Mimi nimethubutu na nimeweza wewe jee???

Mimi nimethubutu na nimeweza wewe jee???

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,720
Mwaka huu ulipokuwa unaaza nilimwomba Mungu anipe moyo wa kutenda matendo ya huruma na upendo na nianze na wale wa karibu yangu.

Ukweli kile nilichokiomba ndicho nilichopewa kwa mwaka huu.Nimefanikiwa zaid kutenda matendo ya huruma hata kwa watu wasiokuwa ndugu zangu wa karibu hapa sifa nampa yeye Mungu mwenyewe. katika mambo mengi ya upendo na huruma niliyotenda napenda kuwashuhudia jambo moja ambalo limenikuna zaid.

Kama mjuavyo familia hazina watu wenye uelewa mmoja na pia hazikosi mtu ama watu wenye tabiza zisizovumilika. Kwenye familia yetu tulikuwa na kaka (binamu) huyu ni mtu mzima 36 by age amekuwa ni mhanga wa madawa ya kulevya kwa muda wa miaka 15. alianza kwa kunywa pombe since akiwa sekondari, aka-advance kwenye marijuana na sasa akaingia kwenye heroin. Kwa miaka 7 ambayo amekuwa akitumia heroin + marijuana iliyomfanya awe kama mgonjwa wa kansa hivi, alifika hatua hawez kula kabisa anashinda kwa kula biscuit na jojo, ukimlazimisha kula basi portion yake ni ndogo kuliko mtoto wa mwaka anavyoweza kula.

kwa kuwa na tabia hii hakupenda kukanyika wala kuskia ushauri wa mtu yeyote yule, tulimwogopa kama ukoma, alifikia mahali akaanza kuiba, alijiibia yeye mwenyewe hadi akajifilisi akageukia kwa ndugu yani ukimkaribisha ndani mwako ujue atakuliza alipoona ndugu wana mkwepa akageukia kitaa akawa anaibia watu pochi na hadi kupanga dili zakuiba kwenye nyumba za watu yaani mchora ramani za wizi. kwasababu ya kukosa nguvu nayo hii ikamshinda akageukia kuokota makopo na kuuza na hela zote hizi akipata yeye anampelekea mzungu tuu ili apate kete zake ambazo kwa maeneo anayokaa alikuwa ananunua kwa sh 1500-2000 kwa kete moja. Uvutaji wake ulikuwa ule wa kuvuta kama sigara na sio ule wa kuchoma kwenye kigae ama kujidunga.

mwezi uliopita nilikutana nae akiwa kama chizi, niliogopa sana na nikasema kwakua ni ndugu yangu wa damu lazima nifanye jambo kwaajili yake. Nilimface bila kushirikisha ndugu wengine nikaongea nae juu ya kutaka kumsaidia apate tiba, alikuwa mkali sana sikukata tamaa nikaenda kwa mshauri nasaha nikamwomba aongee nae ili atibiwe apone. Baada ya kubembelezana sana alikubali kutibiwa.

Wapendwa wangu nilianza taratibu za kumtibia hapa Muhimbili,wiki iliyopita siku ya j4 lakin kutokana na kukosa huduma ya kumlaza nikamhamishia kwenye hospitali moja maeneo ya makumbusho. Nilipata changamoto sana manake siku moja tu alokaa pasi kupata madawa yake aliugua kama vile anakufa, aliharisha kama mgonjwa wa kipindupindu vile non stop, akapata homa kali kama vile mgonjwa wa UTI yaani nikaanza kuogopa tena kwamba huenda ukishaanza kuyatumia hutakiwi kuacha. Dr alinishauri nisiogope atapona tuu kwani hii ni zile sumu za yale madawa zinatoka. alipatiwa matiibabu kwa muda wa siku kumi tu na nikaona tofauti ya ajabu kabisa kwake. Yaani binamu yangu huyu amepona ingawa bado kakonda lakini haumwi popote pale na ameoga na kunyoa nywele na ndevu anaonekana ni mtu.Ninamshukuru Mungu sana kwamba amemponya na sasa ni mzima kabisa. Ninayofuraha sana kuona nimethubutu kumtibia na sasa nimeweza kwani amepona kabisa.

