Mishahara hewa, ilikuwa ikiliwa na nani?

TANZANNIA

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,047
385
Naomba mnisaidie kidogo,

Ni nani hasa aliyekuwa anakula hii mishahara hewa, ni wafanyakazi waliofukuzwa /kuachishwa kazi/kufariki nk na fedha kuendelea kuingia kwenye akaunti zao au viongozi ambao walikuwa wanajua fulani amefariki /amestaafu n.k na kujipakulia hiyo mishahara?

Je,mbinu gani ilikuwa inatumika?
 
Mnyororo wa kuliwa hizo hela ni mrefu sana, ukifuatilia mwanzo mpaka mwisho unaweza kupata ugonjwa bure maana wamo ambao hutaamini macho na masikio yako.
 
Mimi binafsi hilo swali nimekuwa nikijiuliza sn na kwa nini Magu asiwatumbuwe nao?
 
Naomba mnisaidie kidogo,

Ni nani hasa aliyekuwa anakula hii mishahara hewa, ni wafanyakazi waliofukuzwa /kuachishwa kazi/kufariki nk na fedha kuendelea kuingia kwenye akaunti zao au viongozi ambao walikuwa wanajua fulani amefariki /amestaafu n.k na kujipakulia hiyo mishahara?

Je,mbinu gani ilikuwa inatumika?

Mkuu, mtu mmoja kula hizo pesa si rahisi. Ndiyo maana wahusika wanakuwa na vigugumizi kutoa majina ya wafanyakazi hewa. Iweje marehemu aendelee kuchukua mshahara wakati viongozi wake wailyani wanajua alishafariki na si ajabu walishiriki maziko yake.

Hapo lazima kuna magenge ya maafisa utumishi (hatoi taarifa ya kuondoa jina la marehemu). Wahasibu (wanaandaa malipo ya marehemu). Wakurugenzi (wanapitisha malipo ya marehemu).

Lakini kubwa kuliko yote, wana watu wanaoshirikiana nao Hazina kwenyewe.

Hata kama wameficha majina kwenye orodha zao, sasa watuambie nani alikuwa analipwa fedha hizo. Je ndugu wa marehemu wanahusika? ATM zote zina camera kuona nani alikuwa anachukua. Bank zina taarifa za mwenye account. Hizi ni kazi za siku mbili tatu nkuwajua wahusika wote.
 
Wahusika wakuu ni watatu tu! Mkurugenzi, afisa utumishi na Wahasibu

Watumishi hewa wengine ni marehemu, wengine wamehamishwa kutoka halmashauri moja hadi nyingine, wengine wamefukuzwa kazi na wengine wamestaafu
 
Upo sahihi Mkuu, ingawa na mtumishi hewa mwenyewe ni mhusika mamba 4.
Rafiki yangu Fulani aliacha kazi halmashauri x tangu 2012 kumfuata mumewe Songea Manispaa, kwakuwa uhamisho wa halali ulibuma, tangu 2012 hadi miezi ya karibuni alikuwa anakula salary kwa makubaliano na afsa utumishi alikoacha kazi, mwezi mmoja mshahara unaingia kwenye akaunti yake na mwezi unaofuata akaunti ya Afsa.
 
Mkuu, mtu mmoja kula hizo pesa si rahisi. Ndiyo maana wahusika wanakuwa na vigugumizi kutoa majina ya wafanyakazi hewa. Iweje marehemu aendelee kuchukua mshahara wakati viongozi wake wailyani wanajua alishafariki na si ajabu walishiriki maziko yake.

Hapo lazima kuna magenge ya maafisa utumishi (hatoi taarifa ya kuondoa jina la marehemu). Wahasibu (wanaandaa malipo ya marehemu). Wakurugenzi (wanapitisha malipo ya marehemu).

Lakini kubwa kuliko yote, wana watu wanaoshirikiana nao Hazina kwenyewe.

Hata kama wameficha majina kwenye orodha zao, sasa watuambie nani alikuwa analipwa fedha hizo. Je ndugu wa marehemu wanahusika? ATM zote zina camera kuona nani alikuwa anachukua. Bank zina taarifa za mwenye account. Hizi ni kazi za siku mbili tatu nkuwajua wahusika wote.
Naomba mnisaidie kidogo,

Ni nani hasa aliyekuwa anakula hii mishahara hewa, ni wafanyakazi waliofukuzwa /kuachishwa kazi/kufariki nk na fedha kuendelea kuingia kwenye akaunti zao au viongozi ambao walikuwa wanajua fulani amefariki /amestaafu n.k na kujipakulia hiyo mishahara?

Je,mbinu gani ilikuwa inatumika?
hata kama ni chai kubwa hao watu wafuatiliwe then wakibainika wafilisiwe mali zao walizopata kutokana na hzo pesa za watumishi hewa
 
Watu wanaanda majina ya wafanyakazi feki tena ambao hata hawajawahi kuajiriwa.Mfano huyo wa TRA alikuwa anachukua mishahara ya watu 17 yeye peke yake inakuaje hapo.
 
Nadhani hatua inayofuata ni kuwatambua wahusika wa mchezo huu mchafu.Kwa sababu hawa watu hewa walipangiwa bajeti ,ikapitisha na bunge au taasis na hatimaye kwenda kwa mifuko ya watu.Asifukuzwe mkuu wa mkoa tu wengine wafuate
 
Upo sahihi Mkuu, ingawa na mtumishi hewa mwenyewe ni mhusika mamba 4.
Rafiki yangu Fulani aliacha kazi halmashauri x tangu 2012 kumfuata mumewe Songea Manispaa, kwakuwa uhamisho wa halali ulibuma, tangu 2012 hadi miezi ya karibuni alikuwa anakula salary kwa makubaliano na afsa utumishi alikoacha kazi, mwezi mmoja mshahara unaingia kwenye akaunti yake na mwezi unaofuata akaunti ya Afsa.
Pia jumlisha internal auditors na CAG.
Kaka kua mzalendo kwa kuisaidia takukuru
 
Mnyororo wa kuliwa hizo hela ni mrefu sana, ukifuatilia mwanzo mpaka mwisho unaweza kupata ugonjwa bure maana wamo ambao hutaamini macho na masikio yako.

Mkuu sema tuu hujui pia lakini hii ya kutuaminisha kwamba kufuatilia unaweza pata ugonjwa si kweli, mbona juzi tumeelezwa yule aliyekuwa anapokea mishahara 17 kuna hata aliyemeza panadol??
 
Back
Top Bottom