Mimi tarehe 25 ni CCM

Mimi tarehe 25 ni CCM

He,yani ninyi wooooote ni Magufuli, basi ata mimi pia ni Magufuli.
Hapa kazi tu buana.
 
Maandishi mengi hayo yanaonyesha hutumii akili yako vizuri kupambanua mambo vizuri sasa sijui hata kura zako utazidisha pia.Mtoa mada hata mimi kura yangu ni kwa DR. POMBE MAGUFULI, hapa kazi tu.

Kazi ya kumshobokea shemeji yako ndio unasema hapo kazi tu? 🙁 boya wewe
 
Yaan hiyo siku nikiingia pale kwenye kisanduku sifanyi makosa kabisaa
 
Hahahaaaaa naona kitengo cha IT masaki kinatekenyana hapa.
 
Kura yangu ni kwa Mgufuli.
Na mimi mjasirimali nimeteswa sana na shida ya umeme. Mtaji wangu umezama mara tatu shauri ya umeme na kwa sababu umeme unapatikana bila shida sasa mimi kura yangu ni kwa CCM tu...Hapa ni kazi tu. Pia Lowassa ndiye aliyepata fedha zote za Escrow,EPA,nk. Pia amesababisha upotevu wa mabilioni pale wizara ya Miundombinu. Amesababisha rushwa katika jeshi la polisi na kufanya hospitali zetu kukosa dawa. Mahakama hazitoi haki kwa Sababu ya Lowassa.

Lowassa ndiye mwenye IPTL, na Dowans inayoitwa Symbion sasa. Lowasaa aliua viwanda vyote alivyoanzisha Mwl Nyerere na kuweka viwanda vyake na akawa bilionea. Mfano alibinafsisha kiwanda cha Tanganyika Packers na sasa kimekuwa chake kinatengeneza nyama ya kwenye makopo(corned beef). Na hata sasa ukienda supermarket utakuta zimeandika TANGANYIKA PACKERS Corned beef(ukiangalia lile kopo vizuri utaona kwa mbali kuna picha ya Lowassa. Lowassa amefanya elimu ya Tanzania kuwa dhaifu na kutoa watoto wasioweza kusoma na kuandika baada ya kumaliza ELIMU ya msingi. Lowassa anafanya watoto wa chuo kikuu kukosa mkopo na hata watoto wa maskini wanapata mkopo asilimia 30 lakini wale wa matajiri na wanaojiweza wanapata 100%.LOWASSA HAFAI HATA KIDOGO.

Mimi naenda kuvaa T-Shirt imeandikwa #hapa kazi tuu# wakati sijafanya kazi tangu asubuhi,kwa sababu kiwanda changu cha kutengeneza samani hakifanyi kazi shauri ya kukosa umeme. Lowassa hafai. Natumaini nimeeleweka
 
Yaani tuombeane uzima kura yangu unayo Magufuli Mungu mwenye enzi azidi kukupa kibali na afya njema akutangulie.
 
Back
Top Bottom