Mipango YAO...Kuondoa Umasikini WETU! A Must Read article | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mipango YAO...Kuondoa Umasikini WETU! A Must Read article

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by IsangulaKG, May 28, 2011.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Source: Opportunities for Youths in Tanzania: Their PLANS to reduce OUR Poverty!...Mipango YAO kuondoa Umasikini WETU!
  Nikiwa katika safari yangu ya kikazi kuelekea Kilimarondo..katika barabara ya vumbi yenye kilometa zaidi ya mia kutoka katika mji wa Nachingwea,ni asubuhi sana,napita katika kibanda cha makuti kilicho na Matundu mengi ukutani mithili ya Chujio au neti ya Mbu! Nikalazimika kumwomba dereva asimame..Hapo uani nikamkuta baba wa makamo ametandika mkeka amejilaza,huku paa likisuiri upepo mdogo tu lidondoke,nikachungulia kwa kuibaiba pale ndani sikuona dalili ya kiti zaidi ya kuwaona watoto wadogo kama wanne hivi wakigombea bakuli la kiporo cha Ming'oko huku mmoja tu ndiye alikuwa na kishati bila bukta na watatu wale kakiwemo na kabinti walikuwa na vichupi vichakavu sana..juu ya paa ya ile nyumba bendera ya Kijani ilikuwa ikipepea kwa matumaini....


  Haya badondiyo Maisha ya watanzania walio wnegi huko vijijini katika karne hii. Japo serikali hubeba lawama kwa kiasi fulani lakini lawama kubwa zinamwendea huyu mzee. Mzee ambaye nyuma ya Nyumba yake tu kuna pori lenye miti imara ambayo hukatwa na kutengenezewa fanicha zilizo ikulu au Movenpick! Japo yeye kashindwa kabisa kukata miti hiyo kukarabati nyumba yake. Mzee ambaye japo alijua kuwa hana uwezo wa kuwajengea watoto misingi bora ya Maisha...bado aliamua kumpa mimba mkewe na wakazaa watoto wengi.
  Serikali inabeba lawama kwa Upande wake kwani nimesikia mikakati mingi sana..MKUKUTA,MKURABITA na mingine yenye majina ya ajabu ajabu mingi tu. Serikali hiyo hiyo ikajenga soko la kisasa kabisa la Mazao hapo kijijini ambalo hadi sasa limefungw kwa kuwa wanakijiji hawana mazao ya kuuza. Serikali hiyo hiyo ikajenga Zahanati kubwa na kisha ikashindwa kuhakikisha wahudumu bora na madawa yanapatikana. Serikali hiyo hiyo ikajenga shule ikaacha madirisha yako wazi na wanafunzi wanakaa kwenye udongo kwa kuwa madawati kwao ni hadithi. Na lawama nyingine nyingi tu.
  Lakini nikakumbuka kuwa huu ni Umasikini WETU ambao serikali inajitahidi kuunda Mipango YAKE ili iuondoe huu Umasikini wetu. Suala la Kujiuliza ni kuwa je Serikali hii ilituuliza ni mipango gani tunahitaji kuuondoa Umasikini wetu? Umaiskini wetu ni wa kwetu! tumezaliwa nao! Tumeulea..tukabweteka na kuacha kutafuta fursa zilizopo vijijini mwetu kuuondoa huu umasikini wetu...Serikali ikaja na Mikakati YAKE..Tena kuuondoa Umasikini WETU! Ndiyo maana ikajenga SOKO LA MAZAO wakati hatuna hata uwezo wa kuzalisha mazao ya kututosheleza chakula cha mwaka mzima..ya kuuza yatatoka wapi? Tena ikatujengea zahanati na kupiga marufuku wakunga wa jadi ambao hata sisi wakati tunazaliwa ndio waliotushughulikia...na zahanati yenyewe haina wataalamu na dawa hakuna! Serikali hiyo hiyo ikatujengea shule bila walimu wala madawati...mikakati Yao kuondoa umasikini wetu.
  Nikapata nafasi kukumbuka mwalimu mmoja aliwahi kutusimulia kuwa wazungu fulani walitembelea kijiji fulani wakakuta watu wanajisaidia porini.bila hata kuwauliza kwa kuwa waliona huo si ustaarabu wakaja wakajenga vyoo vya kisasa kabisa na wakaondoka,waliporudi wakakuta vyoo VYAO vimejaa mahindi wakawauliza kwa lugha yao..'Kwa nini hamjisaidii chooni na sasa mnatunzio humo mahindi'. Wanakiji wakajibu 'sisi tatizo letu hapa ni maghal ya kutunzia mazao yetu..soiyo choo" Hapo ndipo wazungu waligundua kosa lao wakaondoka kimya kimya!
  Nikakumbuka tena kuna wahindi walijenga choo cha kisasa pale Busurwa,kijijni nilipozaliwa ili kuwazuia wanakiji wasijisaidie kando kando ya ziwa victoria, wakaondoka ,kijiji kikaweka ada ya shilingi mia...hakuna hata mmoja aliyeingia, kila aliyeulizwa alisema,'siwezi kulipia chakula nilipie na kinyesi'. Kwa mso mi aliyesikia jibu hilo aliwakaripia wanakijiji na kuwaita majina ya mjinimjini..mara washamba,mara wapinga maendeleo n.k..lakini majibu YAO waliyatoa.
  Nikakumbuka tena miradi tunayoifanya kupitia shirika letu kushirikiana na Serikali. Tunatoa Dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi Bure kabisa..lakini baada ya miezi michache kama walianza kutumia mia basi sabini watakuwa wameacha au wamepotea.
  Unadhani kwa nini haya mambo hayafaniniwi? Mikakati YAO kupunguza matatizo YETU! Mipango yao kuondoa Umasikini WETU!


