Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Kwa vile wafanyakazi Benki Kuu wanastahili maisha ya juu kama ya wale wa Benki za nchi zilizoendelea na wabunge wetu nao wanastahili maisha kama ya wabunge wa nchi zilizoendelea; na kwa vile wapo watu wanaostahili katika utumishi wa umma maisha ya kimagharibi.. naomba kuuliza je madaktari wetu wanalipwa mishahara inayolingana na madaktari kama wa nchi za US na UK?
Je itakuwa vibaya kama na wao wakiamua kudai "mastahili" yao kutoka kwa watawala?
au hawastahili nyumba nzuri zenye mabwawa nje na magari na posho kubwa zaidi? Labda niulize tu kwa wastani daktari wa Tanzania analipwa kiasi gani na kiasi kinalinganishwa vipi na daktari wa US.
Sasa Hivi watakuja na kusema wewe mchochezi. Serikali haina priorities.Ma-klassmate wangu walimalinza interniship mwaka jana hapo Mbeya Referal hospital,wakapata ajira hapo hapo,two months later wakaacha kazi,shida,wamechoka kuandamana kudai mishahara. Hadi "wapachimbe" ndo kieleweke.
Inasikitisha.Ubinasfi,kushibisha matumbo ndo vitu vinavyowamaliza watanzania.Angalia mshahara wa Dr. pale Rwanda.What goes around comes around, wanakwiba ili wajenge,wakatibiwe nje. It is a failed social security system. Vitambi, Diabetes, Hypertension, Hyperlipidemia, Sedentary life, Nyumba ndogo...........list goes on vitawamaliza. Even how much you steal,you will end up in cheap hospitals in India not even in South Africa.Guess what,you will die at the end.
Hapa sina la kuongeza, maana ujumbe wako ni mfupi lakini umejitosheleza kila kona.the list will end to mention all professional ila la msingi ni moja, watu walipwe kulingana na mazingira ya nchi na hili lianzie kwa viongozi wa serikali mpaka mfagiaji ktk ofisi ya umma, ukweli uko wazi serikali haiwezi kulipa mishahara kama ulaya, kulazimisha ivyo ni kama kuiambia serikali ifanye miujiza!
uzalendo ndio kitu cha muhimu kuliko vyote! we need to change people mentality especially hawa viongozi wetu wanaoishi maisha ya kuigiza!
Kwa vile wafanyakazi Benki Kuu wanastahili maisha ya juu kama ya wale wa Benki za nchi zilizoendelea na wabunge wetu nao wanastahili maisha kama ya wabunge wa nchi zilizoendelea; na kwa vile wapo watu wanaostahili katika utumishi wa umma maisha ya kimagharibi.. naomba kuuliza je madaktari wetu wanalipwa mishahara inayolingana na madaktari kama wa nchi za US na UK?
Je itakuwa vibaya kama na wao wakiamua kudai "mastahili" yao kutoka kwa watawala?
au hawastahili nyumba nzuri zenye mabwawa nje na magari na posho kubwa zaidi? Labda niulize tu kwa wastani daktari wa Tanzania analipwa kiasi gani na kiasi kinalinganishwa vipi na daktari wa US.
polisi,walimu na manesi wanapata(kianzio) £18,000
Nimekugongea senksi kule !!Na wahandisi je??????????