Misamaha ya kodi Bakwata na Taasisi nyingine

Mara nyingi kazi zinazofanywa na taasis za Dini zina msaada mkubwa kwa serikal,

Huduma za elimu, matibabu, ajira ambazo kwa namna yake zinasaidia kutekeleza wajibu Wa serikali,

Sion msamaha wanaopatiwa kama unalingana na wanachofanya,wanafanya mazuri kupitiliza wanachosamehewa

Wasemehewe tu, maana wana wajibu sawa na msamaha huo, tuache wivu wa kitoto.
Huwa wanapewa ruzuku na inapobidi watalipwa mishahara watumishi wanaofanya kazi ktk taasisi za kidini!
Shida ni Hawa wanaosamehewa kodi, je misamaha ilitolewa kwa taasisi au ulotumika ujanja kupitisha magari ya watu!
Mfano ukiondoa bakwata taasisi nyingine yenye magari machache ni Roman Catholics ambao wao ndio wenye hizo taasisi nyingi kuliko dini zote kwa ujumla wake!
Kumbuka miongoni mwa magari ni pamoja na hammer au range za wahubiri kuna tija gani kila wiki usamehewe gari jipya? Faida kwa umma iko wapi?
Nadhani TRA waende kuchunguza taasisi zote, issue sio kulipa waliposamehewa Ila kujiridhisha kuwa hatukusamehe wafanyabiashara!
 
Ziangaliwe taasis zote iwapo pana usahihi wa matumizi ya misamaha hiyo
 
Mara nyingi kazi zinazofanywa na taasis za Dini zina msaada mkubwa kwa serikal,

Huduma za elimu, matibabu, ajira ambazo kwa namna yake zinasaidia kutekeleza wajibu Wa serikali,

Sion msamaha wanaopatiwa kama unalingana na wanachofanya,wanafanya mazuri kupitiliza wanachosamehewa

Wasemehewe tu, maana wana wajibu sawa na msamaha huo, tuache wivu wa kitoto.

kwani wanatoa bure? magari yote yatafutwe na yalipishwe kodi tangu yaingie nchin isipokuwa magar ya wagonjwa.

kuhusu utajiri, kati ya dini zetu, wapi kuna matajir?
 
mkuu mashirika ya dini yanafanya kazi nying za kuisaidia serikali hasa
elimu na afya
hospital kama
bugando
kcmc
tumaini
hydom
selian
etc zinatibu mamilioni ya watu bila kujali imani
vyuo au shule kama
marian
mau semimary
loyola
st agustine
tumaini
ruaha
bugando heath college
kcm etc
wanasoma maelfu ya watoto so si jambo jema kuwadai kodi vingnevyo serikali iendeshe shule zote na hospipali zote

wanasoma bure? tunatibiwa bure? kama huna ada, unaweza endelea na masomo?

vifutwe tu ila kwa mambo ya msingi tu. mbona Nassar alilazimika kulipa kodi ili alitoe bandarini gari la wagonjwa wa jimbo lake?
 
Tutoe michango yetu kwa busara na kuheshimiana. Huo ndo ustaraabu.

Kiislamu Kuhamisha Madhara Yaende Kwa Mwenzako Ni Kosa Kisheri, Wale Wote Wanaotaka TRA Ipite Kote Wajue Kwamba Bado Hakutafuta Ukweli Kama BAKWATA Wameenda Kinyume Na Taratibu Za Kodi. Hvyo BAKWATA Wajisafishe Ili Tuone Ukweli Na Si Kutafuta Huruma Ya Jamii/Waislamu Hii Si Haki.
 
Mi nadhani TRA wameanza na bakwata lakini watahoji kila taasisi!
Labda kwa kuwa bakwata ilikuwa na idadi ndogo ya magari kuhoji imekuwa nyepesi, wengine uchunguzi unaendelea wakiwa tayari wataombwa nao walete vielelezo!
Shida ya watanzania wengi hawajui wanamtumikia nani?
Wapo ambao Tanzania nafasi yake ni ya tatu baada ya dini na kabila, wengine ya NNE, baada ya kabila, dini na chama! Etc!
Hayo sio tatizo Ila linapokuja suala la kuwa Tanzania imedhulumiwa na dini, kabila au chama au mtu binafsi, tunaomba muipe haki yake jamhuri!
Mimi ni muislam na nimeipenda dini yangu na Tanzania ya pili lkn kama dini yangu Imeidhulumi Tanzania basi ijiandae kulipa, au kama wajanja wachache ndani ya taasisi wamefanya hivyo, wawajibisjwe na nchi, na taasisi!
Wale wakristo wakiwemo viongozi wa nchi, nao pia wajue haki ya Tanzania italindwa na dhamana ya vyeo vyao, wote tutoe ushirikiano kwa TRA