  Miradi au mikakati mingi,imekuwa ikishindwa kuleta mafanikio kutokana na Kuandaliwa na WAO ili kutatua Matatizo YETU pasipo kujua kuwa haya ni matatizo YETU!
  --------------------------------------------------------------------------------------------------------------
  Matatizo mengi tuliyonayo Tunaweza kuyatatua wenyewe..Wanakijiji Vijijini wanaweza kuwa na Maisha Bora hata kama Serikali haitaingilia..wakiamua! Wakitamani maisha Bora! wakifanya kazi kwa Bidii!
  Ninao Ushahidi:

  • Watu wengi waliofanikiwa ni wale tu waliokuwa na mawazo na Tamaa ya Mafanikio, 'aspirations' sijui kiingereza chake. Lakini watu kama akina Reginald Mengi au akina Erick Shigongo walikuwa Mafukara sana.Matamanio yao,Mawazo yao ya Mafanikio ndiyo msukumo wa Mafanikio yao.
  • Watu wenye uwezo mzuri vijijini ni Bidii zao Binafsi za kufanya Biashara au kilimo ndizo zinazo wapa mafanikio
  Kila mtu ana Nguvu ndani yake ambayo akiitumia vizuri atafanikiwa. Nguvu hii imejificha na ili kuigundua ni lazima uwe na fikra za matamanio 'mazuri' ya Mafanikio. THOUGHT is the greatest weapon in Connecting man to his Power inside him.

  'Strong personalities,who have a great belief in their own Power to ACHIEVE and SUCCEED draw unconsciously on hidden powers and thus are able to raise themselves higher above their fellows'


  Kimsingi FIKRA ndicho chanzo kikuu cha Mafanikio ya mtu.Fikra za Mafanikio,Fikra za kutamani maisha Bora ..ndicho chanzo cha kuweka bidii thabiti ili kuboresha Maisha ya Mtu.
  Tatizo kubwa ambalo serikali na wafadhili wanashindwa kuelewa ni kuwa KAMA MTU HANA FIKRA ZA MAENDELEO hata ukimwekea Mipango alfu ya Maendeleo hakuna Mafanikio, Kumbe basi kitu cha Msingi kuliko vyote ni kuwabadilisha watu Fikra. Ili waweze kutambua kuwa:

  • Wajue maana ya Maisha bora na watambue kuwa Wanastahili Maisha bora na wawe na Matamanio ya Maisha Bora
  • Watambue umuhimu wa kuwa na faya Bora ili kujiletea maendeleo
  'Maisha bora' yana maana tofauti kwa kila mtu.kwa babu yangu maisha bora ni kuongeza mke wa pili, kwa kijana wa kijijini maisha bora ni kununua baiskeli au piki piki na kwa kijana wa mjini maisha bora ni kununua gari na kujenga nyumba nzuri. Ni wajibu wetu kuielewesha jamii kutengeneza definition YAO ya maisha bora kulingana na resource zilizopo. Na wanajamiaa kujenga fikra hizo za maisha bora vichwani mwao na kuwa na matamanio ya kufikia hayo maisha bora.
  Serikali inao wajibu wa kujenga mazingira mazuri na Miundo mbinu endelevu ili kuwasaidia wanakijiji kufanya kazi kwa afyaimara ili kufikia ndoto zao.

  -----------------------------------------------------------------------------------------------------------
  NI WAJIBU WA NANI KUBADILI FIKRA ZA WANAKIJIJI?

  • Ni Wajibu wako wewe uliyezaliwa kijijini ukasoma na sasa umeng'ang'ania mjini badala ya kurudi huko kuwabadili fikra wanaKijiji wako
  • Ni wajibu wangu kama nilivyoanza kuutimiza kwa kuandika makala hii
  • Serikali ina nafasi yake hasa baada ya Wanakijiji kuwa na fikra za kufanikiwa
  Tuonane wakati mwingine


  Nimeiona hii nikaipenda si mbaya kushare
   
 2. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii Ni kweli sana tu
   
 3. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Nilikuwa naangalia Bunge leo ...Na Mheshimiwa Silinde ameongelea Mipango..Mipango mingi tu ambayo haijaonesha mafanikio! Mipango yao kuondoa Umasikini wetu..Mipango ya Kutekelezwa kwa miaka minne...lakini imeshindwa kutekelezeka kwa Miaka 50!
   
Loading...