jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,128
- 8,648
Habari,
Katika pita pita zangu za kuanza kujichanganya na kufahamiana na watu kuna member mwenzangu humu,alinipa mwaliko pamoja na ticket ya vip kabisa kwenda kutazama shindano la miss Tanzania.
Naweza kusema hili ndio shindano langu la kwanza kwenda kuona live kutokana na mengi yaliyopitaga kuanzia 2009 kurudi nyuma kuyaona tu kupitia TV.
Hakika nilichokishuhudia kiliweza kuniumiza moyo na hata kuona aibu mbele ya mwenyeji wangu maana kwa jinsi alivyokuwa anasifia na tulichoenda kukiona humo ndani ni aibu kwa wizara ya michezo na burudani na hata kuharibu kabisa taswira ya mashindano haya kitaifa
Kwani tangu tuingie ukumbini kuanzia mishale ya saa 12 jioni mpka tunaondoka ukumbi ulikuwa na watu nusu yani viti vingi mno vilikuwa wazi kiasi cha kufanya baadhi ya watazamaji kuangalia huku wakiwa wamenyoosha miguu kwenye viti vilivyo wazi
Wito wangu kwa Serikali ni kwamba kuna baadhi ya mashindano inabidi yawe yanasimamiwa na serikali sababu impact ambayo itapatkana kupitia mashindano hayo huweza keta faida kubwa kwa serikali hasa kwenye upande wa mapato na kujitangaza hasa vivutio vyetu kupitia mamis walioshinda hasa kwenye kipengele cha kuvutia watalii na wahisani mbali mbali.
Mwisho wa siku Waziri anahojiwa badala ya kujibu wamesapoti vipi kuhusu suala hili anaanza kuongelea masuala ya ndege?
Nitoe kwa pongezi kwa mis Tanzania
Sylivia sebastian,ambae alitwaa taji hilo kwa kujinyakulia kitita cha 10m pia nitoe pongezi na pole kwa kampuni ya The look iliyoandaa shindano hilo,kwa kupata hasara kubwa ya kuwekeza kwenye shindano hilo mwisho wa siku watu hakuna,na pia pongezi za dhati kwa kuonyesha uzalendo na moyo wa dhati wa kudhamini mashindano hayo.
Wito kwa serikali yangu,hasa wizara ya utamaduni na michezo ni kuwaomba wasapoti mashindano mengine mbali ya mpira wa miguu kwani wizara hii ya michezo na utalii wakiwa wabunifu wanaweza kuwekeza kwenye michezo na kuleta impact kubwa sana katika uchumi hasa kwenye kutangaza nchi na vivutio vyake kama zifanyavyo nchi za wenzetu.