Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,347
- 26,153
Kuna mvutano kuhusu mita 200 siku ya uchaguzi na tafsiri yake. Nami najitokeza jamvini kuweka kifungu cha sheria husika pamoja na kuchambua kwa tafsiri kifungu husika. Naweka jambo hili katika jukwaa hili kwakuwa ndilo Jukwaa linalotembelewa na wanaJF wengi kuliko mengine. Nawaomba wakuu moderators mnivumilie kwa hili. Nia yangu ni kuchangia na ikiwezekana kuelimisha.
Sheria husika katika jambo hili ni Sheria ya Uchaguzi wa Kitaifa ( the National Elections Act), Sura Nambari 343 ya Sheria za Tanzania. Kifungu husika ni kifungu cha 104 cha Sheria tajwa. Nakiweka kama kilivyo, katika lugha ya kiingereza, ili ituongoze kuunga mkono au kukosoa tafsiri yangu juu ya kifungu husika. Kifungu cha 104 kinasomeka hivi:
104.-(1) No person shall hold a meeting on election day or within any building where voting in an election is in progress, or at any place within the radius of two hundred metres of such building wear or display any card photograph, favour or other emblem indicating support for a particular candidate in the election.
(2) Any person acting in contravention of this section commits an offence and shall be on conviction to a fine of not less than fifty thousand shillings and not exceeding one hundred thousand shillings.
Sasa twende taratibu. Kifungu cha 104 (1) kinamkataza mtu yeyote kufanya mkutano katika siku ya kupiga kura au kwenye jengo lolote ambamo upigaji kura unaendelea au katika sehemu yoyote ya umbali wa mita 200 kutokea jengo la kupigia kura kuvaa au kuonyesha picha, ushawishi au nembo zozote zinazoonyesha kumuunga mkono mgombea fulani kwenye uchaguzi husika.
Kifungu cha 104 (2) kinatoa adhabu kwa mtu atakayekiuka kifungu cha 104 (1). Adhabu husika, baada ya kukutwa na hatia mahakamani, ni faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na kuzidi shilingi laki moja. Kimsingi, kosa lililoainishwa katika kifungu cha 104 (1) halina adhabu ya kifungo jela.
Kwanza, kifungu cha 104 (1) kinakataza nini? Kinakataza kufanyika kwa mkutano katika siku ya kupiga kura. Pia, kinakataza kuvaa au kuonyesha picha au nembo inayoonyesha kumuunga mkono mgombea fulani kwenye uchaguzi ambao unakuwa unafanyika. Mkutano, uvaaji au uonyeshaji unakatazwa kwenye jengo la kupigia kura na kwenye sehemu yoyote au jengo lililo kwenye umbali wa mita 200 kutoka jengo la kupigia kura.
Kwanini vitu hivyo vinakatazwa? Mosi, kwakuwa muda wa kampeni ulikwisha. Mambo hayo yalisharuhusiwa na kufanyika. Pili, ni kwa ajili ya kulinda amani. Wananchi wanaweza kuvurugana sehemu ya kupigia kura kama watatambuana kiushabiki wa vyama au wagombea wao. Tatu, siku ya uchaguzi, mambo hayo huwa ya kitaifa zaidi. Nne, utulivu. Mikutano ikiruhusiwa siku hiyo na mahali pa kupigiakura, ukimya utapotea.
Iko wazi hadi hapo kuwa, kama wananchi hawatafanya mkutano, kuvaa au kuonyesha picha au nembo zinazoonyesha kumuunga mkono mgombea fulani kwenye uchaguzi husika baada ya mita 200 wanaruhusiwa kuwepo. Wanaruhusiwa kuwepo kuendelea na shughuli zao ikiwa tu hawapo ndani ya mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura. Ingawa adhabu ya kukiuka Sheria ninayoizungumzia hap si kubwa, kinachoogofya ni jinsi ya kukamatwa kwa watuhumiwa.
Nasisitiza kuwa hii ni tafsiri yangu binafsi ya kifungu cha 104 cha the National Elections Act, Chapter 343. Nawashukuru wanaJF. Karibuni kwa mjadala.