Mishahara New Habari tatizo kubwa

Mishahara New Habari tatizo kubwa

makamaka

Member
Joined
Dec 1, 2011
Posts
55
Reaction score
28
New habari Kunani?

Ndugu zangu wale wenye mawasiliano na ndugu Rosatm Aziz tunaomba mmfikishie ujumbe huu.Sisi wana familia ambao ndugu zetu wamekuwa wakifanya kazi katika kampuni hiyo ya uchapishaji wa magazeti ya Mtanzania tunaishi maisha ya dhiki kwelikweli,mme wangu ameikimbia familia yake na kuniacha mimi na watoto ambao wote wamerudishwa kutoka shule kwa ukosefu wa ada.

Mzazi mwenzangu anadai sasa ana miezi ipatayo sita hajalipwa mshahara wake pamoja na muda wake wote kuutumiaakiwa katika kampuni hiyo.ninasikia kuwa mmiliki wa kampuni hiyo ni ndugu Rostam aziz.Baba tunakuomba kama kweli kampuni hii ni yako okoa jahazi.Watanzania wenzako hasa hawa watoto wasio na hatia wanateseka sana.

Mlipeni mwenzangu aweze kuwasaidia watoto wake na familia kwa ujumla irudi pamoja.Watoto sasa wana wiki nzima hawajagusa shule na hakuna matumaini yeyote kama wataweza kurudi shule.
 
Kiukwel hali ya biashara kwa sasa n mbaya kampun nying znapunguza wafanyakaz n juz tu gazet pendwa la mwananchi limepunguza wafanyakaz kuna haja kuwe na mjadala wa kitaifa juu ya muelekeo wa uchumi s ajabu pia watu wakabeza hili wakakwambia nyie n miongoni mwa wapiga dili wa awamu iliyopita kwamba mlinufaika na mfumo uliopita japo mm napinga sana hili MAONI YANGU 2020 ipo jirani tusikwepeshe tuwamalize hawa watatuua tukiwapa miaka 5 mingne huyo ROSTAM AZIZ mwenyewe kanyosha mikono juu kama mateka kurudi kwa JIWE hali n tete hasa MEDIA INDUSTRY kama magazeti bora kidogo radio na TV
 
kama kwenye familia chanzo cha kipato ni mzazi mmoja kusomesha shule binafsi ni ujinga. mpeleka kayumba akasome bure ili usimtese mtoto.


mwandalie mazingira ya uwekezaji pindi anahitimu anaendesha miradi.


sio umlipie ada bei mbaya ahitimu mkae mnatazamana.



nikirudi kwa new habari, anayedaiwa ni new habari kama kampuni na sio kachelo rostom.



hali itakuwa tete 2021-2022. mabeberu sio wa kawaida.
 
Kiukwel hali ya biashara kwa sasa n mbaya kampun nying znapunguza wafanyakaz n juz tu gazet pendwa la mwananchi limepunguza wafanyakaz kuna haja kuwe na mjadala wa kitaifa juu ya muelekeo wa uchumi s ajabu pia watu wakabeza hili


Jana tu kule Mbarali amesema tupo kwenye mwelekeo mzuri kabisa
 
Ogopa kuwa na mkuu wa kaya wa kujifungia chumbani kwake bila kupata mawazo mbadala ya majirani! Ukweri ni kuwa ataamini kuwa,hata watoto wakibaki na nguo moja yeye ataona mambo safi kwa sababu haoni watoto wa majirani wanavyovaa nguo na kupendeza. Maendeleo hayaji kwa baba kusema nataka iwe hivi au vile na ikiwa Bali ni mipango mchanyato na madhubuti,hapo ndo utaonana na bwana anayeitwa maendeleo ambaye atafanya hata watoto wako Wawe na sura za kug'ara na furaha tele maana watavaa nguo nzuri hata wakitaka kununua pipi au kitumbua wataweza kwa sababu umewawezesha kuwa na visenti!!!!
 
Kweli jamani hali ni mbaya sana sio hapo tu,kama nchi tunaelekea pabaya kila MTU Amalia...ada...kodi....mahitaji muhimu..sekta ya habari na mawasiliano imedhoofika baada ya kuingiliwa na kudhibituwa na wanasiasa..biashara haziendi....pesa hakuna...mzunguko Wa pesa ....umedorora.....huwa nafikiria sijui itakuaje?nimesikia Jana kua hats IPP media hawajalipwa karibu miezi mitatu..yaani kiujumla kampuni IPO taaban,Sahara media hiyo ndio wengi tuliokua tunajua mgogoro wao ndio maana ile channel ten na radio times zikanunuliwa na ccm maana ilishindwa jiendesha
 
Yani utoe elfu moja yako ununue gazeti badala ya kununua maandazi kumi watoto wanywe chai? Magazeti huwa tunasoma tu vichwa vya habari. Habari kamili zinapatikana mtandaoni...
Teknolojia imeua ajira nyingi sana hapa Duniani...
 
Kiukwel hali ya biashara kwa sasa n mbaya kampun nying znapunguza wafanyakaz n juz tu gazet pendwa la mwananchi limepunguza wafanyakaz kuna haja kuwe na mjadala wa kitaifa juu ya muelekeo wa uchumi s ajabu pia watu wakabeza hili wakakwambia nyie n miongoni mwa wapiga dili wa awamu iliyopita kwamba mlinufaika na mfumo uliopita japo mm napinga sana hili MAONI YANGU 2020 ipo jirani tusikwepeshe tuwamalize hawa watatuua tukiwapa miaka 5 mingne huyo ROSTAM AZIZ mwenyewe kanyosha mikono juu kama mateka kurudi kwa JIWE hali n tete hasa MEDIA INDUSTRY kama magazeti bora kidogo radio na TV
Wazo lako ni zuri sana ila ni Media ipi itakayokuwa tayari kuuandaa huo mjadala,haiogopi kufungiwa ?
 
Back
Top Bottom