Haya Ndo Maneno Ya Muislamu Muungwana, Tuko Pamoja Ndugu Namwomba Allah Atukutanishe Ktk Haq
 
Kiislamu Kuhamisha Madhara Yaende Kwa Mwenzako Ni Kosa Kisheri, Wale Wote Wanaotaka TRA Ipite Kote Wajue Kwamba Bado Hakutafuta Ukweli Kama BAKWATA Wameenda Kinyume Na Taratibu Za Kodi. Hvyo BAKWATA Wajisafishe Ili Tuone Ukweli Na Si Kutafuta Huruma Ya Jamii/Waislamu Hii Si Haki.

Naona sasa mnataka kuubadilisha mjadala au mnakwenda nje ya maada ili kutekeleza agenda yenu.Nani aliyesema taasisi za kiislam zionewe huruma.Hakuankitu kama hicho kama wanatumia ujanja ujanja na kuitumilia bakwata kupitishia magari yao binafsi lazima wawajibishwe kwani hapo inakuwa kama umeidhukumu Tz. Lakini tukiangaloa magnitude ya problem ni kubwa mmo katika taasisi nyengine na kuna madudu kuliko hayo ya bakwata lakini kwa nini TRA imekaa kimywa na kuna malalamiko ya miaka mingi sana kwa taasisi hizo kwa viongozi wake kutumilia vibaya taasisi hizo kwa kujinufaisha wao binafsi na si kwa manufaa ya Tanzania kwa jumla.

Na kitu chengine wachangiaji wengine wame kipoint out inakuwaje taasisi inapokea misaada, kusamehewa kodi na hata serikali kulipa mishahara kwa wafanyakazi wao lakini gharama za matibabu ni sawa na taasisi nyengine ambazo hazipokei vitu hivyo na kama huna pesa once ukitaka huduma katika taasisi hizo basi utaisoma namba.... Huo kama si ujambazi ni kitu gani? imeshafika stage hii MOU iangaliwe upya je inamnufaisha mtanzania kama wanavyojidai
 
Huu ni mtazamo wangu binafsi, nadhani Serikali isifute hiyo misamaha a akodi, ILA, KAMA ITABAINIKA kua kuna taasisi inakwenda kinyume na masharti basi na ifuatiliwe bila kujali chochote na kama ikibainika kua ni kweli kuna MTU BINAFSI au KIKUNDI CHA WATU wanatumia mgongo wa hizi dini basi na ASHUGHULUKUWA bila huruma maana ni kinume cha sheria. OVER AND OUT,
 
Naona sasa mnataka kuubadilisha mjadala au mnakwenda nje ya maada ili kutekeleza agenda yenu.Nani aliyesema taasisi za kiislam zionewe huruma.Hakuankitu kama hicho kama wanatumia ujanja ujanja na kuitumilia bakwata kupitishia magari yao binafsi lazima wawajibishwe kwani hapo inakuwa kama umeidhukumu Tz. Lakini tukiangaloa magnitude ya problem ni kubwa mmo katika taasisi nyengine na kuna madudu kuliko hayo ya bakwata lakini kwa nini TRA imekaa kimywa na kuna malalamiko ya miaka mingi sana kwa taasisi hizo kwa viongozi wake kutumilia vibaya taasisi hizo kwa kujinufaisha wao binafsi na si kwa manufaa ya Tanzania kwa jumla.

