Misukosuko ya Ndoa na Mshauri wa ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misukosuko ya Ndoa na Mshauri wa ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Mar 2, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,998
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  Ndugu wapendwa

  Leo hii nimekuja kutoa Mawazo yangu kidogo jinsi ya kuokoa ndoa za watanzania,,, leo hii ndoa si kama wazee wetu walivyokuwa wakipendana kutoka moyoni,.... ndo zao leo hii zimejaa madhumuni kibao ambayo mengine yanawekwa kwenye imani yatatokea baada ya ndoa na hatari ni pale mambo yanapoenda kinyume harusi za leo zinaisha ndani ya siku saba,.

  Nimekaa nkaona tusiporekebishana haya mambo hata sie wahudhuriaji makanisani tutaishia kubeba dhambi juu ya awa wanandoa wa leo kama mpenda maendeleo ya wanandoa ningeshauri kuwepo na jukwaa la wanandoa ama kama una mawazo yoyote ama umekumbana na misuko suko ukafanikiwa kuichomoa embu karibu hapa tupe dondoo tupate kushare jinsi ulivyofanikiwa kuhimili vishindo.

  ....wewe msomaji bwana harusi mtarajiwa unakaribishwa kupata hints nini cha kufanya na je baada ya ndoa kuna soln yoyote yakitokea matatizo....

  Nawatakia ndoa njema zenye utulivu,tusaidiane kutoa mawazo endelevu jamani na kusaidia ndoa zetu,..yapo matatizo mengi katika ndoa ,...kama ni mwathirika mmoja wapo karibu jukwani tupate mawazo yako
   
 2. M

  Mundu JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  ...nasema hivi, sometimes inapotokea umri kwenda kombo hasa kwa akina dada, huamua kucheza karata zake zote na kumpata yeyote kwa njia yeyote ili afunge naye ndoa. hapo panakuwa na mapenzi ya uongo kwa ajili ya kupata sehemu ya kujishikizia. Baada ya muda mchache ndoa kufungwa mapenzi huporomoka kama barafu ya juani, na ndio ndoa nyingi za siku hizi.
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Ninatafakari......nina ndoa ya 8yrs lakini mmmmmh kam vileninaenda salendaer kwa manyoya ya paka.
  ......Nitarudi jukwaa likianzishwa. Mx na invizibo mmesikia?
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,998
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  jamani nawaomba wenye uwezo kutuwezesha hili mi nina mengi sana
  hivi natoka salender club kuhojiana na wanandoa tuliowasimamia pale
  azania mwezi wa 11 sasa sijui...nasema sijui kama tutafika tusipoamka
  wenyewe....
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,998
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  nasema hivi, sometimes inapotokea umri kwenda kombo hasa kwa akina dada, huamua kucheza karata zake zote na kumpata yeyote kwa njia yeyote ili afunge naye ndoa. hapo panakuwa na mapenzi ya uongo kwa ajili ya kupata sehemu ya kujishikizia. Baada ya muda mchache ndoa kufungwa mapenzi huporomoka kama barafu ya juani, na ndio ndoa nyingi za siku hizi.


  yawezekana mpwa lakini wakngu imekuwa tofauti
  mi nilikaa na kadada kabichi nkajua nimepata baada ya miezi mitatu nikashtuka nimepatikana baada ya muda nikamwomba mungu anisaidie kabla ya kunionyesha mwanamke alienizidi 2 yrs nina miaka 5 sasa naishi kama niko mbinguni
  mcha mungu aibi,anamjua na kumpenda Mungu hela yake yangu yangu yake we acha tu
  kwangu nikaja kujua age nayo iliniathiri kukimbilia vidogo maana nilikaita kama miaka miwiwli....we acha tu tuzaliwe tuyaone
   
 6. M

  Mundu JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  ...mwanahalisi, kukuzidi miaka 2 haimaanishi kuwa umri wake wa kupata mwenzi ulikuwa umeshapita! Labda utueleze alikuwa na umri gani wakati huo.
   
