Kwa akili hizi za mpanuko wa miji ndio hutuletea shida. Huwezi kutumia masaa 4 kutoka Dar mpaka Dodoma na unataka kuunganisha Babati, Iringa Singida etc Uje uzuiwe masaa mawili kwenye kuunganishwa.
Miji yote mikubwa iliyopangiliwa inaangalia hili. Tutalitambua hili tumeshachelewa tuishie kubomoa majengo na kuharibu miundo mbinu. Ikiwezekana iwekwe provision ya city railways kuunganisha Uwanja wa ndege, Uwanja wa mpira, Stend za mabasi, mji wa serikali ili tuwe na mji wa mfano uliopangika na wenye usafiri wa uhakika.