Mishahara hakuna mpaka leo 31, manisaa ilala

Mpatanishi

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,810
623
Wakuu.
Mm ni mtumishi wa umma idara ya elimu. Mpaka leo tar 31 mishahara haijaingia bank.

Inasemekana hela za mishahara wamelipwa watu wa Sensa mana waligoma na serikali haikua na hela.

Hivi hii haki kweli? Kwa nini serikali imeshindwa kulipa mishahara wakati muafaka? iweje mishahara ya watu ifanywe posho za sensa?
Ikumbukwe wilaya ya Kinondoni wamelipwa mishahara tangu tar 24 tena kwa mafungu, temeke wamelipwa jana. Ilala naona wahusika wamekausha tu ila wajue kabisa wasipotoa leo jioni basi jumatatu patachimbika tumechoka na Upuuzi wao.

Kwa kweli navumilia kuwa mtanzania..
 
Vumilia mkuu, enzi zetu za ustaadhi rukhusa Mwinyi tulisubiri mshahara mpaka tarehe 47, na wengi wa enzi hizo tuliishia kuoa mama ntilie waliotufaa wakati wa shida
 

Kama kuna halimashauri ambazo zimwshalipa wafanyakazi mishahara yao basi hilo ni tatizo la halimashauri yako. Mishahara ikitoka inatoka kwa wafanyakazi wote.
 
Utalipwa kesho kaka si unaona mwezi haujaisha?

kaka mwez ndio unaisha huu. Kama vp tuuze mali za ofisi tuweze kujikimu, waache upuuz hawa kamashahara kenyewe kaduchu je wanategemea salary ya july mpaka leo itakuwepo?
 
mkiambiwa habari za mabadiko mnsema ccm imewalea,na wakati mwingine mnanunuliwa kwa pesa ya siku moja,hangaikeni.
 
Vumilia mkuu, enzi zetu za ustaadhi rukhusa Mwinyi tulisubiri mshahara mpaka tarehe 47, na wengi wa enzi hizo tuliishia kuoa mama ntilie waliotufaa wakati wa shida

haaah haaah nimecheka sana mkuu japo nina hasira
 
kaka mwez ndio unaisha huu. Kama vp tuuze mali tuweze kujikimu waache upuuz hawa kamashahara kenyewe kaduchu je wanategemea salary ya july mpaka leo itakuwepo?

Sema kale ka EID kalikuja vibaya mi mwenyewe niko vibaya. Tupeane pole tu
 
mkiambiwa habari za mabadiko mnsema ccm imewalea,na wakati mwingine mnanunuliwa kwa pesa ya siku moja,hangaikeni.

sisi wa dot com ndio tunaendesha m4c madarasani mamajack usijali kura zitakazoiondoa ccm madarakani nyingi zitakua za wanafunzi na watumishi wa umma.
Mark my words.
 
Sasa bora nyie wa serikalini.Sie wa sekta binafsi za magumashi mshahara kutoka tar 55 kila mwezi ni kitu cha kawaida kabsa!
 
dah pole kaka ila nyie si mnachukua nusu japo tar 15 then tar 30 mnamalizia

Kakudanganya nani?Hizo policy zipo lakn Wagumu haoo ka nini sjui,mpaka upate the whole process is as tedious as applying for a Us viza from Iran!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…