Mipango hatari ya Mwigulu na Emmanuel Nchimbi dhidi ya CHADEMA,wahusika toeni ufafanuzi kuhusu hili

Status
Not open for further replies.
Kuna mawasiliano haya yaliyoletwa humu sasa hadi muda huu hakuna aliyetoa ufafanuzi kuhusu mipango hii hatari.Imeendelea kusambaa Facebook,Twitter na huku Jamii Forums kwa muda mrefu huku wahusika wakiwa kimya na badala yake Mwigulu Nchemba mwenye jina lilalofanana na jina la Naibu Katibu Mkuu wa CCM ambaye ni member huku amezingatia zaidi kulialia na maamuzi yaliyofanywa na kamati kuu CHADEMA dhidi ya Mhusika ambaye kwenye mawasiliano yanayoonekana hapa walipanga kumsaidia.

Pia mtu aliyetajwa kama Emmanuel Nchimbi (Jina linalofanana na Waziri wa Mambo ya Ndani) aliyeonekana akiwasiliana na huyo niliyemtaja hapo juu ameonekana akipanga kutumia vyombo vya dola kuhakikisha kumsaidia huyo aliyeadhibiwa na kamati kuu CHADEMA kwa tuhuma za uhaini .


Mara kadhaa vyombo vya dola vimetuhumiwa kutumika kisiasa na pia Mwigulu(Naibu Katibu Mkuu-CCM) amehusishwa kushirikiana na vyombo vya dola kuhujumu CHADEMA.Sasa inapotokea jina la mtu kama Waziri mwenye dhamana ya vyombo vya dola kutamba kutumia dola kisiasa kuhujumu chama cha upinzani kama inavyoonekana kwenye mawasiliano haya ni jambo la hatari linalohitaji ufafanuzi na lisilokubalika hata kidogo

Pia jina la mhusika anayetajwa kutoka CHADEMA alionyesha tabia zilizotia shaka katika sakata la kesi feki za ugaidi dhidi ya chama chake cha CHADEMA ikiwemo kuvujishwa barua za siri humu zilizokitaka chama kimtose mkurugenzi wake wa ulinzi na usalama huku akijua kuwa kama Mkurugenzi huyo angeshindwa kwenye kesi hiyo feki Chama kingehusishwa na hivyo mpango uliotangazwa na waziri mwandamizi kuwa CHADEMA kitakufa kabla ya 2015 ungetimia maana wangetaka kifutwe.Mawasiliano haya yanayoonekana hapa yanahitaji ufafanuzi maana kwa jinsi tume ya katiba ilivyohusishwa hapa ni hatari zaidi ikizingatiwa ni siku chache zilizopita tu Taifa limekumbwa na msiba katika mazingira ya kutatanisha ya kifo cha mjumbe wa tume hiyo Dr.Mvungi

Hivyo basi wahusika ni vyema wakajitokeza hadharani kuhusu hili kama nitakavyonukuu mawasiliano hayo jinsi yanavyosambaa kwenye media

Wahusika ni vyema wakatoa majibu ya hicho kilichoandikwa
 
suala la ukanda na udini halitombakiza cdm kijana yeyote anayejitambua_hilo ni doa kubwa sna, niliiliona tangu 2011 na kulisemea sana lakin hakuna aliyejali kipindi hicho lakini sasa imekuwa lalamiko la wengi na multiplier effect yake mtaiona tu_nitazungukuka nchi nzima at my cost kulaani hali hiyo_naamin kamwe batili haitoshindana na kweli

Sina uhakika kama kweli upo sawa kichwani. Unatumia gharama zako kuzunguka kusambaza taarifa ambazo azimu pekee ndie anayeweza kuziamini, endelea na zoezi lako labda kuna faida au nafasi ya kuwa mpiga deki wa Mwigulu.

Hivi lile suala la Udini na Ukanda(uzanzibari) wa CUF pamoja na zile Kontena za Visu kutoka nchi za kiarabu vya CUF liliishia wapi? Siku hizi CUF sio wadini na Wakanda tena baada ya kufunga nao ndoa kule Zenji?
 
Huwa mnapoguswa kidogo kule kwa kukalia, mnaanza kutoa vitisho na mapovu mengi. Jibuni hoja na sio kuleta vioja hapa. Muambieni Nchimbi na Nchemba waje kujibu na wasiwatume wake zao kuja kuwatetea hapa.
Nani kakwambia jina ni uthibitisho wa hizo email za kutengeneza. Hizi kweli ni akili za kuku.

Watanzania walio wengi hawana akili za kuku (brainless) kama hizi mnazozionyesha hapa.

Nchimbi na Nchemba yupi wakati dunia ina watu bilioni 7.127.

Umekosa hoja kwa sasa unaanza kuleta matusi kama ilivyo jadi yenu BAVICHA.
 
Hukakosea mkuu. Ndiyo huyo huyo aliyeshirikiana na Mwigulu kulipua bomu soweto

Mkuu mungi acha kuhadaa UMMA wa wanajamvi; bomu la soweto ulikuwa ni mkakati wa Chadema ili kutafuta huruma kwa wanaarusha. aliyepanga yote ni Lema; siri ilikuja kumbumburuka baada ya Lema kuwarusha fedha zao; ndio maana wakamfanyazia na kusambaza zile picha chafu.
 
