Misamaha ya kodi Bakwata na Taasisi nyingine

Kizibao

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2010
Posts
1,299
Reaction score
751
Hivo Hatuna haja ya Kubisha na kusema kwamba Serikali ya CCM au Serikali ya Muungano Haina Dini.. Ushahidi Mdogo ambao ulikuwa Unajulikna kutokana na Unawiri wa Kundi la Dini Fulani na Unyonyaji au UDhoofishaji wa Kundi la Dini Nyengine ni Huu hapa.

Hapa tunaweza kuona Tofauti kubwa ya Misamaha ya Kodi ya Taifa Baina ya BAKWATA na MAKANISA. Na Hii nataka niwambie Wasomaji kwamba sio FITINA ya Kidini bali Tunataka Nchi Zetu Mbili Tuzipendazo yaani Tanganyika na Zanzibar na Serikali ya Muungano. Ziwe INVIGILANT na kadhia hii.

Nakufanya FAIRNESS (Haki) juu ya Misamaha hii. Kwasababu Nchi Nyingi za Ulaya Zina Makanisa mengi kuliko Misikiti au Vikundi Vingi vya NGO za Wakristu kuliko Waislamu. Lakini Ruzuku ya Serikali inapogaiwa Hugaiwa Sawa Sawa Nor Matter Who is Religion are?

Kodi za Nchi huwa hazisamehewi Ovyo Ovyo kwasababu tu ya Udini, Ukabila au Ucheo.. Nchi ya Tanzania imekuwa masikini kushindwa hata kumiliki Ndege yake Wenyewe. Na Wananchi Wake Wamekuwa na hali dhaifu na hata kukosa Basic Services kama vile Maji Safi. Na Tanzania imekuwa Omba omba kwa Serikali yake ya CCM, ambayo imetutawala zaidi ya miaka 52 sASA- kukosa democrasia na kukataa maendeleo.

Isipokuwa kufanya Ufisadi kutudunisha sisi Wananchi wa kawaida dhidi ya Umasikini.. Matajiri Wanazidi kutajirika na Masikini wanazidi kumasikinika.. Wananchi wenye asili ya Kikristo Wanazidi Kunawiri kwa Vyeo na Elimu za Juu na Wale Nduguzao Waislamu Wanazidi Kudhalilishwa, kufelishwa na kukamatwa wakiwekwa Jela.

Hii Ndio Tanzania ya Leo, tunalilia Amani na Utulivu, lakini Watanzania hasa ( Raia) lazima tukumbuke kwamba Amani haiji ikiwa Serikali zetu zitafanya Ubaguzi juu ya kundi Fulani.

Ifuatayo hapo chini ni Orodha ya makisio ya MISAMAHA YA KODI kwa magari (TU)?yaliyoingizwa nchini kupitia Taasisi za Dini kuanzia mwaka 2006-2015 (hadi sasa).

1. BAKWATA na Taasisi zake (Shule, Vyuo, Hospitali, misikiti etc)
-magari 82 ya aina tofauti yenye thamani ya Bil 6.8 (Kodi iliyosamehewa Bil 1.9),
2. Kanisa Katoliki na Taasisi zake (vyuo, shule, hospitali, parokia etc) ? Magari 691 yenye thamani ya Bil 59.5 (Kodi iliyosamehewa Bil 19.3),
3. CCT na Taasisi zake (vyuo, shule, hospitali, makanisa etc), magari 527 yenye thamani ya Bil.42.9 (kodi iliyosamehewa Bil.13.8),
4. Makanisa ya Pentecoste na Taasisi zake (vyuo, shule, hospitali, makanisa etc) ? magari 2,719 ya aina mbalimbali yenye thamani ya Bil 186.1 (kodi iliyosamehewa Bil 57.4),
5. Taasisi nyingine za dini (Hindu, Budha etc) magari 203 ya aina mbalimbali yenye thamani ya Bil 36.4 (kodi iliyosamehewa Bil 9.01).

JAUMLA ya Magari yaliyoingizwa nchini kwa mwavuli wa Taasisi za dini tangu Mwaka 2006 (Magari 4,222).
JUMLA ya Kodi iliyosamehewa BIL 102.41. Na ‎Hizi‬ ni pesa zinazotosha kujenga Mabunge matatu yenye hadhi sawa na Bunge la Dodoma na chenge ikabaki.

