Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,667
- 218,171
Wengi tunajiuliza hivi ni nani hasa anayeandaa miswada ya namna hii, anaanzaje kuiandaa, anashauriwa na nani, au anaamua mwenyewe tu, yeye ni nani hasa na huwa anatokea wizara gani , au anatokea ofisi gani , je miswada hii huandaliwa wizarani , ikulu au huandaliwa na CCM?
Nafahamu wengine watasema Miswada yote huandaliwa na serikali , hata mimi nakubali lakini serikali ni pana sana , ni akina nani hasa wanaanda miswada hii ( namaanisha think tank ) , wazo hutolewa na nani na kwanini yeye ndiye atoe wazo hilo na je huwa wanaleta sheria hizi baada ya kuona nini ? bado siamini kama Rais wa Nchi ndiye mtunga miswada , bila shaka wapo wenye kazi yao , je majina yao yanafahamika na wanatokea ofisi ipi , au ni watu wa siri , kwanini ?
Ni vema tukawajua wahusika wa jambo hili ili tuwaweke kwenye kumbukumbu ya milele ya watu walioshiriki kwa moyo mkunjufu katika kudidimiza nchi , hii itasaidia pia kuwaondoa watu wengine wanaolaumiwa kwa mambo yasiyowahusu .
Natanguliza shukrani na naomba kuwasilisha