Mimi nitakuwa tofauti na hao..manispaa ya ILALA labda ni sera ya CCM!!

Mimi nitakuwa tofauti na hao..manispaa ya ILALA labda ni sera ya CCM!!

KakaKiiza

Platinum Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,948
Reaction score
9,465
Mimi ninalitambua kuwa kila mji,jiji duniani kunatakiwa kuwa katika mandhari nzuri lakini wanakuwa wameshatoa vipa umbele na kinachobki nikutengeneza mji/jiji!!

Nia yangu nikutaka kujua hii manispaa ya Ilala kwakutumia Mamilioni ya pesa kwa kujenga vipita shoto kwa gharama ya kutisha!!zaidi ya milioni 300ml zitatumika kujenga mandhari ya vipita shoto!!
Kweli mimi ninauliza hakuna vipa umbele vingine kwenye hii manispaa ya ILALA??
Wakati kuna shule hazina vyoo??
hazina maji??Hazina madawati??
Wakati hospitali zake nyingi hazina Dawa??
hakuna vitanda vyandarua??!!
Mimi ninaona huu ni mradi wawatu wakumaliza pesa za serikali!!
Je wewe unaona vipaumbele kwenye hii Manspaa ni kuweka Mamba za vyuma na ngarawa za mabati?? kwa gharama ya mamilioni???
Kweli kweli mimi naumia kwa kodi zetu kuliwa na mtu mmoja wakati watoto wetu wanakaa chini!!:A S thumbs_down::nono:
 
Hii ndiyo serikali ya hawa jamaa ukiuliza bei ya vile vibati hutaamini mamilioni yaliyotumika.
 
KakaKiiza hawana vipaumbele na wala hawajui ni nini lengo lao la kuwa pale
Zaidi wanatafuta sehem ya kula maana wakienda kununua hayo madawa au madawati hawapati kula kirahisi
Je huo mpango ulipitishwa na nani na una manufaa gani kwa wananchi wa kawaida wakati barabara kibao ziko ovyo na huduma za kijamii ndo kabisa hazifai
 
Last edited by a moderator:
Uongoazi dhaifu = Vipaumbele dhaifu
 
KakaKiiza hawana vipaumbele na wala hawajui ni nini lengo lao la kuwa pale
Zaidi wanatafuta sehem ya kula maana wakienda kununua hayo madawa au madawati hawapati kula kirahisi
Je huo mpango ulipitishwa na nani na una manufaa gani kwa wananchi wa kawaida wakati barabara kibao ziko ovyo na huduma za kijamii ndo kabisa hazifai
Mimi nilipoambiwa pesa itakayotumika na ambayo imetumika kutengeneza hizo pitashoto nimeshangaa sana!!
 
Tatizo la msingi liko kwenye mfumo. Tumefikia mahali kuamini kuwa mambo ya maendeleo yatafanywa na wafadhili pamoja na wawekezaji. Yaani masuala ya kuboresha/kujenga vyoo, madarasa, kununua vitabu vya mashuleni n.k yatafanywa na wafadhili ama wawekezaji kama tunavyoona mara kwa mara kwenye vyombo vya habari. e.g Shirika/ makpuni flani imetoa vitabu, madawati, kujenga vyoo, kuchimba visima n.k

Kwa maana hiyo wajibu wetu wa maendeleo tumeubinafsha nasi tumebaki na wajibu wa kupamba maeneo yetu ili hayo wafadhili/wawekezaji wafurahi mitaa yetu.
 
Hii MANISPAA kwanza hawana dira kabisa. Cha ajabu mnakumbuka kuna alama za barabarani zilizowekwa katikati ya jiji karibia mwaka na nusu sasa, hizo alama mpaka zimeanza kuondolewa taratibu. Kwa madereva wageni wanao ingia jijini watapa shida kuendesha magari yao katikati ya jiji, na hii inadhihirisha uwajibikaji mbovu wa viongozi wetu. Je nina wa kuwachukulia hatua viongozi wanao buni miradi hisiyo tekelezeka? Kama huu wa alama za barabarani? Ukifatilia kuna barabara nyingi hazina alama za wazi, madereva wakipata wanakamatwa na polisi, je nani mwenye makosa? Na pia mnakumbuka misanamu ya matwigwa ilisimikwasikwa kila bustani na kwenye mizunguko ya barabara (round about) siku za nyuma kidogo haikuchukua muda ikaondolewa, je nao ulikuwa mradi wa nani? Je nani wakuwachukulia hatua viongozi wa manispaa kwa matumizi mbaya ya kodi za walala hoi? Kuna mambo mengi ukiyafatilia ktk manispaa zetu utapatwa na kichefuchefu. Mimi nina wasiwasi na viongozi wetu, hawana uwezo wa kubuni mradi yenye manufaa kwa taifa, wanaangalia watapa nini ktk mrida hii mibovu. Mungu Ibariki Tz.
 
Mimi nilipoambiwa pesa itakayotumika na ambayo imetumika kutengeneza hizo pitashoto nimeshangaa sana!!

Usishangae hivyo ndivyo viongozi wanaofadhiliwa na chama cha magamba wanavyopata hela za kukifadhili chama chao na wao wenyewe wakati wa uchaguzi; ndio maana meya wa ilala alikamatwa na TAKUKURU huko Iringa akiwa na mapesa chungu nzima aliyokuwa anawahonga wapiga kura kwenye uchaguzi wa Umoja wa vijana wa magamba!! Hutuibia fedha zetu kwa kupitia miradi yao ya pwagu na pwaguzi!!!
 
Back
Top Bottom