Mishahara, marupurupu ya viongozi na kupambana na umaskini Tanzania!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara, marupurupu ya viongozi na kupambana na umaskini Tanzania!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mshiiri, Jul 25, 2009.

 1. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Wakuu heshima sana na huu mjadala ni very educative, kuna mengi sana hapa yamesemwa ambayo ni valid na hayakwepeki, ni muhimu sana hii debate ikapanuliwa katika sekta nyingi za serikali yetu ukianzia na ofisi ya rais hadi chini,

  - Pamoja na kwamba Spika indiviually hana makosa kisheria kwa kuishi kwenye hii nyumba, ni kweli he is obligated kuangalia matumizi ya ofisi yake, kwa sababu hata Obama alipoingia amebadili mengi sana ya matumizi ya ofisi yake ili kupunguza matumizi ambayo yako okayed na sheria.

  - Bunge letu lianze kujiangalia upya, kama kweli linaishi within our national financial means maana reading between the lines hii thread inaonekana kuna some financial abuse huko kwa visingizio vya sheria na hili ni kwa wabunge wote kuanzia CCM na hata Upinzani,

  - Kamati ya bunge ya mahesabu ianzishe utaratibu wa kuweka wazi matumizi ya ofisi mbali mbali za serikali na hasa mishahara ya maofisa wa serikali, I mean mimi sikujua kwamba tuna wananchi wanaolipwa mpaka Shillingi Millioni 18, garademiti that is 18,000 USD are you kidding me or what hivi unajua what it takes kwa US government kukulipa hela kama hizo tena monthly?

  I mean nilitaka kuu'dissmis huu mjadala, kwa sababu ya kukosekana kwa facts, lakini damn this is a valid national debate Tanzania tunakuwaje na maofisa wa serikali wanaoweza kulipwa US Dollars 18,000 kwa mwezi hela za kodi za wananchi? That is insane, sasa hawa wabunge wanafanya nini huko bungeni zaidi ya kwenda kukusanya pay day tu, yes hili la nyumba ya Spika ingawa halina anything to do na yeye binafsi as a leader kisheria, lakini ni justified tena 100% kulijadili as a starting point against matumizi mbaya ya hela za kodi za wananchi.

  Respect.

  Kamanda FMEs! + Mshiiri
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Zitto [​IMG]
  Zitto has no status.
  JF Senior Expert Member

  [​IMG] Re: Spika anaishi nyumba ya milioni 10 kwa mwezi!
  Mijadala yetu watanzania wakati mwingine huwa ninapata nayo shida sana. Mara kwa mara tunaangalia mtu na kuachana na hoja kabisa. Hebu nije kwenu kwa kuangalia mtu. Lengo ni kupanua tu mjadala ili mjaribu kuona kuwa suala la malipo au stahili za dhamana ya kikatiba ni suala la kuliangalia kwa mapana yake.

  Agalia mifano ifuatayo.

  1. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania mshahara wake ni 16,000,000 kwa mwezi
  2. Kamishna Mkuu wa TRA analipwa sh 18,000,000 kwa mwezi
  3. Mkurugenzi Mkuu wa TBC analipwa sawa na Gavana wa Benki Kuu.
  4. Orodha ni ndefu na hao wote mshahara wao (mshahara tu bila marupurupu mengine) ni zaidi ya ule anaopata Rais wa Nchi (Rais analipwa 5.4m kwa mwezi).

  Turudi kwenye hoja, malipo ya nyumba ile yanaendana na soko? Taratibu zilifuatwa? Lakini kama lengo lenu ni kumsulubu Sitta, mnaweza kuendelea na wala hamtapata suluhisho maana kesho akiwa Spika Slaa au Hamad Rashid au Marmo nk, atalipiwa nyumba hivyo hivyo kama hatutamaliza tatizo la Nyumba kwa viongozi wa Kikatiba.

  Fenicha za 200m zilizonunuliwa kwa ajili ya nyumba ya Spika, ndizo hizo hizo na thamani hiyo hiyo ambayo amenunuliwa Jaji Mkuu na ni zaidi ya hapo alizonunuliwa Waziri Mkuu amara alipoteuliwa maana PM anaetoka hutoka na kila kitu alichokuwa anatumia (wanasema ndio commonwealth tradition)
  __________________
  "To see my country Tanzania becoming a strong Democracy and completely ending Single-Party Dominance."
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Hivi rais analipwa hata hizo Sillingi Millioni 4 for what? Si analipiwa kila kitu mpaka kufa kwake, sasa haya malipo ni ya nini hasa?

