Miss jf

JF2050

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
2,085
Reaction score
45
Ndugu zangu wapendwa,


Nimeona litakuwa ni jambo jema ikiwa tutafanya mpango wa "kuorganize" shindano la kumtafuta Miss JF. Kama mnavyojua "JF is the Home of Great Thinkers", pamoja na mapungufu ya baadhi ya wanachama hilo bado haliwezi kuifanya Jf kukosa hadhi hiyo.

Nimefikiria itakuwa ni vizuri kama Miss JF atapatikana kwa kuangalia misingi kama vile uadilifu wake, michango yake na mawazo yake chanya katika kujenga, kuelimisha, kufundisha, kuwajibisha na kuonya kama viashirio vya kujenga jamii inayojitambua, inayojiheshimu na yenye mahusiano mazuri kuanzia ngazi ya familia hadi taifa katika nyanja mbalimbali za kimaendelao, kielimu, kiuchumi na kiustawi.

Sio vibaya pia kama uzuri wake ukawa ni kitu cha ziada, ikiwa tu utahusianishwa na sifa nilizoziainisha hapo juu. Lakini uzuri lisiwe ni jambo la kutilia maanani sana kwa sababu mwanamke ni tabia.

Kwa kifupi, tutafute mwanamke humu Jf ambaye anaweza kuwa mfano wa kuigwa katika jamii. Shindano hili litachangia sana katika "kupromote" tabia njema Jf.



Wadau mnalionaje hili wazo? Tutauomba uongozi wa Jf umpe mshindi alama fulani kwenye profile yake (alama yoyote ya kumtambua kama 2013 JF lady), labda kitu kama diamond member n.k. Ikiwa tunataka kwenda mbali zaidi hili shindano linaweza kufanyika kupitia media kama TV!


Kama tumeridhia basi ni vizuri tukaanza kutoa mapendekezo yetu, nani anafaa kuwa Miss JF 2013, yakiambatana na sababu mbili tatu!
 
Sio vibaya pia kama uzuri wake ukawa ni kitu cha ziada, ikiwa tu utahusianishwa na sifa nilizoziainisha hapo juu. Lakini uzuri lisiwe ni jambo la kutilia maanani sana kwa sababu mwanamke ni tabia.
huo uzuri unaousema tutaujua vipi,au hili ni shindano la uso kwa uso jukwaani,,,,,,,,kama hiki kigezo kikitumika utamjuaje Asnam ni mzuri,au tutabase kwenye imagination?
muongozo tafadhari!!!!!!!!
 
huo uzuri unaousema tutaujua vipi,au hili ni shindano la uso kwa uso jukwaani,,,,,,,,kama hiki kigezo kikitumika utamjuaje Asnam ni mzuri,au tutabase kwenye imagination?
muongozo tafadhari!!!!!!!!

Tutaangalia Avatar............
 
^^
Wazo ni zuri,,changamoto kubwa ni ukubwa wa JamiiForum yenyewe.
Kuna watu tupo selective sana na majukwaa kiasi hatuwajui wengine.
Kwa MMU nitapiga kura wakati ukiwadia Simplicity
^^
 
Last edited by a moderator:
I find it very difficult,nani anapiga kura???Watajuaje hiyo michango chanya hapa Jf???Members wapo wa longtime kitambo ambao leo wanaonekana kwa nadra sana na michango yao haitakumbukwa kirahisi,wale wageni watapa faida ama waliokaa muda sana humu,anyway ngoja nisubirie.
 
Tutaangalia Avatar............

itakuwa sio fair kwa sababu kuna watu wameweka avatar nzuri sana lakini hawana sifa za kuwawezesha kushinda tofauti na yule mwenye avatar ya ajabu ajabu,,,,,,kuna suala la ushabiki pia nalo ni tatizo kuna watu wanaongea pumba na wana wafuasi wengi utashangaa na roho yako akalitwaa taji huku vigezo na masharti vikiwekwa pembeni.....all in all i will caste my votes to any one deserving my vote.
 
wazo zuri! apatikane mwenye mawazo na mtizamo chanya, anayejiheshimu, mwenye kusimamia mawazo yake ! mi naanza na lara 1
 
Last edited by a moderator:

maana mie mwenyewe nimejiuliza kuujua uzuri wa Sura itakuwaje!!!!!!!!!nikahisi

labda tutatumia avatar zetu.......ngoja nione mawazo ya Simplicity yakojeeeeee na hii MISS jf
 


Kwa mtazamo wangu zoezi hili litaingia dosari la kupendeleana. Kama hujagundua humu JF kuna kakikundi ka urafiki fulani ambapo ndipo hupeana nakala na kutaja majina kila wakati, kuna watu wanapost humu karibu kila siku lakini huwezi kukuta wamepewa nakala (cc) hata siku moja ila ni wale wale..... hii italeta shida kumpata huyo miss. Mfano uliohai ni hao uliowacopy hapo juu ina maana hakuna wengine humu? bila shaka hata miss atatoka humo humo! ------------------- huu ni mtazamo wangu tuuuuuuuuu
 
Asnam kigezo cha uzuri amesema kitumike kama kitu cha ziada, hvyo akaweka MISINGI ya huyo atakaechaguliwa.. Mshinga sidhani kama kijana wa zamani leo anaweza kuwa miss labda kama tungekuwa tunawashndanisha kwa uzuri wao wa kitambo hcho.. Simplicity hzi kura as znapgwa waziwazi zitagombanisha watu labda ufanye mpango wa kura ya siri (walau kwa members hapa na public)
 
Last edited by a moderator:
Acheni KUZUNGUKA MBUYU! Tajeni KURA YAKO INAENDA KWA NANI? TOP 5, ZINAPIGWA TENA TOP 3, AFU MSHINDI!!!!!!!!!!

Top 3 nawaalika MMU Exclusive tujadili bei yao! DALALI NISHAPATIKANA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…