Mimi sio mchoyo wa mawazo njoo uchukue na hili

Wabongo hatuna utamaduni wa kununua packaged food,ungesema labda upack halafu uexport kwenda mfano kenya sawa,ila kwa hapa utauza labda mifuko 50 ya kilo mbili,na bidhaa itakudodea tu,watu wanataka mchele waushike kwa mikono kujiridhisha kuwa haujavunjika na hautoki pakstani,
haakubali kununua mbuzi ndani ya gunia,
kuna mtu alipack hivyo huko kusini,lakini naona haijamlipa yuko kimyaaaa
Nazani sikwamba hatuna utamaduni wakununua vyakula vilivyo kuwa packed ilaa ni kwamba the level of social development ndani ya nchi ni ndogo sana laiti kama tutaweza kujikwamua kutoka kweny level ya uchumi tuliopo kama mpango wa serikali ulivyoo basi jua tutakuwa pia na social development/welfare ambo ndipo utapoona watu wanaprefer safety and healthier product kama izoo ni sawa leo watu wengi wanalalamika kuhusu kilimo cha maind kutokuwa na faida yote io nazani ni kwasababu ya unga packed watu wengi leo ii wanatumia unga kama uo soo musishangae itakapo kuja time mchele pia utakuwa ivyo ivyo kwa mfano unaambia in the continent ambapo once lilikuwa halitamaniki which is Africa ofcoz, out of every three people ina Africa one is in middle class pia for top ten countries zinazo kuwa kwa kasi kiuchumi duniani 4 to 6 of them there in Africa (opportunity just knocking out of your door)
 
changamoto ili kuboresha wazo Hili:

1. Watanzania hatuna utamaduni wa kununua packed foods km Mchele. Kwa mentality tu, wengi wanahisi KUPIGWA! mf Kilombero Sugar wanapack sukati 1 kg lkn Bado watu wanaamini ya kupima kwa mzani!

2. Ukiupack huo Mchele usijpeleke dukani. Utadoda! Kama kusambaza labda uwasambazie watu maofisini. Angalia changamoto ya usafiri hapa!

3. Maisha ya kukariri. Ukmpelekea mama Mchele Ofisini kwake kwa 2500 pkg atawanong'oneza wenzake "HUU MCHELE KWA MANGI ANAUZA 2100!

4. Kuna cha ziada lazima ukijue, wamama wa kitanzania wengi Wao kuchambua Mchele sio tatizo na kwa hiyo hawaoni sababu ya kununua packed rice. Kwao kuchagua Mchele ni sehemu ya socialization!

5. Kwa business kama hii, lazima ujipange kwa mtaji mkubwa ili market Penetration yako iwe kuwakopesha huko maofisini then baadae ndio unaenda cash ba cash

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bo
changamoto ili kuboresha wazo Hili:

1. Watanzania hatuna utamaduni wa kununua packed foods km Mchele. Kwa mentality tu, wengi wanahisi KUPIGWA! mf Kilombero Sugar wanapack sukati 1 kg lkn Bado watu wanaamini ya kupima kwa mzani!

2. Ukiupack huo Mchele usijpeleke dukani. Utadoda! Kama kusambaza labda uwasambazie watu maofisini. Angalia changamoto ya usafiri hapa!

3. Maisha ya kukariri. Ukmpelekea mama Mchele Ofisini kwake kwa 2500 pkg atawanong'oneza wenzake "HUU MCHELE KWA MANGI ANAUZA 2100!

4. Kuna cha ziada lazima ukijue, wamama wa kitanzania wengi Wao kuchambua Mchele sio tatizo na kwa hiyo hawaoni sababu ya kununua packed rice. Kwao kuchagua Mchele ni sehemu ya socialization!