  - Hivi kweli akiwa a sitting rais kuna mtoto au ndugu yake wa karibu anayehitaji kumilipia elimu?

  FMEs!
   
 4. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  It is insanity. Ndo maana maprofessor hawaishi kukimbilia siasa kwani wenye vyeo vya kisiasa wanajipangia mishahara. Sijui 18m kwa mwezi ni scale gani ya mshahara au ni KANDAMIZA MWANAWANE SCALE???? Tanzania balaa eehe!!!


  Mi nafikiri ni zaidi ya hata ya insanity it is an insult as well na tunahitaji watanzania sasa kuchoka na kusema YES WE CAN! Kama amani ikiwa ni kufanyiana hivi kumbe ni amani imla. We should have been in a battle, BUT we are being sirened happiness na hivyo tunakuwa patient. Sijui ni hali gani itakayotuamsha Watanzania kama si hii.

  Katiba inafuatwa kweli, mbona naona hata ile ya binadamu wote ni sawa ambayo ni preamble tu imefanywa mbaya? Kimsingi katiba ndio msahafu au biblia ya nchi na kama hata kipengele kimoja kinavunjwa na kundi la watu au mtu vita ni halali kabisa.

  Scale ya chini ya mshahara kwa sasa ni take home kama 80k ambayo ni matusi matupu yet hawa jamaa wanaishi kwa kodi za hawa take home 80k na kula poda na kuku kwa mrija. Hivi tutasubirinini mpaka lini??? Nafikiri we need to wake up and react. Viongozi tumewachagua sisi, au tumewasomesha sisi, na kamwe sisi ndio msingi wa uwepo wao na katu haimaanishi wanatutawala kama wakoloni ambao waliitumia hii nchi kuvuna rasilimali. Hamna haja basi ya uwepo wao ikiwa wanakuwa sawasawa na wakoloni. Namna hii hamna mantiki ya kuwafukuza wakoloni, ni bora wangebakia au wakarudi tukajua moja.

  Ndo maana utaona vyeo hivi vikubwa vikubwa vinapatikana kimchongo huwezi ona ikiwa wazi na fanya tafiti utagundua nchi hii sasa hivi inaongozwa kifamilia which is not different from uchifu, umangi, usultani nk. Better then we revert to our communal/ancestral leadership ambayo tutai-modernise.

  At least this is my anger and rage against those that do not practice what they preach by heart!!!
   
 5. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Changieni mawazo basi au tubadili mwelekeo na kujadili aina za mapishi humu?
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  1. Ndo maana Wabunge wanadai zaidi..yaani mishahara na maslahi ya 7m kwa mwezi ni kidogo..ukilinganisha na na say Katibu Mkuu wa Wizara anayepata 14m kwa mwezi!

  2. Hoja hapa: kama cake ni kidogo: ni kwa nini wachache wachukue kiasi kikubwa hivyo bila hata iabu??? Je huu ni Uungwana??

  Fikiria Mwalimu ya Primary ambaye naye kama Mtanzania anayehitaji kula, kuvaa, kusomesha watoto n.k analipwa 150,000.
   
 7. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Nafikiri tukatae kulipa kodi tuone watatoa wapi hiyo mishahara. Tunaamka asubuhi moja tunatangaza mgomo wa miaka kumi bila kulipa kodi then tuone hizo milioni watalipana na mavi ya mama zao!
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Jamani wizi unaanzia kwa wabunge tuliowachagua wenyewe kwenda kutupigania.
  Ole wako ukisema "Jamani wabunge mishahara yenu ni mikubwa mno kuliko yetu waliowapeleka huko"
  Ngoja jibu tena utakalopata toka pande zote mbili yaani chama tawala na wapinzani!
  Si tuna ushahidi? Mimi niliona live TBC wakimshambulia Dr Slaa kuwa anajitafutia umaarufu! Wao kutuibia sawa kupinga wizi ni kujitafutia umaarufu.
  Hizo ndizo sera za wakina Marmo! mbunge ambaye watu wa kabila lake ukiwaona wanavyoishi kimaskini utashangaa ni jinsi gani wanamrudisha bungeni kila siku.
  Nafikiri tuwaombee wote hawa wafe. Maana hata hawana faida. Na kama wanautajiri wamejilimbikizia nao ufe.
   
