"Mimi sio mtoto, nina miaka 20"

Papa Mobimba

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
1,153
1,359
⁣Hakika dunia hii ina maajabu ya kila aina. Kuna magonjwa na maradhi ya kushangaza na kuogopesha. ⁣

Moja wapo ya magonjwa hayo ni maradhi ya Hallermann-Streiff (Hallermann-Streiff Syndrome). Ugonjwa huu una athiri watu wachache sana. Na uanambatana na magonjwa mengine zaidi ya 20 ikiwemo matatizo ya moyo, nywele kutoota sawa, kuwa na mifupa dhaifu na wengine huzaliwa wakiwa hawana ubongo. ⁣

Ukimuona mgonjwa wake unaweza kufikiri ni mtoto kumbe ni mtu mzima. Mojawapo ya watu wenye maradhi hayo ni Michelle Elizabeth Kish. Akihojiwa na BBC Michelle alisema, " watu wengi wakiniona wanadhani mimi ni mtoto, mimi sio mtoto, nina miaka 20"⁣

Kwa sasa inaaminika kuna watu wasiozidi mia mbili wenye ugonjwa huo. ⁣Ugonjwa huo ni ugonjwa wa kijenitiki (genetic disorder)
Screenshot_20190214-124325_Gallery.jpg


Pichani ni Michelle akiwa na dada yake Sarah
 
magonjwa ya wazungu haya, huku kwetu ukizaliwa na hizo genetic defects basi hata wiki humalizi unakufa, mwisho wa siku hauji kumwona mtu mwenye hayo magonjwa.
 
Back
Top Bottom