Kumbuka hii ni misamaha ya Kodi kwa magari tu bado vitu vingine kama Vifaa vya Hospitalini, Vitabu vya mashuleni na vyuoni,biashara za ujenzi na etc?

N:B Je TRA itaomba nyaraka kwa taasisi nyengine za kidini? kwani misamaha kwa taasisi za hizo nyengine inatisha na hayo kuna watu waliuliza bakwata na magani 82 ni ya kazi gani.. Sasa sijui watasemaje na magari 2719, 203, 527 na 691.

Tujadili hili na najua wengine watasema udini kwa sababu limewagusa wao
 
Hii misamaha ifutwe tu, inatumika ndivyo sivyo
 
Kuna wahuni wengi wanaagiza magari kwa mgongo wa kipentekoste kwa sababu usajili wa makanisa ya kipentekoste ni rahisi sana,mtu yeyote unaweza kuanzisha kanisa hata kama hauna kiwanja na kuliita Magwangala Pentekost Church of Tanzania
 
Mara nyingi kazi zinazofanywa na taasis za Dini zina msaada mkubwa kwa serikal,

Huduma za elimu, matibabu, ajira ambazo kwa namna yake zinasaidia kutekeleza wajibu Wa serikali,

Sion msamaha wanaopatiwa kama unalingana na wanachofanya,wanafanya mazuri kupitiliza wanachosamehewa

Wasemehewe tu, maana wana wajibu sawa na msamaha huo, tuache wivu wa kitoto.
 
Hili n suala la kuangaliwa kwa umakini sana! Taasisi za dini zimesaidia sana kutoa huduma kwa waTz wa chini, ila misamaha hii ya kodi inapaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu, na ukisema unaifuta bila taarifa ya jambo hilo n kusababishia hasara zaidi mashirika hayo! Busara itumike
 
Hapa wamepakimbia kuchangia wala hawatojitokeza, kwa Taifa lenye unyonge wa kupindukia ni aibu kubwa kuwaona wachache wakijitanua kwenye taasisi za Dini.

Misamaha yote inastahili kufutwa haraka sana bila ya kuathiri kikundi au dini yoyote, wenzetu wanautajiri mkubwa utajiuliza ni biashara gani wanafanya au ni Kutoa maneno mazuri makanisani na miskitini tuu wanakua hivi?

Kumbe kodi wanakusanya wao badala ya TRA huu ni unyonywaji haustahili kuwepo kwenye taifa hili. Cha ajabu kumbe hata hiyo Bakwata si lolote si chochote?
 
Sasa sijui watasemaje na magari 2719, 203, 527 na 691.

Tujadili hili na najua wengine watasema udini kwa sababu limewagusa wao

Mimi nafikiri kwa kuwa kuna wanaoweza kuwa wanatumia vibaya misamaha ya kodi haitoi uhalali wa kuifuta. Kwani lengo lake ni kuwezesha taasisi zinazohudumia jamii zifanye hivyo. Taasisi hizi zinafanya yale ambayo kodi zinazokusanywa zingefanya mambo hayo. Hivyo uthibiti uongezwe na ukaguzi sahihi ili kila anayeomba msamaha wa kodi athibitishe kuwa kweli anafanya hivyo kwa usahihi na sio kuingia katika biashara na kuua ushindani ulio fair kwa wenye biashara.
 
Unajua tatizo siyo kwamba watu wanapinga misamaha ya kodi au vp lakini hii move the TRA kwa BAKWATA na wachangiaji wengi sana maoni yao yalivyokuwa hapa iliwafanya watu waangalie data za misamaha ya kodi. Ukitilia maanani ya kuwa bakwata ndiyo inayoombea jumuiya karibu zote za kiislam misamaha ya kodi na watu wali question gari 82 za bakwata Tanzania nzima. Sasa ukiangalia Dini nyengine angalia idadi ya gari na misamaha ya kodi waliyoipta na hatujaona movement yeyote katika hilo na kwa bahati mbaya hizi data zipo mitaani kabisa.
 