 9. M

  MathewMssw Member

  #9
  Jul 27, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu wa mbinguni waangamize mafisadi wote hawa! yaani wanamnyonya mnyonge nakujilimbikizia. Hawa wanapaswa kulaaniwa kabisa! Hawana hata haya! Ninawalaani kwa ufisadi huo
   
 10. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Wabarikiwe na waishi miaka 900 kama kina nabii Musa
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu usikate tamaa. Binafsi niko tayari kuchangia tena sana tu. Sasa tunachohitaji ni data ili tuweze kuongelea mambo (issues) badala ya watu. Zitto katupatia mfano. Tunaomba walio na taarifa watuwekee.
  1. Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Naibu mawaziri na makatibu wakuu (na manaibu wao) wanapata mishahara kiasi gani na marupurupu yapi ili tusonge mbele. Zamani kulikuwa na tetesi kuwa Waziri anakuwa na gari 3, moja lake, moja la mama na jingine la watoto. Je, hali ikoje sasa?
  2. Wakuu wa mihimili mingine ya dola na wasaidizi wao wanalipwa kiasi gani?
  3. Wakuu wa taasisi za umma nao wanapata nini?
  4. Ikibidi tunaweza kulinganisha na wafanyakazi wengine ambao data zao ni rahisi kuzipata kwani scale zao zinapatikana kirahisi.

  Tukiweza kupata hizo taarifa basi tutaweza kujiridhisha kwa nini sehemu kubwa ya bajeti yetu inaishia kwenye mishahara na marupurupu ya viongozi na wafanyakazi badala ya kujielekeza kwenye shughuli za maendeleo.
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,885
  Trophy Points: 280
  Zamani nilikuwa naona matumizi ya Jeshi kuondoa utawala wa kiraia ni uonevu mkubwa. Ila sasa naanza kufikiri tofauti.
   
 13. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hapo umegusaa..

  wabunge wetu sio wawakilishi halali wa masilahi ya wananchi bali nafsi zao tuu.

  wabunge wana ,mamlaka ya kuisimamia serikali mojawapo ikiwa kupinga matumizi mabovuu ya rasilimali za umma kama masurufuu yasiyokuwa na uhalisia na utendaji.

  Dr slaa alikuwa sahihi sana ila kwa kuwa jamii sehemu kubwa (vyombo vya habari, taasisi za kiraia, taasisi za dini na vyama vya siasa) haijatambua jinsi ya kukabiliana na mapungufu ya utawala kwa mustakabali wa taifa na kuweka mbele siasa za ubinafsi(kujadili watu) haikupewa kipaumbelee..

  hatuwezi kuendelea/kusonga mbele kwa kujadili mtu au watu bila kulazimishia kubadili mfumo wa kiutawala unaolinda mapungufuu yotee haya kwa asilimia zaidi ya 100.
   
 14. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #14
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Mchukia Fisadi,
  Nilipoanzisha mjadala wa hoja ya mishahara na marupurupu makubwa ya Wabunge, nilikuwa nikilenga hoja ya kuwa kunajengeka Gap kubwa sana kati ya watu mbalimbali katika Taifa letu. Kwa bahati mbaya wengi hawakuelewa hoja yangu wakati ule. Kimsingi hoja ile ililenga kuwa na mjadala wa kitaifa, na kufikia mahali tufunge hii gap kwa namna ambayo tutakubaliana, keki ndogo ya Taifa igawanywe kwa uwiano wenye mantiki, lakini pia wale wa chini waweze kunyanyuliwa ili nao waweze kuishi maisha yenye hadhi ya ki-utu na kibinadamu. Huu ndio mjadala unaotakiwa kuendelea. Nimetamka hadharani, hakuna soko la Wabunge au viongozi wa juu wa Serikali. Wote tunapata mahitaji yetu muhimu ya kibinadamu kwenye soko hilo hilo. Hivyo hakuna justification ya kundi fulani kuwa na mshahara au marupurupu makubwa ya kupindukia.Tunaachiana kwa majukumu kweli, lakini sote tunahitajiana. Tunaishi katika mfumo wa "chain". Pingili mmoja likidondoka, hakuna chain. Hivyo hata mhudumu mwenye jukumu la kufagia ofisini ni muhimu, akikosekana si Gavana, wala Kamishna Mkuu wa TRA au Spika anayeweza kufanya kazi kwa ufanisi. Kama tunahitajiana, ni lazima kuwe na uwiano fulani, unaojali nafasi, hadhi, lakini pia unajali ubinadamu wa wale wa chini sana. Vipi tutapata uwiano huu, ndio msingi wa mjadala wa kitaifa!
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,639
  Likes Received: 82,248
  Trophy Points: 280

