao wanamtangazia nani?

watu wanahaki ya kulinda kura zao kwa sababu kura ni mali kama zingine.
tuwahamasishe na ambao hawakujiandikisha waje tulinde kura zetu hawa viwavi ccm wasifanikiwe kuiba hata kura ziliziharibika.
 
Uchambuzi mzur Mkuu, kwa mtazamo wangu sioni haja ya kupiga kura alafu usisubiri matokeo. Ina maana thamani ya mpiga kura inakua imeisha mara baada ya kupga tuu kura??
 
safi sana mkuu kwa tafsiri yako tusubir shauri lililoko mahakama kuu tuone tafsiri sahihi uzuri wa wana ukawa ni watu weledi wenye kufuata misingi ya sheria na sio watu wa vurugu .
 
umeweka mada yako vizuri sana mkuu,tena kwa kiingereza unaipata vilivyo haimkatazi mtu kuwa nje ya mita mita 200.sasa unakuta polisi hadi povu linamtoka anauliza sheria gani hiyo??na Lubuva mwenyewe utadhani sio mwana sheria kajaa woga na hofu tupu hizi hela hila kweli zilimuuza Yesu.Mita mia mbili nitatulia huku nakunywa wine yangu baridiiiiii.hapa hata Tundu Lisu hahitajiki mleta mada na mkuu PTER nimewapata.
 
umeweka mada yako vizuri sana mkuu,tena kwa kiingereza unaipata vilivyo haimkatazi mtu kuwa nje ya mita mita 200.sasa unakuta polisi hadi povu linamtoka anauliza sheria gani hiyo??na Lubuva mwenyewe utadhani sio mwana sheria kajaa woga na hofu tupu hizi hela hila kweli zilimuuza Yesu.Mita mia mbili nitatulia huku nakunywa wine yangu baridiiiiii.hapa hata Tundu Lisu hahitajiki mleta mada na mkuu PTER nimewapata.

Asante Mkuu
 
safi sana mkuu kwa tafsiri yako tusubir shauri lililoko mahakama kuu tuone tafsiri sahihi uzuri wa wana ukawa ni watu weledi wenye kufuata misingi ya sheria na sio watu wa vurugu .

Kuna uzi humu unadai kuwa jambo hilo litamalizwa leo
 
Tutapiga kura tutahesabu mita 200 tutakaa kwa utulivu tutalinda kura
 
Kifungu chenyewe cha Sheria kiko wazi lakini Serikali inakitafsiri visivyo ili kupitisha ajenda zake. Kama kifungu chenyewe hakijitoshelezi kwa mahitaji ya sasa, wapeleke hoja Bungeni kubadili Sheria au Rais atumie 'Presidential decree' tujue moja..
Serikali ikisikia 'Kulinda Kura' inapata hofu sana, sasa tuseme 'Kusubiri Matokeo ya Uchaguzi Mkuu' ili kuwapunguzia hofu..
 
MAAJABU YA VYOMBO VYA DOLA VYA TANZANIA.

Wanawatishia watanzania kupiga kura na kulinda kura kitu ambacho ni haki kikatiba lkn cha ajabu:
-Wameshindwa kuwalinda maalibino(ndg zetu wanauawa)
-Wameshindwa kulinda vituo vya polisi(Vinavamiwa kila wkt)
-wameshindwa kuwalinda twiga wetu wanaopelekwa ulaya
-Wameshindwa kuwapiga na kuwakamata majambazi
-Wameshindwa kulinda raia na mali
-Wameshindwa ht kudai haki zao wanaishi maisha mabaya sn sn.

Wameshindwa mengi lkn ss hv serikali wananunua magari,mabomu na vifaa vya mauaji vya kuwatishia raia kwenye haki yao ya kikatiba ya kupiga kura
#EWE MTANZANIA SIMAMA IMARA,PIGA KURA LINDA KURA#LINDA KURA.
 
Tumesikia waheshimiwa wakisisitiza wafuasi wao wasiondoke walinde kura.

