Misaada: To hell with it!!

Ni aibu kubwa sana kunyimwa misaada kwa sababu za uhalifu dhidi ya ubinadamu , hii maana yake ni kwamba mnanyimwa misaada kwa vile viongozi wenu ni wakatiri mithili ya wanyama wa mwituni , ni fedheha kubwa sana kwa nchi
Wanatunyima kwasababu hatutaki kukosea wakati wa kujamiiana. Hizo zingine ni icing tu kwenye keki.
 
Huu ni mtazamo wa kizungu. Uwa nawaambia watu demokrasia will never work out with Africans. Siyo utamaduni wetu.
 
Kweli kabisa, kuna wakati mzee wa msoga alisisitiza kutembea na bakuli kwa hao matajiri, ilikuwa aibu ilioje! Bado tumedumaa na hayo, kama ya sehemu za imani, tukifikiri tukitoa leo buku kwa omba omba aliyemzima wa afya tunamsaidia! Kumbe....
Misaada ni silaha wanazotumia hao walioendelea kuweza kutu-control, tena ile ya magharibi inayokuja na vitisho na kila ya aina ya vipengele.
Pia wanaoalialia na hili sana, ni vyama kinzani, sababu hata vyama vyao vyaendeshwa kwa misaada, viongozi wanashibisha matumbo yao kwa misaada, sidhani kama utaeleweka..
 
Tatizo watanzania vichwani mwetu tumeweka mambo ya mazoea sasa Magufuli yupo tofauti sana maamuzi magumu anayo yachukua ni vitu ambavyo watu hawakuzoea kwa hiyo sishangai kuona kila kona ya nchi hii kwa sasa watu wanalalamika .
 
kwenye bajeti ya maendeleo Tanzania/own source tunatoa ngapi? hao wazungu wanatoa ngapi.tuanzie hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…