Miradi mikubwa ya maendeleo ya nchi na Idukilo yetu

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Huku Idukilo leo nimewadokeza kuhusu SGR. Mmoja akafikiri ni kifupi cha neno sigara akaniambia sasa kutufanya sisi tuvute sigara ndiyo maendeleo.

Kuhusu flyover mwingine kafikiri ni ndege na kudai kwamba alikuwa anasikia milio tu zikipita kwenda kutua Mgodi wa Mwadui kuchukua almasi. Nikamwambia ukiacha flyover kuna mradi wa kununua ndege pia.

Akasema basi anashindwa kutendanisha flyover na ndege. Nikamwacha na kutafakari. Nikamkuta jirani yangu mwingine nikamdokeza kuhusu treni ya mwendo kasi itayoishia Dodoma. Akaniuliza inafafanaje?

Nikazidi kumweleza ilivyo mwishowe akaniuliza itafika lini huku kwetu Idukilo ituletee na chakula nikashindwa kumjibu nikapiga bla-bla na kupiga miayo.

Cha kufurahisha jirani yangu naye akapiga mwayo kama mimi kuashiria tuna njaa kali sana, msosi hakuna.
 
Back
Top Bottom