EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,708
- 35,719
Yule mgonjwa akamjibu, "Bwana mimi sina
mtu wa kunitia birikani maji yanapotibuliwa, kila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu” Yohana 5:7.
Hiki ni kilio cha watu wengi, yule mgonjwa kutokana na udhaifu wake hakuweza kuingia mwenyewe ili aponywe maana alihitaji mtu wa kumbeba na hakuwa nae.
Katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa na maneno haya sina referee wakuniwezesha kupata kitu au postion fulani, utakuta mtu kahuzunikaaa! Kisa katika ukoo wao hana mtu wa kumsaidia kupata kazi au kupata mtaji, yeye ndio mwenye unafuu wa maisha ukoo mzima,
kila wakati maneno yake ni haya "SINA WAKUNISAIDIA.
Asubuhi ya leo nikutie moyo.
Yupo YESU referee mkubwa, NDUGU na RAFIKI wa kila mtu.
Huwa anatokeza msaada pasipo na njia na ana uwezo wa kukuinulia watu ambao hukuwatarajia, anaweza kukupa dili au kazi ambayo hukuwahi kuwaza na pengine hata hukuisomea
Vumilia ni kipindi tu kinapita hata yule mgonjwa alipona pamoja na kwamba alikaa sana mahali pale Endelea kumtegemea Yesu.
Ubarikiwe na Kristo Yesu.
#Mwinjilisti na Mwalimu Emanuel
C&P