Miss World atua Arusha, agawa Pedi kwa wanafunzi wa Kike

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo,Dkt Harrison Mwakyembe amesema ujio wa Mrembo wa dunia(Miss World)hapa nchini katika jiji la Arusha,Venessa Ponce De Leon utasaidia kuitangaza Tanzania kibiashara ya utalii kupitia kampeni yake ya kuhamasisha matumizi ya taulo za kike kwa wanafunzi wa kike.

Vanessa ambaye ni Raia wa Mexico kwa sasa yuko mkoani Arusha,kwa ziara ya siku NNE ambapo akiwa mkoani hapa amezindua mashine ya kutengeneza Taulo za kike zinazojulikana kwa jina la Uhuru Pads na kugawa taulo za kike 1000 kwa wasichana wa shule ya sekondari Moshono iliyopo katika halmashauri ya jiji la Arusha.

"Changamoto kubwa ya watoto wa kike katika nchi za Afrika ni kushindwa kutimiza ndoto zao za elimu kutokana matatizo ya Hedhi ,tupo katika kampeni za kuwatafutia pedi za kike za kutosha ili wasome wakiwa salama" Amesema Vanessa.

Akiongea na vyombo vya habari Waziri Mwakyembe amesema ni bahati kubwa kwa Taifa kutembelewa na Mrembo wa dunia aliyeambatana na mwanzilishi wa Miss World, Maadam Julie ambao wamekuja kuanzisha kampeni ya mradi wa taulo za kike Zitakazowasaidia watoto wa kike kutimiza ndoto yao ya kupata elimu bila kuwa na shida yoyote.

Dkt Mwakyembe amesema atamshawishi Rais John Magufuli ili taulo hizo za kike ziwe zinauzwa kwa bei nafuu na pia kuwepo kwa viwanda vitakavyokuwa vikizalisha taulo hizo za kike na kusambaza katika shule zote nchi .

Naye mkurugenzi mwendeshaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi amesema hii ni mara ya kwanza kwa Mrembo anayeshikilia Taji la urembo la Dunia mwaka 2018/2019 kuitembelea Tanzania tangu kuanzishwa kwa mashindano ya miss Tanzania mwaka 1994 hapa nchini.

"Nia na madhumuni ya mashindano ya urembo ni kuitumikia jamii katika nyaja mbalimbali jambo ambalo limekuwa likifanywa na warembo mbalimbali" Alisema Basila

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kampuni Uhuru Pedi inayotengeneza Taulo za Kike Sarah Gunda ,amesema kuwa tangu wamezindua mpango huo wa kuzalisha taulo za kike wameshagawa taulo hizo za kike pamoja na chupi zipatazo 4000 kwa wanafunzi was kike katika shele kumi za wasichana Mkoani Arusha.

Amesema lengo ni kuendelea kutengeneza na kugawa bure taulo hizo ziweze kuwafikia wanafunzi wengi zaidi wa kike na kuondoa changamoto walionayo

"Pamoja na kutoa bure taulo hizo za Kike kampuni yetu imekuwa ikitoa elimu kwa watoto wa kike jinsi kutambua mzunguko wao wa hedhi jambo linalosaidia kujitambua na kuepuka kupata mimba za utotoni" Amesema Sara.

Baadhi ya wanafunzi wa kike walionufaika na mpango wa mgao wa taulo hizo za kike ,Glori Mosses amesema kuwa ujio wa mrembo wa dunia utawasaidia kuwapunguzia changamoto za ukosefu wa Pedi kwa watoto wa kike ambao wamekuwa wakikosa masomo wanapoingia kwenye mzunguko w Hedhi.

Pia alishauri taulo hilo za kike zipelekwe pia kwa wanafunzi wa kike waliopo vijijjni ziweze kuwasaidia kuondokana na changamoto inayowakabili pindi wanapokuwa kwenye siku zao.

Ends.....





IMG_20191028_155009.jpeg
 
Kwanini agawe Vitaulo na sio Vitabu?
Huwa ninaamini kuwa kama wanaume wangekuwa wanapata hedhi hata walau mara moja kwa miezi sita, taulo za kike na vifaa vingine vya kujisitiri (ikiwemo vyoo na maji safi mashuleni) vingepatikana kwa urahisi sana na kupewa umuhimu wake. Ila kwakuwa wanawake wamefanya swala la hedhi kuwa siri ndio maana halipewi umuhimu wake kwenye maswala ya kitaifa.

Vitabu ni muhimu na pia kumsitiri mtoto wa kike akiwa kwenye hedhi ni muhimu.
 
Back
Top Bottom