  Dr Slaa, juhudi zako za kutetea maslahi mbali mbali ya watanzania katika Bunge wengi tunazifuatilia kwa karibu sana na pia tunazithamini sana. Wengi tulishangazwa pale ambapo Wabunge wa CCM walipoamua kukuzomea ndani ya Bnge ulipoanzisha mjadala huu.

  Ni ukweli usiofichika kwamba sasa hivi kuna gap kubwa sana kati ya mishahara ya Rais, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wabunge ukilinganisha na mishahara ya Watanzania walio wengi wakiwamo pia Walimu, Polisi, Madaktari na manesi watu ambao wana umuhimu mkubwa katika nchi yetu.

  Halafu inashangaza kuona Wabunge wa CCM walipinga sana juhudi zako za kuweka wazi ukubwa wa mishahara hiyo na marupurupu wanayoyapata kila mwezi. Pamoja na kuwa mishahara hiyo inalipwa na walipa kodi wa Tanzania lakini Wabunge wa CCM wangependelea kuona kwamba walipaji wa mishahara hiyo ambao ni walipa kodi wa Tanzania wanaendelea kutofahamu viwango vya mishahara hiyo na marupurupu wanayoyapata. Leo hii tunajua mshahara wa Rais wa Marekani, Masenata na wawakilishi wengine lakini mshahara wa Rais wetu, Mawaziri na Wabunge ni siri kubwa sana, sijui hili linasababishwa na nini hasa.

  Miaka ya nyuma gap kati ya mshahara Viongozi wa juu wa Serikali na Wabunge haikuwa kubwa sana ukilinganisha na mishahara ya Watanzania wengi. Miaka ya karibuni tumeona viongozi hao wakijiongezea viwango vikubwa sana vya mishahara na marupurupu wakati huo huo ongezeko la Wafanyakazi wengine lilikuwa ni dogo sana ama kutokuwepo kabisa.

  Hali hii inaweza kuleta hatari ndani ya nchi pale ambapo wananchi wataona hawapigi hatua zozote za kimaendeleo miaka nenda miaka rudi kutokana na viwango vidogo vya mishahara ambavyo hata havikidhi gharama zao za maisha ya kila siku wachilia mbali kufanya mambo ya maendeleo katika maisha yao kama vile kusomesha watoto wao kujijengea nyumba zao badala ya kuendelea kupanga miaka nenda miaka rudi.

  Kwa kumalizia nakuomba usichoke na juhudi zako ambazo wengi tunazithamini sana za kuhakikisha gap iliyokuwepo kati ya mishahara na marupurupu ya viongozi mbali mbali wakiwemo Wabunge inapunguzwa sana ili kuhakikisha Watanzania walio wengi nao wanafaidi utajiri tuliojaliwa na Mwenyezi Mungu.
   