Je ni hakii kuidai bakwata tuu

Ishu iliyopo sio kwamba bakwata wameagiza magari mangapi ila wameshindwa kuitolea maelezo ya kutosha hiyo starlis iveco waliyoagiza simply..
 
Sidhani kama TRA wamekurupuka katika kuibana Bakwata na hii misamaha.

Kwa kuiangalia tu ile barua nahisi kuwa yale maombi hayakuwa ba maelezo ya kutosha kuhusiana na matumizi ya gari tajwa.

Kuna kosa pia ambalo ninaliona hapa. Bakwata inatumika kama mwamvuli wa kupatia misamaha ya kodi kwa niaba ya taasisi nyingine. Jambo hili ni makosa.
Msamaha unapaswa kuomba na 'mlipa kodi' mwenyewe. Na akivunja masharti ya msamaha basi 'mlipa kodi' ndio anapaswa awajibike. Ninaamini ni kosa katika 'Tax Compliance and Administration' kuipa Bakwata misamaha ya kodi kwa niaba ya walipa kodi wengine.

Kumekuwa na hoja kuwa makanisa na taasis za kikristo zimepewa misamaha ya magari lukuki na hivyo Bakwata wanaonewa kwa sababu ya dini yao.
Hili nalipinga. Bakwata naamini kabisa kuwa Bakwata hawajanyimwa sababu ya DINI. Bali kutokana na maombi ya msamaha kutoendana na shughuli zilizosajiliwa za Bakwata. Hiyo inaleta shaka na kuhitaji kufanya "audit" ya msamehewa na misamaha aliyopewa.
Kwa mfano shule moja ya kidini (taasis) haiwezi pewa misamaha ya magari 30 bila maelezo ya kutosha na kuthibitisha kufuata masharti ya misamaha iliyopita.

Hata taasisi hizo nyingi za kikiristo kila moja huomba na mara kadha wa kadha taasisi hizo mbali mbali hunyimwa pia. Ni kwa sababu tu watu hawaweki mitifuano yao na TRA kwenye mitandao.

Na hata wafanyakazi wanaostahili misamaha ya kodi za magari nao hunyima misamaha hiyo pale maelezo au vigezo vinapokuwa havikidhi.

Tuache kuleta udini kwenye mambo ya kiutawala na udhibiti hasa wa kodi.
Tuwe makini na misamaha yote. Mambo ya NGO za Ukimwi yatajirudia kwa kasi, ambapo watu walijinufaisha na misaada lukuki ikiwa ni pamoja na misamaha ya kodi.
 
Unajua tatizo siyo kwamba watu wanapinga misamaha ya kodi au vp lakini hii move the TRA kwa BAKWATA na wachangiaji wengi sana maoni yao yalivyokuwa hapa iliwafanya watu waangalie data za misamaha ya kodi. Ukitilia maanani ya kuwa bakwata ndiyo inayoombea jumuiya karibu zote za kiislam misamaha ya kodi na watu wali question gari 82 za bakwata Tanzania nzima. Sasa ukiangalia Dini nyengine angalia idadi ya gari na misamaha ya kodi waliyoipta na hatujaona movement yeyote katika hilo na kwa bahati mbaya hizi data zipo mitaani kabisa.
Sina hakika kama wote tuna uelewa wa pamoja kuhusu hii misamaha TRA kupitia kwa meneja wa misamaha Bi Mwantumu Salimu haijakataa kutoa misamaha kwa BAKWATA ila wanahitaji nyaraka kadha ili kujiridhisha kuwa ni kweli misamaha ya awali ilikua inatumika ipasavyo na hii hufanyika kwa taasisi zote za dini, kuna tetesi kuwa baadhi ya taasisi wakipata msamaha baada ya muda mfupi unakuta hayo magari yanabadilishwa umiliki kwenda kwa mtu binafsi na unapobadili umiliki unaenda tena TRA kwa hiyo wanaposema upeleke kadi ya gari wao tayari wanajua kuwa utakwama kwa sababu msamaha wa kwanza uliutumia vibaya kwa kubadisha umiliki kwa kisingizio cha taasisi ya chini.
Uwingi wa magari ktk taasisi za kikristo inategemea na shughuli za kanisa pia kuwa nyingi mfano kanisa katoliki wanna seminari nyingi hospitali karibu kila mkoa tena kubwa makiungu na st Gasper Singida, peramiho na litembo ruvuma, bugando MWANZA, st. Gema Dodoma Mbulu Manyara st Francis Ifakara ndanda masasi n.k. nimetaja chache na hizi ni hospitali kubwa sio zahanati zinahudumia watu wengi shale za msingi na sekondari kila mkoa sasa wenzetu hawa vitu vyao vipo ktk rekod ukitaka nyaraka zozote kuhusu magari yao unapewa kwetu tunasema ni vigumu kupatikana hapo tatizo ni la nani? kwa upande Wangu nimetembea maeneo mengi nimekuta hospital nyingi za makanisa zikitoa Huduma kuliko hata za serikali muundo na taratibu za uendeshaji wa makanisa ni tofauti na jinsi tunavoendesha misikiti, tembelea ofisi ya askofu uone mtiririko wa uongozi mpaka parokia inakua na magari unaweza kuta jumbo lina parokia 20 na kila parokia ina gari 2-3 kutegemea na ukubwa wa hiyo parokia na hata paroko akihamishwa anakadhi Mali na magari kwa anaemuachia kwa utaratibu wa maandishi, sasa tujiulize kwetu mfumo wa uendeshaji wa taasisi upo mpaka ngazi ipi?

