Dowans nayo ilipwe dirishani. Kwani dirisha lina nini? Watanzania tu wajinga kabisa.
SERIKALI imetangaza kuwalipa watumishi wa umma mishahara yao kupitia madirishani kwa muda wa miezi miwili.
Katika kipindi hicho, itachukua hadhari zote ikiwamo ya kuhakikisha hakutokei uporaji mishahara hiyo ili kuwagundua watumishi hewa wanaotafuna fedha za umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, alisema hayo juzi mjini hapa kwenye mafunzo ya maboresho ya utumishi wa umma awamu ya pili.
Utaratibu wa kuwalipa watumishi madirishani utakuwa wa muda tu, angalau miezi miwili tu. Nia ni tuwatambue, tusiowaona, tutawaondoa kabisa, alisema Ghasia.
Alisema, ulipaji huo wa mishahara utawezesha kugundua watumishi hewa na kutolea mfano wa uhakiki uliofanywa katika shule za sekondari, ambako moja ilielezwa kuwa ina walimu 17, lakini ikakutwa na walimu wawili na nyingine walimu 70, lakini ukweli ilikuwa na walimu 20.
Kuhusu uboreshaji wa maslahi ya watumishi ikiwamo mishahara, alisema Serikali itaendelea kuiboresha kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.
Akiwa kwenye mafunzo hayo, Ghasia aliwataka watendaji wa halmashauri kusimamia vema fedha ili kuondoa mawazo kuwa halmashauri zimejaa wezi.
Kuhusu ajira, alisema kuanzia sasa mtu atakayefaulu usaili wa kazi katika utumishi wa umma na kupangiwa kituo cha kazi, hataitwa tena katika usaili wa kazi yoyote serikalini.
Alisema hiyo ina nia ya kukabiliana na watu ambao wanapewa kazi, lakini wanakwenda kuripoti vituoni na kuchukua fedha za kujikimu, kisha kutoweka.
Waziri Ghasia yuko katika ziara ya mafunzo kuhusu mabadiliko ya utumishi wa umma awamu ya pili na jana alitarajiwa kuwa Misenyi.
nimeiweka hii habari ili nijue je ni njia sahaha ya kubaini wafanyakazi hewa?kwasababu miaka kama 4 iliyopita wafanyakazi walikua wanachukulia dirishani na bado kulikua na wafanyakazi hewa kibao
mawazo ya huyu mama yapo miaka kumi kabla,amabayo ni hatari zaidi kwani hata majambazi yanaweza kukomba hela zote
Jamani walio karibu wamsaidie haiwezekani kulipa kwenye dirisha iwe ndiyo njia ya kubaini ambao hawapo
na hii inadhihirisha kuwa hata wizara haijui ina wafanyakazi wangapi kwa secta zote za serikali
Tumia hata huu ushauri wa Wayne
Serikali ilianza vizuri kupitisha mishahara benki,controls zilizopo benki are much more stronger than those wanazopendekeza, ni suala la kutoa maagizo kwa wakuu wa idara na taasisi za serikali kuwasilisha physical stock ya watumishi waliopo kwenye vituo, then you compare payrol, stock list na account zinazotumika kulipia hiyo mishahara, zoezi hili likiwashirikisha branch managers wa mabenki husika, then you get the variance ambayo lazima ipo.
mwenye cv yake atupe tafadhali. naona kama hamnazo vile na pia kaota usiku ndo kaamua kutangaza hili jambo nadhani IQ yake sawa na zero
Mkulu
Heshima mbele,nakubaliana na wewe kwa asilimia 100.Tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele, hivi kweli tumeshindwa kubuni njia mpya ya kubaini watumishi hewa kuliko kurudi kwenye njia za zamani ambazo ndizo zilikuwa chanzo kikubwa cha watumishi hewa.Unapofanya maamuzi kama yaha,you need to consider ukubwa wa serikali kwa sasa kwa maana ya number ya watumishi,serikali imeajiri watumishi wengi mno kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita ,kitu ambacho binafsi sina shida na hilo kwani ililenga kuboresha huduma kwa umma.
Kulipa dirishani ni ku-create mkanganyiko zaidi, my take ni kwamba zoezi zima halita-yield results wanazotegemea kwani ni watu wa zamani au wenye mawazo ya kizamani waliopendekeza njia hii ya kizamani.
KIPI KINGEFANYIKA:
Serikali ilianza vizuri kupitisha mishahara benki,controls zilizopo benki are much more stronger than those wanazopendekeza, ni suala la kutoa maagizo kwa wakuu wa idara na taasisi za serikali kuwasilisha physical stock ya watumishi waliopo kwenye vituo, then you compare payrol, stock list na account zinazotumika kulipia hiyo mishahara, zoezi hili likiwashirikisha branch managers wa mabenki husika, then you get the variance ambayo lazima ipo.
Utaratibu huu unakuwa unaufanya periodically.
Wakati mwingine ukiona watu wanafanya maamuzi kama haya unapata picha ni watu wa aina gani tulionao ...