Mpatanishi
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,811
- 623
- Thread starter
-
- #61
Ha ha haaaa una akili sana!!!!!
Mkuu OLESAIDIMU huu msimamo hadi kwa HR nilishamueleza, mwezi may mwaka jana walikosea nika miss salary. nilichofanya ni kuwaandikia barua kuwa sitofika kazin kwa mwezi mmoja kutokana na kukosa mshahara tena kwa uzembe wao.
wakajua natania, ilipofika wiki hawanioni wakanipigia niende shule nikopeshwe hela na akaunti ya shule.
Nikaenda nikalipwa ndio nikaendelea kufanya kazi.
Leo sijaenda nipo kwenye mishe zangu, salio kama litasoma leo basi kesho panapo majaliwa nitakuwepo kazini ila kwa leo HAPANA.
Ha ha haaaaaaa Mpatanishi unajua ndio maana hayati JK aliona hili! !!!
Alijua watu wakiwa na vipato nje ya mishahara huwa hawatingishiki, ukishika mboga ye anamwaga ugali ugali nusu kabisa anasubiri umwage mboga naye amalizie nusu iliyobaki!!!!!
Sio jambo zuri ila sasa watu wafanyaje???!!!
Mtu kajikopa wese mwezi mzima halafu holaaa!!!
Wala vumbi mnatia huruma!
Bora kuliko kuendesha gari la taka lililojaa viporo na pampas zenye kimba za watoto wa kizungu
Haaah haah mkuu mwaka jana walijaribu kunitisha eti watapeleka jina langu ngazi za juu wataniwajibisha.
Nikawajibu waanze kujiwajibisha wao kwanza kwa kushindwa kuhakikisha ninapata mshahara wangu,haki yangu wakati wao ndio kazi yao na wanalipwa mshahara na marupurupu kwa kazi hiyo.
Katika hali isiyoeleweka mpaka sasa mishahara haijatoka. hususani kwa kada ya ualimu kwa manispaa zote tatu hapa Dar Es Salaam na kwa hili nadhani hata mikoani hali ni hii hii.
Hii serikali mbona haieleweki iweje mishahara isitoke na hakuna maelezo yoyote, wahusika wapo kimya.
Katika hali isiyoeleweka mpaka sasa mishahara haijatoka. hususani kwa kada ya ualimu kwa manispaa zote tatu hapa Dar Es Salaam na kwa hili nadhani hata mikoani hali ni hii hii.
Hii serikali mbona haieleweki iweje mishahara isitoke na hakuna maelezo yoyote, wahusika wapo kimya.
Ulinawa mikono? Au unakula na kinyesi cha vibibi?Nimemaliza na mtonyo wangu nshakabidhiwa na sasa hivi niko hapa nakula ribeye steak, caviar, na mvinyo ya Pinot Grigio. Hakuna cha kusubiri sirikali wala hazina.
Una jingine?
Ulinawa mikono? Au unakula na kinyesi cha vibibi?
Wizara ya Elimu Walio kwa Katibu Mkuu(Vyuo vya Ualimu na Shule za Mazoezi) Pia bado. Hawa watu wanaleta utani na maisha ya watu!!!