Nalog off
 
Haya makanisa ya Pentecoste kwann yasifungiwe jamani,
Maana mtu anaanzisha kanisa anajibana kwny kichochoro yan mtaa mmoja una makanisa hata 10 matokeo yake wanaanza kurushiana vijembe,

Nadhani serikali iangalie upya juu ya haya makanisa yanayoibuka kila uchwao,
Ndio na mafisadi wanajichomeka humo humo kufanya yao.
 
Nimependa hii wote waombwe kuleta walichowaomba Bakwata wawape.

Duh mbona hao wa magari elfu hawajaombwa?

Hizo kodi zikatwe kabisa.
 
Haya makanisa ya Pentecoste kwann yasifungiwe jamani,
Maana mtu anaanzisha kanisa anajibana kwny kichochoro yan mtaa mmoja una makanisa hata 10 matokeo yake wanaanza kurushiana vijembe,

Nadhani serikali iangalie upya juu ya haya makanisa yanayoibuka kila uchwao,
Ndio na mafisadi wanajichomeka humo humo kufanya yao.

Sasa ihusishe hii post yako na mada ya misamaha ya kodi.
Vinginevyo ihamishie kwenye mjadala husika ili michango yakinifu itolewe.
 
Hivo Hatuna haja ya Kubisha na kusema kwamba Serikali ya CCM au Serikali ya Muungano Haina Dini.. Ushahidi Mdogo ambao ulikuwa Unajulikna kutokana na Unawiri wa Kundi la Dini Fulani na Unyonyaji au UDhoofishaji wa Kundi la Dini Nyengine ni Huu hapa.

Hapa tunaweza kuona Tofauti kubwa ya Misamaha ya Kodi ya Taifa Baina ya BAKWATA na MAKANISA. Na Hii nataka niwambie Wasomaji kwamba sio FITINA ya Kidini bali Tunataka Nchi Zetu Mbili Tuzipendazo yaani Tanganyika na Zanzibar na Serikali ya Muungano. Ziwe INVIGILANT na kadhia hii.

Nakufanya FAIRNESS (Haki) juu ya Misamaha hii. Kwasababu Nchi Nyingi za Ulaya Zina Makanisa mengi kuliko Misikiti au Vikundi Vingi vya NGO za Wakristu kuliko Waislamu. Lakini Ruzuku ya Serikali inapogaiwa Hugaiwa Sawa Sawa Nor Matter Who is Religion are?