5. Kwa business kama hii, lazima ujipange kwa mtaji mkubwa ili market Penetration yako iwe kuwakopesha huko maofisini then baadae ndio unaenda cash ba cash

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora useme ww ...!bora umeandika!hata maharage tu packed huwa hayatoki..tumezoea kuyang'ata kwanza kama malaini😅😅
 
bo

Bora useme ww ...!bora umeandika!hata maharage tu packed huwa hayatoki..tumezoea kuyang'ata kwanza kama malaini
Itatuchukua muda sana kubadilika. Mi nina duka na najionea. Hili nililicopy pale SOKO LA KISUTU. nlikuwa nanunua gunia 2 za Mchele afu nawapa wadada wanaupembua! Mwenyewe nasema naongeza thamnani. Ulinidodea. Nikashusha bei!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itatuchukua muda sana kubadilika. Mi nina duka na najionea. Hili nililicopy pale SOKO LA KISUTU. nlikuwa nanunua gunia 2 za Mchele afu nawapa wadada wanaupembua! Mwenyewe nasema naongeza thamnani. Ulinidodea. Nikashusha bei!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nazani kuna maana unavooambia any business inatakiwa kuwa na niche yake sas unavoleta kitu unatakiwa ujue kwamba watu utakao wauzia ni watu wa aina gani wanapendelea nini na vitu vingine kwa apo naweza sema inajikita sana level ya income na education typically apoa target yako muimu kuwa ni watu wa upper class,upper middle class pia na middle class unaweza kuwatarget working class pia na lower class ila uandae mikakati itakayo weza kumeet their need kma kulower/kupunguza cost ya production as much as possible ilii uuze price ndogo kuweza kwa watu kweny class izoo mbili kuafford inaonekan kama ni kitu impossible but back to enzi za henry ford utatambua kuwa ndio alie make it possible kwa mtu wa kawaida/middle class kuwa na gari leo mtu kuwa na gari n kitu cha kwaida lakn back then it was something impossible even to imagine thats wat we call entrepreneurship sio uajasiliamali wa watanzania walio wengi
 
Soko lipo sana tu, hao wanaokatisha tamaa watakuwa wauza maduka ya rejareja, siku hizi watu wameelimika wanahitaji kununua vitu visafi na tayari kwa kupikwa hata unga Wa uji wananunua packed sembuse mchele! Kikubwa hapo ni kuweka bei ndogo isizidi sana ya DUKANI, weka na sifa ya mchele baada ya kupack kwamba ni tayari kwa kuoshwa na kupikwa yaani hauna chuya wala mchanga, hata usiku unaweza kupika bila kuchambua, siku hizi wote tunapika yaani wanaume na wanawake sasa mwaume mchele Wa kuchambua ataweza wapi? Mahotelini, mashuleni, supermarket, wanaouza unga Wa lishe we pack kauze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biashara yako hii itakulipa endapo utafanya kwa kutumia machine kufanya kazi hizi zote ukitumia man power itakula kwako mana kuchambua tu unatakiwa wafanyakazi wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ni mama wa nyumba sawa
lakini watu kama nyinyi wapo wengi wakisikia wazo cha kwanza wanachowaza kutoa changamoto tu za wazo lako
Kwani mtu akikwambia maono ya changamoto kwenye jambo unalotaka kwenda kufanya tafasiri yake ni kuwa hakutakii mema yaani anakuonea gere?!

Hapana bwana, hiyo ni nidhamu ya uoga uliyonayo wewe. Me nilitegemea mtu anapokutahadharisha basi unatakiwa umsikilize kisha ufanyie kazi na utafiti kile alichokwambia badala yake unaanza kumshambulia tena kuwa anakuchuria au anakutakia ubaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupepeta mchele ni sehemu ya tamaduni za kiswahili. Utajuaje kuwa wamepika ubwabwa asipokaa kibarazani kupepeta na kutoa chuya.

Kwa kifupi hii ndio kitu inaitwa 'customer's perception' kuielekea bidhaa au huduma.

Ni sawa sawa na huduma ya counseling namna inakuwa ngumu kueleweka kwa watanzania sababu wanaona misukosuko ya kisaikojia huwa si tatizo ni mambo ya kuvumilia na kupotezea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaah watu bana!! Yaan jamaa hataki kupewa changamoto ata kidogo anataka tu[ige makofi kama tupo mtaani kwetu Lumumbah.. Ukiona mtu anayeona changamoto kwenye wazo lako inabidi utulie na ujibu vizuri sababu kama wewe umefikia hatua ya kulileta hapa ni kwamba umeshajiuliza haya yote na majibu uko nayo. kwahyo unatakiwa kuteleza tu kama unasoma Mathew 7.7
Mtu ambaye hana uhakika na anachokwenda kufanya utamjua kwa reactions zake. Yaani hataki kusikia mtu anakuwa against naye kwa lolote anataka kuungwa mkono tu asipingwe hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom