Mipasho CCM: Nahisi ni danganya toto... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mipasho CCM: Nahisi ni danganya toto...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Mar 26, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ........Siku za karibu kumekuwa na mipasho inayoendelea kati ya viongozi wa ngazi za juu wa chama cha CCM(napata hata kichefuchefu napokitamka) na baadhi ya jumuiya zake kama ile ya UVCCM nk..Nimeanza kuwa na wasiwasi na hawa jamaa kama sio ni njia ya kututoa na kutupoteza watanzania kwenye mada za msingi kama Katiba,Malipo ya Dowans,Mikataba mibovu ya Madini,Umeme nk.Ukifatilia kwa makini zaidi utagundua kuwa magazeti mengi na vyombo vingine vya habari kwa takribani mwezi mmoja vimejaa hiyo mipasho...and even threads nyingi na post zetu wanaJF zimejaa hayo matukio....Je hii sio njia madhubuti ya kututoa kwenye mambo ya msingi?
   
 2. m

  masingo sharili Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haswaaaa. Bora tudili na mambo mengine kwani hawa mabwana wanatafuta umaarufu kupambana na kasi ya wanaharakati.
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu inawezekana maana hawa jamaa ni mabingwa wa mbinu za medani ya kisiasa na fitna.
   
 4. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni wafitini wakubwa, ni mwanzo maana waliona chadema inatajwa kila mahala sasa wameamua kuanza namna ile
   
 5. J

  Jonas justin Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa wana yao mambo nyuma yapazia...
   
 6. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Acheni inyeshe ili tuone panapovuja.
   
 7. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CDM inajadiliwa kwa mazuri na watu wengi (wachache mabaya) kinyume chake ni kwa CCM
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CHADEMA ACHENI WANYANG'ANYI WA TAIFA HILI WAPARUANE WAMALIZANE WENYEWE
  HUKU 'NGUVU YA UMMA' TUKIWASUBIRI NJIA PANDA YA KURA!!


  Jamani siku zote mjue saikolojia hii rahisi ya kwamba kote dunia hakuna Mtu, Chama na au taifa KIDUME mpaka kwanza kuwepo na Mtu, Chama na Taifa linalojihisi K-INZI pindi tu wote wajitokezapo mbele ya hadhara.

  Hivyo nymbo zisizopata kituo toka kwa wenyeviti wa vyama nchini kama vile Mhe Kikwete, Mrema, Mbatia, Lipumba na hivi sasa Mzee Mapesa na santuri yake mpya ni ujumbe mzito wa ujumbe uliojificha nyuma ya ujumbe tuuonao kiharaka kwenye kelele hizo!!

  Sana sana labda nichukue fursa hii kukiomba CHADEMA kiwatendee haki hawa watangazaji wa hiari waliojikita zaidi kwenye kujulisha Wa-Tanzania tulioamka akilini; juu ya uwepo, nguvu na shughuli thabiti za chama hiki kwa walalahoi, taifa, na dunia kwa ujumla!!

  Nasema hivi kwa sababu nimeona muda mrefu waheshimiwa kama akina Mzee Makamba, mbali na ratiba zao ngumu kweli kikazi, wakijitolea hivi hivi na wala msitambue juhudi zake, Mhe Kikwete kufanya hivo kwa mapenzi makubwa kila apitako (na wala asifanye kwa CCM) huku nyie wala hamuoni. Mama Simba tena ndio usiseme katika juhudi hizi za hiari kukitangaza zaidi CHADEMA bila malipo.

  Naongeza hiviii; acheni wakatutangazie zaidi chama hawa akina TBC1, Rweyemamu wa Magogoni, Chalii Ngoyayi, wakubwa kama Kepteni Chiligati, Benno Malisa, Riz1 Kikwete, Hamad Rashid, Haruna Lipumba a.k.a Mgombea wa Kudumu CUF ... listi ni ndefu sana mpaka najiuliza Dr Ali Mohamed Shein, Maalim Seif, Mzee Msuya, Mzee Warioba, ... wao kukibania CHADEMA matangazo ya hiari katika mkumbo huu wenzetu mnamaana gani??

  Ukiniuliza mie ninavyoendelea kushuhudia mishale mbali mbali kwa CHADEMA hadi baadhi ya maafisa wetu serikalini nao kujichagulia kuwashambulia wapendwa wao tena bila aibu, yooote kwangu ni kichekesho kisicho na kituo!!

  Mwenzenu ninavyoumwa mbavu hapa kuona watu mnavyojichosha pumsi ya gharama kwa kujadili MENDE zinapoigonga KABATI kiajali tu tena kule katika kuruka ruka kwao ovyo tu ndani jiko lilizoeleka kwa kwa mtaji wake wa uchafu kwa wezi na wanyang'anyi wengi tu ndani ya taifa hili, huku zikitafutia makombo ya wafalme baada ya kusaza na kuvimbiwa pia, mwenzenu mbavu katika na machozi ya furaha kusimama machoni!!!

  Acheni hao watumwa wa hiari kwa MFUMO FISADI wajimalize wenyewe kwani kupayuka kwao ovyo ni salamu tosha kwamba kweli CHADEMA na 'Nguvu ya Umma' kote nchini kweli TUMEWASHIKA pachungu sana tena pasipoelezeka zaidi ya mtu mzi kusikika kuendelea tu kutoa gugumia tena wa masharikiiii.

  Mwisho ningemuuliza Mzee Mapesa akawaeleze Wa-Tanzania mradi aliyonayo ndani ya Kamati ya Mahesabu Mapato na Matumizi ya serikali, hata asipende kubanduka mle, waka wenzake hali gumu balaa huku mitaani wakati yeye akiendelea kuchota 10% ya kila fungu la UFISADI kama vile RICHMONDI, DOWANSI, MEREMETA, MRADI WA RADA, EPA ... kabla ya kuzifumbi macho, lakini bora nisubiri siku nyingine.
   
Loading...