Misamaha miwili yenye uzito tofauti

Misamaha miwili yenye uzito tofauti

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,882
Reaction score
828,453
Kwanza uungwana ni vitendo.. Na kujishusha ni kuonesha ukomavu wa akili.. Lakini vilevile kutubu ni kuonesha majuto na kujirudi kulikojaa tafakuri
Lakini yote hayo huwa na maana ama hukosa maana kama yamefanyika kwa kushurutishwa ama kulazimishwa.. Kama mlengwa ni mtu mmoja ama ni jamii
Job Ndugai alimuomba boss wake msamaha.. Mazingira yakionesha wazi "alishurutishwa" kufanya hivyo! Imagine hata viatu alikuwa hajafunga gidamu na vilikuwa oversize! Je kabla ya kuomba radhi mbele ya cameras alikuwa wapi? The walls has a story to tell!
Msamaha wake uligeuka dhihaka na kejeli kwa jamii.. Huku wengine wakiuchukulia kama kituko cha karne! Maana haukuwa na faida yoyote kwa jamii
Humphrey Pole pole kaomba msamaha kwa jamii.. Tena kwa kurudiarudia.. Pamoja na ukubwa wa makosa yake tofauti na ya Ndugai bado msamaha wake umeonekana wa maana zaidi.. Kwakuwa ameiomba jamii na bila shuruti
Msamaha wake umemjenga badala ya kumbomoa.. Msamaha wake umepokelewa kwa heshima kubwa, kwakuwa aliyoyasema yameifungua macho jamii na yanaumiza sana!
Likitokea la kutokea leo Pole pole atakuwa na HERO kwa jamii na msiba wake utakuwa tofauti kabisa na wa Ndugai
Hii ni nguvu ya msamaha kujishusha na kujutia.. Lakini je unamuomba nani na kwa sababu gani
1755843386431.jpg
IMG-20250822-WA0006.jpg
 
Ushauri wangu kwa wale machawa wanaoishi kwa kutegemea kubusu makalio ya watawala mithili ya Tlaatlaah Lucas Mwashambwa johnthebaptist na wengineo wekeni akiba ya matusi na kejeli zenu maana kuna dalili upepo utabadilika na walio kwenye hatamu hawatokuwa kwenye hatamu tena wale mnaowakejeli ndio watakuwa juu.

Sasa ili msiwe na haja ya kubadili majina yenu katika kuanza kusifia mnaowadhihaki sasa ili mpate kula yenu, ni busara mkang'ata na kupuliza.
 
Hao hata kabla ya hili la Polepoe, wana ID za kutosha humu.
 
Kwanza uungwana ni vitendo.. Na kujishusha ni kuonesha ukomavu wa akili.. Lakini vilevile kutubu ni kuonesha majuto na kujirudi kulikojaa tafakuri
Lakini yote hayo huwa na maana ama hukosa maana kama yamefanyika kwa kushurutishwa ama kulazimishwa.. Kama mlengwa ni mtu mmoja ama ni jamii
Job Ndugai alimuomba boss wake msamaha.. Mazingira yakionesha wazi "alishurutishwa" kufanya hivyo! Imagine hata viatu alikuwa hajafunga gidamu na vilikuwa oversize! Je kabla ya kuomba radhi mbele ya cameras alikuwa wapi? The walls has a story to tell!
Msamaha wake uligeuka dhihaka na kejeli kwa jamii.. Huku wengine wakiuchukulia kama kituko cha karne! Maana haukuwa na faida yoyote kwa jamii
Humphrey Pole pole kaomba msamaha kwa jamii.. Tena kwa kurudiarudia.. Pamoja na ukubwa wa makosa yake tofauti na ya Ndugai bado msamaha wake umeonekana wa maana zaidi.. Kwakuwa ameiomba jamii na bila shuruti
Msamaha wake umemjenga badala ya kumbomoa.. Msamaha wake umepokelewa kwa heshima kubwa, kwakuwa aliyoyasema yameifungua macho jamii na yanaumiza sana!
Likitokea la kutokea leo Pole pole atakuwa na HERO kwa jamii na msiba wake utakuwa tofauti kabisa na wa Ndugai
Hii ni nguvu ya msamaha kujishusha na kujutia.. Lakini je unamuomba nani na kwa sababu ganiView attachment 3448713
Msamaha wangu una masharti
 
Makosa ya Polepole yalikuwa ya collective responsibility.

Licha ya nguvu aliyokuwa nayo, Polepole ni mmoja wa viongozi wachache wa awamu ya tano ambao hawakuwa na scandal yoyote.

Ile issue ya V8 hata haikuwa na uzito kama wanasiasa tulivyoitafsiri.

All in all; tuendelee ku #kataawahuni
 
Anaandika Askofu Steven Munga

Nimemsikiliza Balozi Polepole akiongea. Niseme machache katika niliyosikia.

(1) Ameomba msamaha kwa makosa aliyoshiriki yanayoligharimu taifa leo.

(2) Ameongea mambo magumu (ambayo yalisikika siku za nyuma na sasa ni kama amethibitisha) na jinsi CCM ilivyoshikiliwa na wana mtandao.

(3) Ameongea kwamba mifumo ilivyo imekwisha kuonyesha ushindi kwa CCM. Muundo wa mfumo CCM - NIDA - Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Hakika mbeleko moja haiwezi kubeba watoto wawili.

(4) Amesema uchaguzi ni wa chama kimoja na vingine ni wadau kwa makubaliano maalum.

(5) Amesema hazuii mtu kwenda kupiga kura bali afanye hivyo akitambua kuwa hawezi kubadilisha matokea.

(6) Amesisitiza zifanyike juhudi za makusudi na za wazi kuthitisha aliyosema juu ya mifumo ya uchaguzi na ikiwezeka marekebisho yafanywe kabla ya kwenda kwenye uchaguzi.

(7) Ameendelea kushauri Lissu aachiliwe huru ili mambo yaendelee kwa taratibu.

(8) Haoni sababu ya kuombea uchaguzi kwani matokeo yanajulikana kulingana na mifumo ilivyotegwa.

Nimefanya ufupisho wa mengi niliyoyasikia. Nitahitaji muda kidogo ili kuomba na kutafakari kama raia mwema ndipo niweze kufanya tathmini ya mambo haya ya kufadhaisha. Tukumbuke kwamba wapo Watanzania wenzetu wanaojifanya wanaipenda Tanzania lakini ukweli ni kwamba wanaila na kushiba Tanzania. Hawana mchango kwa Tanzania bali Tanzania ina mchango mkubwa kwa mafanikio yao. Tufanyeje ili kukata mirija yao?

Nilizoea kuhimiza kuliombea taifa letu katika mambo ya haki na amani. Tuendelee kuomba hivyo na kujenga dondoo zingine kulingana na aliyoongelea Polepole.

Mungu ibariki Tanzania!
20250729_010133.jpg
 
Anaomba msamaha wake baada ya chama chake kukataa matakwa, maana yake CCM ingesema OK, Samia hata gombea na mchakato urudi chimwaga HP asingeomba samahani kwa jamii naye angeendelea kuwa sehemu ya wala keki.

Siwezi kuamini msamaha wa mtu anayepigania vita ya maslahi.

ndani ya Benghazi Libya.
 
Back
Top Bottom