Mpuuzi huyo,

Mimi watu kama hao huwa siwajibu,

Yeye anadhani eti sisi tutaacha kusema ukweli kwamba ndan ya chama hiko kuna ubaguz wa ukanda,udini na ukabila kisa yeye na wahafidhina wake watachukia??

Hakuna kitu kama hicho,dawa ya ukweli ni kuusema tuh,hata kama ni mchungu....


hapo kwenye bold mkuu ndiyo mwisho wako wa kufikiria , maana kila post lazima uandike hiyo bila kujali unajibu nini.Jaribu kushirikisha na ubongo wako kidogo uwezi hata kuandika na hoja nyingine zaidi ya hiyo tu, inachosha.
 
Asha mohamed,
Huyo THE BIG SHOW siyo mwenzenu, tena yupo kwenye kundi la wabakaji. Hana uchungu na maskini wazalendo wa nchi hii ndiyo maana yupo busy kutetea uhaini
Mkuu mimi naipenda dini yangu lakini sio kiasi cha kueneza chuki kama wanavyofanya wakina THE BIG SHOW wapo upande wa Zitto kwasababu ya dini tu basi kama angefukuzwa kitila mwenyewe wasingeweka neno hii ni tabia mbaya mno ambayo iliasisiwa na Mkuu wetu wa Nchi mwaka 2010 wakati wa Kampeni misikitini akisaidiana na Lipumba
 
Last edited by a moderator:
ndio maana nasema Ben amevurugwa na anafikiri kwa kutumia Ma------
Kwani kwenye siasa kuna kinachoshindikana? Nani hawezi kutengeneza email za Yahoo au GMail humu, mimi pia naweza kujiita Ben Saanane, nikatengeneza email ya bsaanane@yahoo.com, nikatengeneza nyingne kwa kujiita Mbowe, email ya ambowe@gmail.com kwa sababu haihitaji verification.

Sasa baada ya hapo natuma email kutoka Ambowe@gmail.com kwenda Bsaanane@yahoo.com kuagiza kwamba Ben Saanane uhakikishe ile sumu ya panya unaiweka kwenye chakula atakachokula Zitto, hapa utajiteteaje? Si kil mtu ataona kweli!

Kumbuka ni siku chache tu tumeona picha za Mbunge wa Arusha akimiminwa, lakini tuliambiwa kwamba picha ni fake tumekubali. Sasa hata hizo email sio za kweli, soma tu contents utaelewa kwamba information sensitive namna ile haiwezi kusafiri kwa njia ya email.
 
Nashangaa tunaishia kujibizana na kuanzisha mada mpya katika mada ya Misngi ambayo imeanzishwa na Ben ikiwa na lengo la kuwataka Nchimbi na Mwigulu wajibu hizo taarifa. Mnaojibu kwa niaba ya Nchimbi na Mwigulu tuwaelewe kuwa ni ndugu zake, wazazi wake, wake zao au hawala zao?
 
Mbowe anapaswa kuturidhisha juu ya
yaliyoandikwa kama madhaifu yke kwenye Mkakati wa mabadiliko 2013 ndan ya
taasisi...... atolee ufafanuzi hata kama
itamgharimu..

anapaswa atoe ufafanuzi wa dhaifu moja baada ya jingine ili kutudhihirishia umma kwamba waraka ule ni wa uchochezi na uhaini

Kinachotakiwa kushughulikiwa kwa sasa ni hizo barua pepe hapo. Kutozishughulikia baru pepe hizi hapa huo ndio uzembe. Zitajieleza na kizima ndani ya nyaraka zinazoitwa za siri, siri yake ipo hapa. Niliishakuwa shushushu, hapa pia ninanusa kiini cha mabomu ya Arusha.
 
Mkuu mungi acha kuhadaa UMMA wa wanajamvi; bomu la soweto ulikuwa ni mkakati wa Chadema ili kutafuta huruma kwa wanaarusha. aliyepanga yote ni Lema; siri ilikuja kumbumburuka baada ya Lema kuwarusha fedha zao; ndio maana wakamfanyazia na kusambaza zile picha chafu.

Malengo yenu ilikuwa ni kumwua Mwenyekiti wetu na Lema kwakuwa wamekuwa tishio kwa utawala wa ccm, ili kurahisisha kipenzi chenu Zitto awe mwenyekiti wa chadema mtawale kwa amani.
Watanzania wataendelea kuwahukumu kwa tabia zenu za kigaidi
 
Hukakosea mkuu. Ndiyo huyo huyo aliyeshirikiana na Mwigulu kulipua bomu soweto

Huyu jamaa ni mtu hatari sana , hata maafisa Polisi wenzake wanamuogopa sana.Inawezekana na hili la Jamaa wa Tume ya Katiba akawa ana mkono wake nini?
 
Mkuu mimi naipenda dini yangu lakini sio kiasi cha kueneza chuki kama wanavyofanya wakina THE BIG SHOW wapo upande wa Zitto kwasababu ya dini tu basi kama angefukuzwa kitila mwenyewe wasingeweka neno hii ni tabia mbaya mno ambayo iliasisiwa na Mkuu wetu wa Nchi mwaka 2010 wakati wa Kampeni misikitini akisaidiana na Lipumba
Kweli wewe unaipenda dini yako hongera sana.

CC: Matola THE BIG SHOW
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom