Misri: Morsi akaidi amri ya jeshi

mwitaz

JF-Expert Member
Feb 19, 2012
315
93
Katika hatua ya kulikaidi
jeshi lenye nguvu nchini
Misri, rais mpya Mohammed
Morsi, ametoa amri kuwa
bunge likutane. Amri yake inakwenda
kinyume na hukumu
iliyotolewa mwezi uliopita
na mahakama ya katiba,
kwamba bunge la sasa
siyo halali. Bunge hilo lina wajumbe
wengi wa vyama vya
Kiislamu. Hukumu ya mahakama
ilitekelezwa na jeshi,
ambalo lilifuta bunge na
kujipa madaraka ya
kutunga sheria. Televisheni ya taifa
inasema halmashauri ya
jeshi itafanya kikao cha
dharura kujadili amri ya
Rais Morsi.

Source: BBC SWAHILI
 
Back
Top Bottom