Katika kipindi cha awamu ya nne kulikuwa na kaulimbiu ya miradi ya gesi kila kona. Kulikuwa na visima vikiwa vimechimbwa ndani ya bahari na matayarisho ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kwa ajili ya kuuza nchi za nje. Vile vile kulikuwa na mpango wa kutandaza mabomba mpaka Dar ili wananchi waweze kufaidi gesi hii. Tanesco pia imejenga vituo vya kupokelea gesi Dar es Salaam. Kama kweli tuliwekeana mkataba kwa ajili ya gesi mbona sasa sioni kinachoendelea kwa ajili ya miradi ya gesi?. Kama mikataba ya gesi ilikuwa ya hovyo je hatuwezi kurekebisha?. Kama tumewekeza kiasi hicho sasa kipi kinaendelea?.