Miruzi mingiii, humpoteza MBWA!

pitamozes

Member
Jun 10, 2013
28
2
Pamoja na sababu nyingine nyingi zilizochangia watoto wa kidato cha nne kuferi, hii ya miruzi mingi nathani ndio iliyompoteza MBWA!
Miruzi hii imetokana na wizara ya ELIMU kutokua na sera ya ELIMU inayotambulika. Kila waziri atakae ingia madarakani na sera yake.
Hebu ona, huyu PHY peke yake na CHE peke yake, huyu PHY with CHE, ili mradi tu. Utakubariana na mm, kwa wale waliosoma miaka ya 80,90, mpaka 2000, wakikutana Leo hii, story zao za Elimu zinafanana.
Ninani kati yao atakua haijui hadithi ya JUMA NA ULEDI? SADIKI NA CHITEMO JE? Vp kuhusu SIKU YA GULIO? MZEE TOLA ANKULA GIZANI na nyingine nyingi.
Leo hii somo moja la kidato kimoja vitabu zaidi ya vitatu, mtoto anashindwa asome kipi? Hebu cheki na hii, mtoto wa darasa la kwanza anakua na masomo zaidi ya matano!? Enzi zetu yalikua matatu tu, hapa hisabati, huku mwandiko na pale English.
Waziri wa Elimu, Eti watotot siku hizi hawasomi wanashinda FACEBOOK! Facebook ni moja kati ya njia za kujifunza, ni wangapi leo hii hawajui kutumia facebook kwa sababu hawajajifunza? Tatizo ni kwamba, hatuwafundishi watoto kutumia hii mitandao ya kijamii kwa kujifunza. Nani mwenye jukumu hilo mimi cjui!
Ni hayo tu kwa Leo........
 
Back
Top Bottom