Kodi za Nchi huwa hazisamehewi Ovyo Ovyo kwasababu tu ya Udini, Ukabila au Ucheo.. Nchi ya Tanzania imekuwa masikini kushindwa hata kumiliki Ndege yake Wenyewe. Na Wananchi Wake Wamekuwa na hali dhaifu na hata kukosa Basic Services kama vile Maji Safi. Na Tanzania imekuwa Omba omba kwa Serikali yake ya CCM, ambayo imetutawala zaidi ya miaka 52 sASA- kukosa democrasia na kukataa maendeleo.

Isipokuwa kufanya Ufisadi kutudunisha sisi Wananchi wa kawaida dhidi ya Umasikini.. Matajiri Wanazidi kutajirika na Masikini wanazidi kumasikinika.. Wananchi wenye asili ya Kikristo Wanazidi Kunawiri kwa Vyeo na Elimu za Juu na Wale Nduguzao Waislamu Wanazidi Kudhalilishwa, kufelishwa na kukamatwa wakiwekwa Jela.

Hii Ndio Tanzania ya Leo, tunalilia Amani na Utulivu, lakini Watanzania hasa ( Raia) lazima tukumbuke kwamba Amani haiji ikiwa Serikali zetu zitafanya Ubaguzi juu ya kundi Fulani.

Ifuatayo hapo chini ni Orodha ya makisio ya MISAMAHA YA KODI kwa magari (TU)?yaliyoingizwa nchini kupitia Taasisi za Dini kuanzia mwaka 2006-2015 (hadi sasa).

1. BAKWATA na Taasisi zake (Shule, Vyuo, Hospitali, misikiti etc)
-magari 82 ya aina tofauti yenye thamani ya Bil 6.8 (Kodi iliyosamehewa Bil 1.9),
2. Kanisa Katoliki na Taasisi zake (vyuo, shule, hospitali, parokia etc) ? Magari 691 yenye thamani ya Bil 59.5 (Kodi iliyosamehewa Bil 19.3),
3. CCT na Taasisi zake (vyuo, shule, hospitali, makanisa etc), magari 527 yenye thamani ya Bil.42.9 (kodi iliyosamehewa Bil.13.8),
4. Makanisa ya Pentecoste na Taasisi zake (vyuo, shule, hospitali, makanisa etc) ? magari 2,719 ya aina mbalimbali yenye thamani ya Bil 186.1 (kodi iliyosamehewa Bil 57.4),
5. Taasisi nyingine za dini (Hindu, Budha etc) magari 203 ya aina mbalimbali yenye thamani ya Bil 36.4 (kodi iliyosamehewa Bil 9.01).

JAUMLA ya Magari yaliyoingizwa nchini kwa mwavuli wa Taasisi za dini tangu Mwaka 2006 (Magari 4,222).
JUMLA ya Kodi iliyosamehewa BIL 102.41. Na ‎Hizi‬ ni pesa zinazotosha kujenga Mabunge matatu yenye hadhi sawa na Bunge la Dodoma na chenge ikabaki.

Kumbuka hii ni misamaha ya Kodi kwa magari tu bado vitu vingine kama Vifaa vya Hospitalini, Vitabu vya mashuleni na vyuoni,biashara za ujenzi na etc?

N:B Je TRA itaomba nyaraka kwa taasisi nyengine za kidini? kwani misamaha kwa taasisi za hizo nyengine inatisha na hayo kuna watu waliuliza bakwata na magani 82 ni ya kazi gani.. Sasa sijui watasemaje na magari 2719, 203, 527 na 691.

Tujadili hili na najua wengine watasema udini kwa sababu limewagusa wao

Swala sio ukubwa wa misamaha. Bakwata hawajahojiwa kwa nini wamevuka kiwango cha misamaha, la hasha.
Swala ni vigezo vya msamaha wa kodi na masharti yake.
Ukivunja masharti ya msamaha wa kodi ni msala. Haijalishi we ni mkristo au muislam.
Kama wamevunja sheria ya kodi basi wamevunja tu, dini haihusu.
Tutakujaleta dini hadi kwenye ICD na makontena eti mbona watuhumiwa wengi wana majina ya dini ya kiislam. Basi wanaonewa.
Hiyo ni dhana potofu. Ulipaji kodi na ufuata sheria haujali dini.
Bakwata watekeleze matakwa ya kisheria na mjadala upite.
 
Back
Top Bottom