Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na mama yake wahamia CHADEMA kutoka CCM

Aisee, hatari sana. Wanakatika haooo.

Tz kuna majina, kwa mfuga mbwa, kwa mfuga kuku, kwa mfuga majini, kwa mfuga fisi nk sasa tena tuko na kwa mfuga.... waliotimuliwa wote na mama mtu kumbe leo wametia timu kilingemi kabisa.
.

Na washawasha!
 
Wema, tenda wema uende zako, mbona ulitaka wakumbuke wema wako uliowafanyia wakati wa kampeni?
 
Kafanya uamzi mzuri,kila mtu ana uhuru wa kuhamia chama chochote,wakati wowote,kama watamfunga kwa kuhamia huko wamfunge tu,tujue mmoja,
lakini mtu hawezi kujinyima uhuru wake eti kwa kuhofia kuiudhi mijitu fulani....
 
Habari: Miss Tz 2006, Wema Sepetu na familia yake watakuwa na Press Conference Saa 5 asubuhi nyumbani kwao Sinza-Meeda.

Waandishi wote wanakaribishwa.

Hiyo ndiyo meseji ya kutoka kwa akina Wema wenyewe kwenda kwa waandishi Asubuhi hii.

=======



Update: 1337hrs: Bado anasubiriwa Wema Sepetu hajafika, wanafamilia wengine akiwemo Mama yake na Baadhi ya viongozi wa CHADEMA ndo wapo.

Wema Amewasili na Kuanza Kuongea kama ifuatavyo:

⁠ ⁠Mama wema: Habari za mchana, nawakaribisha

⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Kwa jina naitwa Wema Sepeti Isack Abraham
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Naomba mnisamehe kwa kufika kwa kuchelewa
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Sitakuwa na mengi ya kuongea, nataka kutoa tamko moja kutoka kwa Wema mwenyewe
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Nimewaiteni hapa kuja kutamka rasmi kwamba hivi sasa nataka kuhamia Chadema kutoka CCM
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Sio kwa tuhuma zinazonikabili bali nmefanya maamuzi kama mtu mwingine yoyote

⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: Nyote mnajua nlikuwa kada wa ccm na nmepigania chama kwa uwezo wangu wote
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: 2015 niligombea ubunge viti maalum Singida na kura hazimutosha na sikufa moyo
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Marehemu baba yangu alikuwa kada nguli wa CCM na alipata kuwa hadi mshauri wa Zanzibar, Waziri na Balozi wa Urusi. Amekufa akiwa CCM

Wema: Nimetuhumiwa hivi karibuni, wakati najitoa kwa hali na mali ndani ya CCM na nliamini hawatanitupa na haina maana kwamba nilitaka kubebwa hapana
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Kilichotokea kwangu kilikuwa ni uonevu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Nimetafakari sana kwanini hili limetokea
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Kama mwanachama kimenivunja moyo. Tenda wema uende zako usingoje shukurani

Wema: Mimi naamin katika demokrasia. Nmefanya reseach yangu na hata wakati wa kampeni CHADEMA ilitupa tabu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠CHADEMA inapigania demokrasia na mimi nataka uhuru wa watu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Ningejua mapema ningeniunga CHADEMA zamani. Najilaumu sana kuchelewa kujiunga CHADEMA

Wema: Bado sijachelewa kufanya maamuzi. Na hii najua nimeingia kwenye vita na naamini watu wengi wapo wananiunga mkono
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Dola ifanye kazi zake na kifuata sheria kama dola. Ila wazingatie haki za binadamu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Naamini ndani ya CHADEMA tunaweza kuleta mabadiliko nchini
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Kwa kupitia nguvu ya CHADEMA tunaweza pata ule uhuru tunaoupigania.
nenda bibi nenda hatutaki mateja kundini
 
Wema aseme kama kweli 'alitongozwa' na kilichofuata.

Wanawake kutongozwa si ajabu, wengine wanatongozwa wanakataa, wengine wanatongozwa wanakubali na mpaka wanazalishwa watoto ambao wajomba zao ndio wanakuwa baba siku za ubatizo, wapo wapo wengi tu, wote hawa wakisema kweli itasaidia nini nchi? Au tuchague waseme wale waliotiongozwa na wanachama wa CCM tu, tuwaache wanachama wa CHADEMA, ACT na CUF? Au waseme wooote, wooote kabisa?
 
Safari njema,, chema kitaendelea kujengeka,, kuna neno kujihusisha uswahiba na mashoga,, imesikika na mama mzaz hakuikana,, amethibtsha kwa kusema ameshawafukuza,, swalii,, unahisii kujenga uswahiba na mashoga ulilenga kutuvutia na ss tuingie,, then?? Jitafakari ndg kjana mwenzetu, kuna watu /vjana wanafatlia life style yako,,, be smart acha kutapatapa
 
Kaona Mbali sana, na ubunge atapata tu, ccm kuweni makini sana na siasa za kuchafuana, we unafikiri hapo wangapi wataanza kuwazia chadema, mtaji wa chama kushinda ni ushawishi katika Jamii yeyote ile
 
HAPA NDIPO ILIPOFIKA CHADEMA!
HAPA!PA BENDERA YAKE KUVALIWA KAMA ANJIFU YA MIA NA KUTUMIKA KWA STYLE HII!
YES!NI HAPA!


AHSANTE SANA FREEMAN!
KWELI CHAMA NI CHAKO
SIPATI PICHA EDWIN MTEI ANA HALI GANI HUKO ALIKO
ANGALIENI MSIJE KUMKOSESHA LILY BABA!
YALE MNAFANYA NOW DAH!
 
Hivi chadema hakuna wenye akili siku hizi?Au siku hizi ni Chadema-madawa ya Kulevya?
Mnafikiri mnamkomoa Magu?
Sio kwa siasa nyepesi kama hizi!
Yaani Wema mnamuandalia jukwaa?
Mnafikiri headline mtakazopata kwa Wema zitadumu kwa siku ngapi?
Nitafurahi sana siku Wema akiondoka huku akiwatukana matusi ya nguoni!
Itikadi hamna siku hizi?Wema anaifahamu?ataifuata?
Nyie kwenu ni bora tu kuwa na watu bila kujali kiwango cha ukichaa?
Ninasikitishwa sana na upuuzi huu
INAUMIZA KUSEMA UKWELI!
hata kama ukitka kupuuzia kiasi gani!
 
Back
Top Bottom