 16. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Huu mjadala unatukumbusha kitu kimoja kuwa jamii yetu imejaa watu wengi ambao ni walafi, na wachoyo (greedy). Haishangazi kuwa wale ambao tulidhani wangefanya kazi ya kutetea maslahi yetu katika bunge ndio wanafanya kazi ya kutukandamiza. Wabunge wanapokuwa tayari kutetea maslahi ya kikundi cha utawala au chama kuliko haki ya mtanzania kuishi kama binadamu inatia mashaka ubinadamu uliopo ndani yao.
  Katika nchi hii kuna watu wanajiona ni binadamu kuliko wenzao. Wanasahau kuwa ni kodi za watu masikini ndio zinazowafanya wao wastawi.
  Kosa kubwa la kijamii lililotokea nchi hii linazidi kutumaliza kiasi kwamba kilio cha watu wa chini kudai walau stahili za msingi za maisha zinaonekana kama kelele za chura ambazo hazimzuii tembo kunywa maji.
  Mtu anayesimama kuueleza ukweli wa ulafi uliopo anaonekana kama anajitafutia umaarufu wa kisiasa, na bahati mbaya propaganda kubwa zinatumiwa kumnyamazisha.
  Kazi ya wabunge wetu bungeni ni nini? kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja tu?
  Ninaamini tunaweza kuanza upya tukitaka, serikali inaweza kufanya kazi kwa matakwa ya wananchi.
  ....hata hivyo wote tutakufa mwisho wa siku.....
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu kitu kinachofichwa ujue kina tatizo. Hicho si halali. Hata kama kina uhalali wa kisheria basi kinaweza kuwa kinakosa uhalali wa kimaadili na kijamii. Ndivyo ninavyoliona tatizo la wakubwa kuficha mishahara yao wakati wanakodolea macho TV kuangalia habari za Obama akitangaza mapato yake ya mwaka na kodi alizolipa (annual tax returns). Ndiyo maana ukifuatilia kila kitu hapa Bongo utashangaa jinsi watu watakavyolia. Hata hao wanaokodisha nyumba kwa $8000 si ajabu kukuta hawalipi kodi. Kila kitu ni usanii mtupu.
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana nawe kuwa lengo ni thamani na uwezo wa taifa juu ya Huduma na sio kumlenga mtu. Lakini cha kujiuliza hizo STAHILI zinapangwa na nani? Iwapo mtu kama Sitta bila ya kujali wadhifa wake anakuwa mstarui wa mbele kutetea matumizi yaliyo mzigo kwa Taifa tutaacha wapi kumonyesha kidole kwa kupandisha hadhi huduma fulani ambayo ikitolewa kwa kiongozi aliepita.
  Na hili la HADHI kwa viongozi tu linatoka wapi kwani Watanzania wote wanahitaji HADHI yao ipande. Kama walikuwa wakipata mlo mmoja kwa siku basi wapate miwili kwa kuanzia lakini hili halifikiriwi na badala yake kila kukicha wenye STAHIKI YA HADHI ni viongozi tu.
  Mtu wa kawaida hawezi kufahamu ukimwambia kuwa mtu analipiwa Mill. 10 kwa mwezi kwa nyumba huku aliyelipuliwa nyumba yake kwa mabomu anaishi kwenye hema akisubiri "wakubwa" waamuwe kumpa Millioni 5.
  Jambo jengine ni kuwa hizi STAHIKI ZA HADHI mbona ni stahiki ya wachache tu? Hivyo mtu wa kawaida haitaji makazi, mbona halipiwi? haitaji kulipa bili ya simu, haitaji maji na vyenginevyo vyengine?
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Maneno mazito sana mkuu, ubarikiwe.

  Respect.

  FMEs!
   
 20. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Nakupongeza sana kwa juhudi zako za kupambana na ufisadi uliokubuhu katika jamii yetu.


  Tatizo langu katika hoja yako hii ni jinsi gani unaweza kuniridhisha kwamba unachokisema ni kweli kinatoka moyoni, kwa dhati, ama ni mwendelezo ule ule wa siasa zisizokuwa na faida kwa jamii yetu. Kwa maana ya kwamba mnaongea tu ili kuwahadaa wananchi kwamba mnawatetea, na mkishamaliza mnaendeleze ufisadi ule ule.

  (a) 1995-2000 ukaweka kibindoni kiinua mgongo (kimyaaaa)

  (b) 2000-2005 ukaweka kibindoni kiinua mgongo (kimyaaaa)

  (c) 2008, Miaka 13 baadae (tangu 1995) ndiyo unagundua ufisadi wabunge mnaolifanyia Taifa hili? MLAANIWE kwa unafiki huu.. Leo hii keki imekuwa ndogo tena?

  Ni hivi: Kuna wabunge ambao wameingia kwa mara ya kwanza 2005 nao wanahitaji kunufaika kama wewe ulivyonufaika huko nyuma kwa kutunyonya sisi wananchi. Kwa hiyo usitegemee kwamba watakuunga mkono hata kidogo.

  Sasa kwa mahesabu hayo hapo juu, mimi kama mwananchi wa kawaida nashindwa kukuelewa hadi hapo utakaponieleza jinsi ya kuzirudisha hizo mlizotuibia tangu mmeingia bungeni. Vinginevyo hizi ni siasa tu za nitoke vipi!
   
Loading...