Mishahara ya watumishi yazidi kupaa

Mishahara ya watumishi yazidi kupaa

Bornventure

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2017
Posts
529
Reaction score
523
Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania inaonyesha kuwa mishahara imeongezeka kwa takriban Sh31 bilioni kwa miezi 12 iliyopita.Ripoti hiyo inakuja wakati ambapo sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma nchini humo ikionyesha ni watu 6,099 pekee ambao wameajiriwa ndani ya miaka mitatu iliyopita.

Ripoti ya tathmini ya hali ya uchumi ya kila mwezi inayotolewa na BoT inaonyesha mwezi Oktoba, Serikali ilitumia Sh553.3 bilioni kulipa mishahara, ikiwa imeongezeka kutoka Sh522.4 bilioni zilizolipwa Oktoba, 2017.

Ripoti hiyo ya Novemba inabainisha kuwa katika mwezi huo, Serikali ilikusanya Sh1.3 trilioni Oktoba huku ikitumia Sh1.5 trilioni. Katika kiasi kilichotumika ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 22.1, Sh893.4 bilioni zilikuwa kwa matumizi ya kawaida na Sh635 zilitekeleza miradi ya maendeleo. Kati ya fedha za miradi, asilimia 72.6 zilikuwa mapato ya ndani.

Mishahara ya watumishi wa umma ilikuwa ni zaidi ya nusu ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida katika mwezi huo. Makadirio yanaonyesha kuwa Sh553.3 bilioni ikiwa imepanda kutoka Sh522.4 bilioni zilizolipwa mwezi kama huo mwaka jana, sawa na ongezeko la Sh30.9 bilioni.

Mishahara hiyo imeongezeka katika kipindi ambacho katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Xavier Daudi anasema ajira zilizotolewa ndani ya miaka mitatu iliyopita zilikuwa sawa na asilimia moja ya walioomba.

Sio mishahara pekee iliyoongezeka, ripoti inaonyesha mauzo ya mazao ya biashara nje ya nchi na mapato yatokanayo na huduma hasa za usafirishaji na utalii yaliongezeka pia ndani ya kipindi hicho. Webradio
Sauti
6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
 
Imeongezekaje hio mishahara wakati watumishi wanalalamika muda.mrefu na Rais alisema wasubiri kabla hajamaliza urais ndio ataongeza
 
Imeongezekaje hio mishahara wakati watumishi wanalalamika muda.mrefu na Rais alisema wasubiri kabla hajamaliza urais ndio ataongeza
Unaweza kuongezeka wakati hayupo madarakani.
 
Huyu mtoa mada inayohusu. Watumishi wa umma kua waliongezewa mishahara 2017-18 no mwehu labda aliongezwa yeye.
 
Sasa nchi inaendeshwa bila katiba wale sheria. Ni hatari mno.
Tutofautishe vitu viwili.
1. Kupanda kwa mshahara, na
2. Ongezeko la kila mwaka au annual increament kufuatana na daraja la Mtumishi.

Pombe amegoma kupandisha mishahara. Yaani kwa mfano mwenye mshahara wa laki kuupandisha hadi laki 7 kwa mfano.

Lakini kitu cha ajabu na kinyume cha sheria na kanuni za nchi kasitisha annual increament ambayo huwa automatic mwaka mpya wa fedha. Kama mtumishi hakupanda cheo, hilo ongezeko ni lazima hadi afikie ukomo.

Kuzuia annual increament ni kukiuka sheria za nchi. Rais hayupo juu ya sheria.
 
Ingekuwa busara wale watumishi wa umma wanaoondolewa kwenye nafasi za uongozi warudishiwe mishahara yao ya zamani. Kuendelea kuwaacha wafaidi mishahara hiyo huku kazi wanazofanya ni za mishahara midogo ni upotevu wa rasilimali fedha, kwani yule mpya anaeteuliwa nae atalipwa mshahara mrefu.
 
Ingekuwa busara wale watumishi wa umma wanaoondolewa kwenye nafasi za uongozi warudishiwe mishahara yao ya zamani. Kuendelea kuwaacha wafaidi mishahara hiyo huku kazi wanazofanya ni za mishahara midogo ni upotevu wa rasilimali fedha, kwani yule mpya anaeteuliwa nae atalipwa mshahara mrefu.
Huu ni wivu sasa.
 
Mei Mosi 2019 nikiwaona watumishi na mitisheti yao ya buku mbili wamemebeba mabango ya : BABA SEMA NENO MOJA NA ROHO ZETU ZITAPONA nitasema tumerogwa na Sind Bad
 
Huu ni wivu sasa.
Hao ndio wanaofanya watumishi wa umma waonekane wanavuna pesa nyingi, regardless ya kuondoa wenye vyeti feki, watumishi hewa n.k bila kuwapunguzia hao, zigo la mishahara bado litabaki kubwa. Kuwa mzalendo wa nchi yako
 
Back
Top Bottom