Mipango ya Kufunga Kituo cha Televisheni Aljeezira ni Mikakati ya Marekani

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,081
2,000
Katika mgogoro uliotokea kati ya Qatar na nchi za Saudh Arabia na washirika wake serikali ya Marekani ilitaka Saudh Arabia kumaliza mgogoro na Qatar kwa haraka.
Katika moja ya masharti Saud Arabia iliyotoa ni kufungwa Kituo cha Televisheni cha Aljezzira. Kituo cha Televisheni cha Aljeezira (kiaarabu) kilianzishwa mwaka 1996 baada ya kituo cha BBC Arabic kufungwa kwa shindikizo kutoka kwa nchi ya Saudi Arabia baada ya kituo cha BBC Arabic kutangaza jinsi ukiukwaji wa binadamu unavyofanyika nchini humo. Mwaka 1998 wakati Marekani na Uingereza walifanya mashambulizi dhidi ya Iraq (Operation Desert Fox) Aljeezira TV ndicho kilikuwa kituo cha pekee kilichotangaza madhara ya mashambulizi ya Marekani na Uingereza ambapo raia wasiokuwa na hatia walipoteza maisha. Mwaka 2003 Aljeezira Tv walianzisha kituo kinachozungumza kiingereza kituo hiki kikawa ni kituo kikubwa na kilileta upinzani mkubwa kwa vituo vikubwa kama CNN, Fox News, NBC, BBC etc kwani kituo hiki kilitangaza habari zake bila upendeleo na kwa uhuru katika migogoro mingi duniani na haswa mashariki ya kati bila upendeleo.
Tarehe 1 April 2003 ofisi ya Aljezzira huko Baghadad Iraq ilishambuliwa na ndege za kivita za Marekani na mwandishi wa kituo hicho Tareq Ayoub aliuwawa katika shambulio hilo.
Kituo cha Aljezzira tv ni kituo kinachoangaliwa na idadi ya watu wengi mashariki ya kati, kituo hiki kimekuwa ni mwiba kwa sera ya marekani huko mashariki ya kati. Vitendo vyote vinavyokiuka haki ya binadamu popote duniani kituo hiki hutangaza bila upendeleo. Serikali ya Marekani Mara nyingi ilimuomba Mfalme wa Qatar alizuie shirika hili kutangaza vitendo vya majeshi ya Marekani yalivyokuwa yakifanya Iraq Na Afghastan lakini Mfalme huyo alikataa kuingilia masuala ya kituo hicho huru cha Aljezzira Tv.
Baada ya Saudh Arabia na washirika wake kutaka kituo hicho kifungwe hakuna nchi yeyote ya magharibi ikiongozwa na marekani iliyoshutumu suala hilo. Saudh Arabia haiwezi kutoa Tamko bila baraka ya Marekani. Mfalme wa Qatar ameruhusu majeshi ya Uturuki yaingie nchini humo kumsaidia kwani Marekani ina kituo kikubwa cha kijeshi nchini Qatar chenye idadi ya Askari 10000 kunauzekano wa Marekani na Saudh Arabia wana mpango wa regime change katika nchi hiyo ndogo tajiri ambayo inaushawishi mkubwa mashariki ya kati ambayo inaenda kinyume na Saud Arabia na washirika wake.
 

brian filbert

Member
Oct 27, 2015
68
400
Kwangu Al jazeera hana upinzani kwenye suala zima la habari, wanakupa ukweli kama ulivo, tofauti na nchi kama za uingereza (BBC) na marekani (CNN, FOX NEWS)wanaopenda kukunja ukweli kwenye baadhi ya mazingira kwa lengo la kuficha hadhira,. Al jazaeera doesn't SUGAR COAT, na huu umekua mwiba haswa kwa Western communities.
 

kiduni

JF-Expert Member
Jun 26, 2015
256
250
Kuna muda naweza sema sijui nawaza.ujinga ila naonakuna uwezekano siku moja dunia watasema imetosha kwa Marekani halafu akachapwa kama anavyowachapa wengine
 

Jics

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
236
500
sisi ni watazamaji tu kwenye hii movie kwa
hiyo wacha tuone mwisho wake utakuaje?
 

Ubavu

JF-Expert Member
Jun 19, 2012
2,793
2,000
Aisee kikifungwa hiki kituo sidhani kama ntafatilia international news tena.. Maana ndo sehemu nnapopata habari za dunia... Si cnn wala bbc wanaoweza kubalance habari zao zaidi ya
Al jazeera! Nitasikitika sana kama kikifungwa!
 

yahoo

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
3,452
2,000
Ukweli ni kwamba Katal walikuwa wanafadhili magaidi ,ushadi upo,na waliostukia ni waarabu wenzao kupitia email zilizovuja (between katal na is )
So waarabu wasiopenda ugaidi wameamua kupambana na ugaidi na wafadhili wao mnaanza kusema marekani inahusika...mtamsingizia marekani kila kitu
 

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,155
2,000
Aljazeera ni kituo pekee kinachotoa habari bila ya upendeleo.
Bila shaka huu ni mpango wa US wa kukimaliza hiki kituo.
 

Leonard Robert

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
10,114
2,000
Aljazeera nao wanafiki tu kama BBC mbona hawatuonyeshi mambo ya kikati kama ya kuchinja watu wanayofanywa na saud arabia
 

Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,714
2,000
Kilichobakia kuchapwa bakora tu hao Qatar so wamegoma masharti ikiwemo kuachana na Iran
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom