Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 5,768
- 21,871
MISAADA: JE NI PICHA YENYE SURA MBILI?
Am just curious!!!
Ni nani hasa anapaswa kubeba sura ya mpewa msaada. Inajulikana wazi hawa wenzetu hawatupi misaada bure kama wanavyojinasibu, they demand something in return. Iwe ni materialistic in nature or idealistic in nature, but in real picture hii sio misaada as long as inakuja na conditions.
Sasa why sisi ndio tuonekane ni wasaidiwaji wakati in real sense it’s a mutual exchange. Hata historia inasema kipindi wakoloni wanafuata malighafi kwetu kama madini na malighafi za kilimo walizipata either for free or in exchange with things like clothes, lakini kiukweli wao ndio walikuwa wanachukua vitu vyenye thamani zaidi kuliko walivyovileta kwa sababu walichukua malighafi ambazo ndizo walizitumia kutengeneza refined products ambazo walituletea kama zawadi ili kujipatia hizo malighafi. Kwa hiyo ni kama cycle fulani hivi ya ka mchezo baina ya mwerevu na mjinga.
Hata kwa upande wa mikopo hali ni ileile. Mikopo mingi hailipiki kiurahisi na kama mikataba ilosainiwa inaruhusu wadai wetu kujimilikisha rasilimasi/malighafi yoyote basi hawatasita kufanya hivyo, mfano sakata la China na Zambia.
Sasa ni vizuri sisi kama Waafrika tujiulize kwa akili za Kinyerere na Kimandela, hii misaada na mikopo inatusaidia sisi ama wao ama both parts benefit from the relationship?. Kinachotukwamisha sisi Waafrika sio akili kama tunavyoambiwa, bali ni approach. Akili tunazo sana kinachotukwamisha mpaka tuko hapa tulipo hatuna usemi ni kukosea “namna/approach”.
Sasa naombeni mnisaidie ndugu zangu, ni sisi ndio tunaopokea misaada ama sisi ndio tunaotoa misaada?
Am just curious!!!