Na kitu chengine wachangiaji wengine wame kipoint out inakuwaje taasisi inapokea misaada, kusamehewa kodi na hata serikali kulipa mishahara kwa wafanyakazi wao lakini gharama za matibabu ni sawa na taasisi nyengine ambazo hazipokei vitu hivyo na kama huna pesa once ukitaka huduma katika taasisi hizo basi utaisoma namba.... Huo kama si ujambazi ni kitu gani? imeshafika stage hii MOU iangaliwe upya je inamnufaisha mtanzania kama wanavyojidai
Kizibao hapa bakwata wameshutumiwa, huna nafasi ya kumshitaki mwenzako wakati kesi sasa ni ya kwetu! tumalize na hili la kwetu kwanza halafu tuende kudai haki ya jamhuri!
BAKWATA haipaswi kuwa sehemu ya madhalimu, kama taasisi yetu inafanya dhulma utashangaaje taasisi nyingine kufanya hivyo!
Labda ni kweli taasisi nyingine zinapendelewa nazo zinapaswa kuwajibika, ila hii yetu pia umefanya ufisadi, acha Mufti na TRA wawajibishe hawa wachache! Ndugu yangu unachotaka kufanya hapa ni kuingia mkenge sawa na ule wa sakata la ESCROW, ccm walidhani wanakilinda chama lakini kumbe walionufaika ni wachache sana, mwisho wa yote walipoteza heshima zao binafsi na zile za chama chao! Sisi katika hili naamini sio taasisi nzima inayohusika ni wajanja wachache wasiomuheshimu Mungu na wanaotaka kuipaka matope taasisi!
Hata wewe Bwana/Bi Kizibao ukiombwa uoneshe magari 5 tu ya BAKWATA najua fika hutoweza kulipata hata moja, basi hata kujua analitumia nani na kwa kazi ipi ya taasisi huwezi kuja na ushahidi huo!
Acha hawa wadaiwe, walipe na kisha tuiombe TRA kwa uwazi kabisa iendeshe zoezi kama hili katika Taasisi zingine!
Lakini hili la kwetu acha lishughulikiwe liishe!
Namuheshimu sana TEGETA KIBAONI kwa kuangalia mambo katika uhalisia wake, kuliko kujijenga mihengo isiyo na tija kwa taasisi yetu, dini yetu wala taifa letu!
Tusikubali kutumika kwa kunufaisha wachache na kuidhalilisha dini yetu!
 
Last edited by a moderator:

Kijana wacha unafiki huo..Nahisi wewe umekuwa kama watu wengine una mawazo mgando ya kufikiria ya kuwa nimeandika kuhusu bakwata nitakuwa ni muislam tu... Pengine naweza kuwa sina dini angalia post yangu ya juu hapo nimeandika nini

"Hakuankitu kama hicho kama wanatumia ujanja ujanja na kuitumilia bakwata kupitishia magari yao binafsi lazima wawajibishwe kwani hapo inakuwa kama umeidhukumu Tz"

Naona jazba imekupanda na ukafanya haraka ya kujibu bila ya kuangalia nimeandika nini na ukaamuwa kujifanya muislam ili maoni yako yaonekane yako sawa. kwa mawazo yako hapo ni sawa kama kuna paka kijijini anakula vifaranga kwani tu deal na huyu paka kwanza na tumuache chui aendelee kuna mbuzi na Ng'ombe wetu. Na kwa nini watu wanakuwa too defensive wanapoint out maozo katika taasisi hizi za dinina jinsi gani wanavyotumia religious indoctrination kuwadhulumu wananchi na nchi kwa jumla ili kujinufaisha wao na familia zao. Kama uwezo wako wa kufikiria ni mdogo na unahisi watu watu wanalishwa maneno na kutumiliwa basi hilo kwangu halipo.Na nina uhakika huyo afisa wa TRA atakapoamuwa kuzipelekea taasisi zilizobakia basi mtaanza kumpiga vita kupitia wafuasi, wenu na vyombo vyenu vya habari. Tanzania siyo mali ya taasisi au dini Fulani na Nasema tena serikali lazima iangalie hii so called MOU
 
Mustafa mkulo alipokua waziri Wa fedha awamu ya NNE alifanya utafiti na kubaini wizi mkubwa unaofanywa na taasisi za elimu kwa kukwepa kodi.