 7. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huwa imatokea hata mwanaume umri kwenda kombo na kuamua kucheza karata kumpata yeyote ili afunge naye ndoa. Hapo inakuwaje bwana Mundu.
   
 8. T

  Tall JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu kizuri au jambo zuri au tamu duniani kama ndoa, yaani we acha tu.LAKINI hakuna maudhi,mateso,dhiki, unyama, ukatili unaoweza kuupata popote ukazidi wa kwenye ndoa.Waliomo wanataka kutoka na walionje wanataka kuingia.Ndoa ni kama umekata bahati nasibu, lakini huwezi kuichana ticketi baada ya kugundua hukushinda
  Wazo zuri sana la kuanzisha jukwaa la wana ndoa, ndoa nyingi ni NDOANA, mjanja anamvua mwenzie na kwa vile samaki hawezi kuishi nchi kavu muda mwingi, mwisho hufa, hata ndoa ni hivyo hivyo baada ya mikwaruzo mingi mwisho ndoa HUFA
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kwanza naomba nikueleze kwamba ndoa za zamani nilikuwa na matatizo kama za sasa ila ni unyanyasaji na mfumo dume uliwanyima sana haki ya kuhoji wanawake wakati kwa sasa awareness na movement za usawa zimesaidia wanawake kujua na kutetea haki zao... vitu kama vipigo, matusi na masimango kwa sasa vimetungiwa sheria na pia akina mama wanaelimu na wengine wanafanya biashara nk. hivyo relevance ya paragraph one as far as i am concerned ni "qualified"
  hapo tuko pamoja sana, siku hizi ndoa nyingi ni circumstantial na pesa imepata mwenyewe (imeingia kwenye madhumuni ya ndoa, hii ni kwa tafiti kadhaa zhasa ulaya wanaweka haya mamo na sababu zake, kama sikosei...ukisoma Times online kwenye upande wa mahusiano kuna shule tamu sana ya haya mambo

  ndoa has to be made for right reasons, kama sio righ reasons hata ufanyeje haitakuwa right, na solution ni wawili tu!!!

  ushauri ni kwamba divorce ziwe zinaruhusiwa iwapo hakuna right reasons za kuwa pamoja, tusifanye wanawake watumwa kwenye ndoa zetu they have rights too; na akina mama wasifanye wababa mapunda kwenye ndoa kama haiwezekani, then tutambae
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Moja ya wrong reasons kuingia kwenye ndoa
   
 11. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Nasema anzisheni hili jukwaa na liwekewe restrictions kama kule kwa wakubwa; ni muhimu sana!
  Nina mengi ya kushea
   
 12. M

  Mundu JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Labda tujiulize kwanza, nani anakuwa na presha kubwa ya umri kati ya mwanaume na mwanamke?
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  ndoa ni kitu chema na kimeanzishwa na mungu mwenyewe na shetani anapigana sana na ndoa kwani anajua akishavuruga ndoa amavevuruga maisha na familia kwani mwanaume ukishindwa kwenye ndoa utashindwa pi kwenye maisha tunaitaji kujifunza kwanza kuhusu ndoa kabla ya kuingia kupitia vitabu,mahubiri shuhuda nk ikiwa mtu unakwenda kusomea digrii,masters na phd kwa miaka kadhaa inakuwaje unataka kuingia kwenye ndoa wiki moja tu na ufaidi naona hapo ndo shida inaanzaga
   
 14. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145

  mwanamke zaidi
   
 15. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  no comment ww tena nakuaminia
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Naendelea kuwasoma
   
 17. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180

  Kivipi Dr. nasijayasema yalomo moyoni! Weye ni dr kalu nini?:eek:
   
 18. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  kwa hoja mbalimbali hapa kijuweni:)
   
 19. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Nitashukuru kama meseji huwa delivadi
   
 20. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwenda kombo ndio nini?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...