Najiuliza wakati wanalinda watakuwa wanalinda kwa kutumia silaha gani? Hata ukilinda doria ya sungusungu huwa tunakuwa na angalau panga rungu au upinde. Je kura tutalinda kwa kutumia silaha gani?

Haya kura zimeporwa tunafanyaje? Tunaita polisi? Tunawapigia? Au tunapambana na wezi wa kura?

Kama kweli tunadhani wingi wetu ni silaha, je mbona Nkurunziza yuko madarakani? Mbona Morsi kapanguliwa na serikali ingalipo? Mbona Al-bashir yuko madarakani? Mbona Al-Asad yuko ikulu hadi leo?

Tunajidanganya makaburu walimwachia Mandela kwa fujo za Soweto! Tusijidanganye kuwa tutaingia madarakani kwa kuponda watu mawe.

Sote tutakaa mita mia mbili kusubiri matokeo ila tutalindana sisi kwa sisi na tukishikiana mawe tutatoana ngeo sisi kwa sisi na sio watawala. Tufungue macho.
 
Tumesikia waheshimiwa wakisisitiza wafuasi wao wasiondoke walinde kura.


Najiuliza wakati wanalinda watakuwa wanalinda kwa kutumia silaha gani? Hata ukilinda doria ya sungusungu huwa tunakuwa na angalau panga rungu au upinde. Je kura tutalinda kwa kutumia silaha gani?

Haya kura zimeporwa tunafanyaje? Tunaita polisi? Tunawapigia? Au tunapambana na wezi wa kura?

Kama kweli tunadhani wingi wetu ni silaha, je mbona nkurunziza yuko madarakani? Mbona morsi kapanguliwa na serikali ingalipo? Mbona Al-bashir yuko madarakani? Mbona Al-Asad yuko ikulu hadi leo?

Tunajidanganya makaburu walimwachia mandela kwa fujo za soweto! Tusijidanganye kuwa tutaingia madarakani kwa kuponda watu mawe.

Sote tutakaa mita mia mbili kusubiri matokeo ila tutalindana sisi kwa sisi na tukishikiana mawe tutatoana ngeo sisi kwa sisi na sio watawala. Tufungue macho.
Huo ni woga wa usilo lijua... " fear of the unknown " si mara ya kwanza kufanya hivo chaguzi zote tumefanya hivo.... si nchi ya kwanza kufanya hivo nchi nyingi zimefanya hivo na ya karibuni ni Nigeria... kama una INEC na sio NEC, unayo yasema ni murua lakini bila hiyo I kwenye tume yetu.... tutalinda kura zetu wewe gamba na tutapambana na yeyote atakae vunja sheria... sheria ni mita 200 .... na isitoshe hiyo ni police jamii.... tushirikiane na polisi kufanikisha hilo... mbona police ndo wanacho taka na propagate kila mara?.....
 
Kwahiyo nini kifanyike? sheria ya kukaa umbali wa mita 200 ibadilishwe iwe kilomita 200?
 
Nashindwa kuelewa kwa nini CCM tunalalamika watu kukaa mita 200 toka kituo cha kura, je tambo zetu zoooote bado tunaogopa?

Tunajiamini tutashinda sasa basi tuwaache wenzetu wajipange kutetea wanachokiamini, ni haki yao kisheria.
 
Nivigumu kuachia ulichoshika lakini muda haudanganji maana kushikilia daima sitabia ya binadamu muda utakulazimu KUACHIA tu
 
Mikoko kusambaza masanduku ya kimagumashi yenye KURA bandia zilizopigwa tayari, ili wayaache kwenye vituo na kuchukua almasi zenu halali, mlizohangaikia muda wote kwa cheni bandia...yaani chenjikota!

Je, wewe unadhani udhalimu gani mwingine utafanyika? Maana nguvu inayotumika kutuambia turudi nyumbani, magari ya washawasha, haijawahi kutumika kipindi kingine!
 
Back
Top Bottom