ub16
JF-Expert Member
- Feb 19, 2013
- 420
- 316
Nilitaka kuleta rant yangu kidogo na hili jukwaa ndo the closest related I can find, moderators mnaweza kuhamisha mada kama hapa si mahala pake
Siku mbili zilizopita nilienda airtel kudai namba yangu ya simu, flashback kidogo hii si mara ya kwanza, mara ya kwanza ilikuwa mwezi wa saba na wakadai kuwa sikutumia SIM yangu kwa siku tisini(90) kitu ambacho si cha kweli, bahati mbaya sikuwa na ushahidi sababu nilikuwa nikiformat simu mara kwa mara, hivyo basi nikapoteza namba yangu ambayo nimetumia kwa miaka sita(6) na wakampatia mtu mwingine a.k.a Recycle, ikanibidi nisajili namba mpya.
Back to the present, wakati huu nikawa nina ushahidi wa kutosha kukiwa na messages na call log zikionyesha mara ya mwisho namba yangu mpya kutumika ni November 29 2013 lakini bado wanadai system yao inaonyesha sijatumia namba yangu kwa zaidi ya siku tisini(90) na kuwa haiexist, hivyo wameifunga na hawawezi kunipatia, ila wataifungua na kumpatia mtu mwingine baada ya wiki/miezi kadhaa a.k.a Recycle
Kwa mnaofahamu zaidi telecom mtanirekebisha ila kwa mtazamo wangu mfumo wa kurecycle namba za simu ni upuuzi na usumbufu uliopitiliza hususani kama namba zimeunganishwa na shughuli za kibenki.
Tatizo(Possible):
Solutions:
Conclusion:
Kutokana na usumbufu niliopata nadhani ndoa yangu na airtel imefikia kikomo, nimesumbuana nao mpaka nimechoka

- System yao ya kuweka kumbukumbu haifanyi kazi ipasavyo
- Vigezo vya simu kuwa in use haviko sawa
Solutions:
- Fix your stupid buggy sytem
- Mtaarifu mteja siku kadhaa kabla ya namba kufungwa, tena mara kadhaa
- Kama mteja ana ushahidi wa kuonyesha namba ilitumika arudishiwe namba
- Kama wanafunga namba wataarifu huduma zote ambazo namba husika imeunganishwa i.e benki, ving'amuzi, dawasco etc