Miaka50ya UHUNI
Member
- Oct 5, 2011
- 21
- 2
Katika kuhakikisha kuwa serilkali inaondokana na tatizo la watumishi hewa serikali imedhamiria kulipa mishahara ya watumishi
kupitia dirishani kuanzia mwezi huu.Je,ni njia sahihi ya kubaini watumishi hewa?[/QUOTE
Kikwete nae achukulie mshahara dirishani kwani na ni mtumishi hewa(NEC appointee)
Halfcaste, kwanza sio kweli kuwa serikali sasa ndio imeamua kulipia mishahara madirishani kuanzia mwezi huu, bali hili ni zoezi la kawaida ambalo hufanyika japo mara moja kwa mwaka/miaka 2 etc kwa serikali kulipia mishahara madirishani ili maofisa masuhuli, (accounting officers) wajiridhishe kwa kuwahakiki watumishi wao. Baada ya uhakiki, utaratibu wa kawaida huendelea!.Katika kuhakikisha kuwa serilkali inaondokana na tatizo la watumishi hewa serikali imedhamiria kulipa mishahara ya watumishi
kupitia dirishani kuanzia mwezi huu.Je,ni njia sahihi ya kubaini watumishi hewa?
......hata sisi wafanyakazi feki tutaenda kuwachukulia mishahara wahasibu kwa kutumia vitambulisho feki......
Katika kuhakikisha kuwa serilkali inaondokana na tatizo la watumishi hewa serikali imedhamiria kulipa mishahara ya watumishi kupitia dirishani kuanzia mwezi huu.Je,ni njia sahihi ya kubaini watumishi hewa?
Yah mimi binafsi naona kuwa hili linaweza kuwa jambo la msingi sana kwani litapunguza kulipa watu hewa lkn kama kawaida ya watanzania wengine wao wanawaza namna ya kuila hiyo hela itakayobaki, kwa hivyo watakachokifanya hapa ni kwamba wahasibu ndio watakaokula hiyo hela, wao wanajua watailaje watacheza dills na wakubwa wengine na watu watashangaa kusikia tena kuwa bado mishahara mingi imeliwa
Nakumbuka kipindi serikali inabadili mfumo wa kuwatoa walimu wa sekondari kwa katibu mkuu moe na kuwaleta katika halmashauri,kulikuwa na majina mengi sana ambayo yalipo pelekwa katika halmashauri,hayakujulikana ni wakina nani,na wakaendele a kuyaandalia mishahara kila mwezi,hayo majina yalikuwa ni feki toka kwa wahasibu wa wizara ya elimu,waliyaandalia taarifa za uongo kwa kusingizia mikoa fulani na kujikwapulia mahela kila mwisho wa mwezi,lieni na wahasi na sio na watumishi...
Mimi ni Mhasibu Serikalini, kwa uamuzi huu serikali imekula kwao maana kama kawaida yetu malipo yoyote yanayobaki ambayo beneficiary wake hawajatokea huwa tunasaini sisi wenyewe kwa kutumia Mkono wa Kushoto! Unaangalia jina kwenye Pay List linasomekaje then unatafuta saini inayoendana na jina hilo kwa kutumia mkono wa kushoto!
Huu ni upuuzi mtupu tena kuiba mshahara kwa dirishani ni rahisi kuliko benki, Pia hii njia italeta usumbufu mkubwa kwa watumishi kwa mfano mtumishi ambaye yuko likizo bukoba na anafanya kazi dar inabidi aache likizo afuate mshahara tu, mtumishi ambaye yuko masomoni anapataje huo mshahara? Mtumishi iliyelazwa hospitali mbali na kituo chake cha kazi inakuwaje?
Katika kuhakikisha kuwa serilkali inaondokana na tatizo la watumishi hewa serikali imedhamiria kulipa mishahara ya watumishi
kupitia dirishani kuanzia mwezi huu.Je,ni njia sahihi ya kubaini watumishi hewa?
Watumishi hewa wanapatikanaje? Katika mfumo wa taasisi yeyote kuna kurugenzi, idara na vitengo vyote vikiwa na wakuu wake; kusema kwamba kuna wafanyakazi hewa inamaanisha wakuuu wa vitengo, idara na kurugenzi hawajui watumishi walio chini yao?
Naweza kusema jibu ni HAPANA; kila mkuu wa kitengo au idara ya taasisi ya umma anafahamu watumishi walio chini yao hivyo swala la kuwepo watumishi hewa ni "syndicate" pengine kuanzia huko mishahara inakotengenezewa yaani hazina mpaka inakokwenda kulipwa. Iweje kampuni binafsi zenye wafanyakazi zaidi ya 1000 wasiwe na wafanyakazi hewa iwe tuu serikalini?
wameghairi wamesema mwezi huu wanalipa kawaida yaani kupitia mfumo wa account