engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,150
- 1,437
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa halmashauri ya Misungwi, Waziri Magufuli hana mamlaka yoyote ya kuzuia ukusanywaji wa ushuru katika kivuko hicho, na kwamba kamwe agizo hilo hawatalitekeleza, badala yake wataendelea kutoza ushuru huo kwa ajili ya mapato ya halmashauri.
"Waziri Magufuli hana mamlaka hayo ya kutuzuia sisi tusikusanye mapato hapo Kigongo Ferri. Tulimshangaa sana alipotoa agizo lake hilo kwetu.
"Yeye anasimamia sheria, halafu anakuwa wa kwanza kuvunja sheria. Sisi siyo mbumbumbu, ndiyo maana nasema Misungwi tutaendelea kukusanya ushuru Kigongo Ferri, bila kuogopa agizo la Magufuli", alisema mwenyekiti Porcarp kwa kujiamini mbele ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Xavier Tilweselekwa.
Sasa nani mwenye mamlaka hayo? ama kunafisadi akisema huyo ndio mtamwelewa? maana hii nchi bana kila mtu anamamlaka yake,akijisikia tu anaweza hata kumwambia Mh Raisi kuwa huna mamlaka ya kutawala ndiko tunako elekea sasa hivi
CHANZO: Misungwi ‘wampuuza' Waziri Magufuli! | Fikra Pevu | Kisima cha busara!