Misaada: To hell with it!!

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,207
Reaction score
144,106
Kumekuwepo na taarifa kuwa eti tumenyimwa misaada na nchi za jumuiya ya Ulaya, Marekani, na sehemu zingine.

Sababu kuu inayotajwa ni kuzorota kwa hali ya haki za binadamu nchini chini ya huu utawala wa Rais John Pombe Joseph ‘Jiwe’ Magufuli [huyu ngosha ana majina mengi kweli...mara Tingatinga...sijui Sizonje....but I digress].

Nachotaka kuzungumzia hapa si hayo madai ya kuzorota kwa hali ya haki za binadamu. Hiyo ni hoja ya siku ingine.

Hapa nataka kuzungumzia huu upumbavu wa misaada.

Kwa tunaofahamiana humu tokea 2004/2005/ 2006/ na 2007, watakuwa wanakumbuka msimamo wangu kuhusu hii misaada ya maendeleo ambayo taifa letu limekuwa likipewa tokea nianze kupata/ kupatwa na fahamu.

Kwa maneno mengine, ni muda mrefu mno sasa tumekuwa tukipewa hii misaada ya maendeleo.

Kilicho cha ajabu kwangu ni: mbona bado tu hatuendelei? Hiyo si inaitwa misaada ya maendeleo? Miongo na miongo tunapokea hiyo misaada lakini ukiangalia maendeleo yenyewe hakuna.

Mbaya zaidi, tuna idadi kubwa tu ya watu [kwa makadirio yangu] ambao wanaipenda sana hii misaada ya maendeleo. Yaani wanapenda sana sisi kupewa hii misaada na hizo nchi.

Sasa ngoja nirudie ambacho nimekuwa nikikisema miaka yote hii ya uwepo wangu hapa JF na huko kwingineko.

Siipendi hii misaada. Siitaki kabisa. Naamini imetulemaza sana hadi kufikia hatua ya kudhani bila kupewa hiyo misaada basi hatutoweza kuendelea.

Naamini kabisa tunaweza kuendelea kiuchumi bila hata hiyo misaada isiyo na msaada wowote. Ni kiasi cha kuamua tu na kubadili mindset yetu kutoka kwenye ‘can’t do’ kwenda kwenye ‘can do’.

Tuna hali ya kujiona hatuwezi kufanya mambo flani flani bila ya kusaidiwa na flani. Mara zote huwa najiuliza, hivi hao wanaotupa hiyo misaada, wao nani aliwasaidia?

Na sizungumzii misaada ya hapa na pale wakati wa majanga ya kiasili, vita, au mazingira fanani. Kwa kawaida binadamu huwa tunapitia changamoto na hatuna budi kusaidiana saidiana pale inapobidi.

Hapa nazungumzia hii misaada isiyoisha ambayo huitwa misaada ya maendeleo.

Siitaki. Siipendi. Naichukia kwa hisia kali sana. Na nasema watunyime tu hiyo misaada ili tuamke toka kwenye huu utegemezi wa kipumbavu tulionao.

Bila hiyo misaada yao tutaangamia au?

Gonga ‘Like’ kama unakubaliana nami.
 
To some extent you are right, lakini kumbuka ili uondokane na utegemezi lazima uwe una-create value within your country uweze kuwauzia hata watu wengine nje ya nchi na u-broaden tax base by increasing a number of rich people who can create employment. Sasa ukiwa na serikali inayowachukia matajiri jua hata kama unataka kujitegemea haiwezekani maana you are stepping backward instead of moving forward. In fact we on the verge of collapsing..
 

Ndo maana nasema kwamba ‘tunaweza’.

Tatizo tu ndo sijui ni nini hasa...hatujiamini? Hatuna ubunifu? Hatuna akili?

What is lacking in us?
 

Ain’t necessity the mother of invention??
 
Ni aibu kubwa sana kunyimwa misaada kwa sababu za uhalifu dhidi ya ubinadamu , hii maana yake ni kwamba mnanyimwa misaada kwa vile viongozi wenu ni wakatiri mithili ya wanyama wa mwituni , ni fedheha kubwa sana kwa nchi
 
Ndo maana nasema kwamba ‘tunaweza’.

Tatizo tu ndo sijui ni nini hasa...hatujiamini? Hatuna ubunifu? Hatuna akili?

What is lacking in us?
Hatujawa tayari kujibeba
Tumetepweleka
Ni wavivu
Ni wapumbavu
Njaa haiui mtu,lazima atakurupuka tu na atafanya kitu.
 
Ni aibu kubwa sana kunyimwa misaada kwa sababu za uhalifu dhidi ya ubinadamu , hii maana yake ni kwamba mnanyimwa misaada kwa vile viongozi wenu ni wakatiri mithili ya wanyama wa mwituni , ni fedheha kubwa sana kwa nchi

Yaweza kuwa ni baraka iliyojificha.

Ndo tuanze kujitegemea sasa.

Halafu, hata hao watoa misaada rekodi zao za haki za binadamu zina mushkeli vilevile...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…