Alipendekeza misamaha ibaki kwenye speakers, vipaza sauti, nyama na tende tu. Wabunge hawakumuunga mkono ili kuwafurahisha viongozi Wa dini. Hatimaye JK akamuondoa
 
Kijana wacha unafiki huo..Nahisi wewe umekuwa kama watu wengine una mawazo mgando ya kufikiria ya kuwa nimeandika kuhusu bakwata nitakuwa ni muislam tu... Pengine naweza kuwa sina dini angalia post yangu ya juu hapo nimeandika nini

"Hakuankitu kama hicho kama wanatumia ujanja ujanja na kuitumilia bakwata kupitishia magari yao binafsi lazima wawajibishwe kwani hapo inakuwa kama umeidhukumu Tz"

Naona jazba imekupanda na ukafanya haraka ya kujibu bila ya kuangalia nimeandika nini na ukaamuwa kujifanya muislam ili maoni yako yaonekane yako sawa. kwa mawazo yako hapo ni sawa kama kuna paka kijijini anakula vifaranga kwani tu deal na huyu paka kwanza na tumuache chui aendelee kuna mbuzi na Ng'ombe wetu. Na kwa nini watu wanakuwa too defensive wanapoint out maozo katika taasisi hizi za dinina jinsi gani wanavyotumia religious indoctrination kuwadhulumu wananchi na nchi kwa jumla ili kujinufaisha wao na familia zao. Kama uwezo wako wa kufikiria ni mdogo na unahisi watu watu wanalishwa maneno na kutumiliwa basi hilo kwangu halipo.Na nina uhakika huyo afisa wa TRA atakapoamuwa kuzipelekea taasisi zilizobakia basi mtaanza kumpiga vita kupitia wafuasi, wenu na vyombo vyenu vya habari. Tanzania siyo mali ya taasisi au dini Fulani na Nasema tena serikali lazima iangalie hii so called MOU

Huna haja ya kunishutumu, bakwata wanachunguzwa na kama walikosea watawajibishwa, hilo sidhani kama lina mjadala hata Mufti analiunga mkono hilo Kizibao, hatuna haja ya kutoka povu ktk hili maana hata mamlaka za juu bakwata zinataka haki itendeke!
Kuhusu MoU hapa tunakwama sana waislam, taasisi huwa na MoU zaidi ya moja kwani kila ushirkiano au mipango ya pamoja huwa na makubaliano, ukishataja MoU basi lazima useme juu ya nini! kanisa katoliki linafanya kazi na serikali ktk maeneo mengi, mashule, hospitali, biashara, huduma nyingine za kiroho na kijamii kama taratibu za ndoa etc, sina hakika lakini vyote hivyo vitakuwa vimeanishwa ktk MoU, kama BAKWATA hatuna MoU na serikali maana yake taasisi yetu inaishi kwa huruma tu na sio mikataba. hilo sio jambo jema hata kidogo!
Kuhusu imani yangu nadhani sina haja ya kukuaminisha chochote, we amini unavyoamini!
 
Last edited by a moderator:
Hao wengine waliwahi kuombwa kutolea maelezo magari yao? Hamna chochote ni unafiki waache kuomba maelezo waliosamehewa magari 2000 na kitu watake maelezo kwa waliosamehewa magari 82!
sasa nafikiri unakubaliana na mimi kuwa kuna mambo hayajakaa sawa huko bakwata maana kuna viongozi wamesimamishwa
 
Huwezi linganisha udogo wa uhalifu dhidi ya uhalifu mkubwa, pengine walioingiza magari mengi wanayo na yanafanya kazi na yaliyoingizwa na bakwata ingawa machache lakini hayapo
 
Bila kulinganisha idadi ya magari kwa kisingizio cha dini ,je hayo magari 82 wanayo? Inawezekana bakwata hawana magari kwenye ofisi zao na wanaendesha mambo yao kwa magari ya kukodi na kwa ujumla serikali ina mkono mrefu
 
Ukweli ni kwamba huwezi kulinganisha makosa yako na ya wengine ,nakuna uwezekano bakwata waliingiza magari lakini maofisini kwao hakuna magari na kwa taasisi nyingi walioingiza utayakuta yapo. Hivyo bakwata ni makosa kufanya crime kwa kuingiza magari kibiashara au ya watu binafsi.
 
Kipindi cha nyuma Bakwata walifanya sana hivo,nakumbuka Bakwata kulikuwa na masheh wapigaji kama wakina chizenga na wengineo waliingiza sana magari na vitu vingine.
Bakwata pia walikuwa wana ratibu safari kwa vijana kwenda Iran na Pakistan watu kufanya yaooo.
so khsu issue ya kodi hilo limefanyika sana tu
 
Back
Top Bottom