Na wewe mwana jf mwenzangu hebu angalia kwenye familia yako kama yuko ndugu ama mtoto mwenye tatizo hili thubutu kumsaidia naamini kama tukifanaikiwa kupunguza idadi ya watumiaji basi ni wazi kwamba hata hao waagizaji nao watakosa pa kuuzia.

^^
Heri yako umefanya jambo la kheri,,
Mimi nadhani sina nililofanya
^^
 
Hongera sana kwa kitu ulichofanya, umetuonesha njia kwamba ukithubutu unaweza mi nilikua naamini hawa jamaa kupona ni bahati nasibu na lazima na mimi nilipe hisani yako japo hazitofana
 
Hongera sana kwa kitu ulichofanya, umetuonesha njia kwamba ukithubutu unaweza mi nilikua naamini hawa jamaa kupona ni bahati nasibu na lazima na mimi nilipe hisani yako japo hazitofana

hata mimi niliamini hivyo na tena nilikuwa najua mtu akishadumbukia humu ndo kabisaa huwez kumrudisha badala yake utegemee afe tu kwa madawa. lakin ni uongo wana tibika na kupona kabisa. sasa hivi kijana yuko mzima tnajitahd na msosi ili japo kamwili karudi rudi
 
Nilienda pale mhimbili kwa shughuli binafsi siku moja, nikatembea maeneo ya wagonjwa/waathirika wa dawa za kulevya, kidogo nitoe chozi. Ndipo nilipogundua kuwa TZ ina tatizo kubwa la dawa za kulevya.

Hongera sana kwa kurudisha uhai, ni wakati kila mmoja anatakiwa kufanya kitu chanya katika jamii.
 
halafu watu hawajui tu ila ulevi wa haya madawa ni wa kitajiri sana manake unauzwa aghali kuliko hata bia yenyewe lkn madhara yake ni makubwa kuliko yaletwayo na bia.

ukiwaona wale vijana walivyochoka ngozi zilivyopata mafungus, midomo imeungua na afya ni dhaifu utalia machozi. Halafu mahali wanapolazwa ni duni sana hapana stara wala heshima ya kumlaza mtu. na wahudumu wao baadhi wanamaneno machafu utafikiri mwathirika kajitakia ama yy amepona kwenye kizazi chake hatakuwepo wa aina hii. kunahitajika mabadiliko makubwa sana kwenye hili.

Pale Makumbusho ni pazuri sana ukitaka kumtibia mwathirika.
 
umefanya jambo jema na la heri sana. Hongera. Mi nadhani tusijikite kukata matawi, ni vyema kukimbilia kuingoa mizizi. Kuna kundi jipya kila leo linajiingza kwenye uvutaji tukiweza kuwaelimisha hawa wasiingie hata hayo mazungu ya unga hayatakuwa na pa kupeleka.
 
uelimishaji kwa ambao hawajaanza ni jambo la muhimu sana ili kuzuia wasiingie, lkn pia kunusuru wale ambao tayari walishaingia ni jambo la muhimu zaid.

ninaamini kelele za kuwazuia waingizaji hazitasaidia kama hatutajaribu kuua soko lao, manake kama wakikosa wateja ni wazi kwamba wataacha kuuza.
 
Hongera sana mamii.

Sasa hapo ndio kazi inaanza. Anahitaji support ya kila mtu kusudi asirudi nyuma na kuanza tena kutumia madawa. Anahitaji kazi ili awe busy na asiwe na stress sana ya hela. Kuna support groups ambazo zitamsaidia. Naweza kukupa contacts za ofisi ambayo iko upanga na inashughulika na hizi sober houses. Akikutana na waliokaa sober miaka mingi itamsaidia.
 
Hongera sana swetlo kwa kumrudisha kijana kundini. Napata hasira kujua wanaofanya hivi hawafanywi lolote la maana
 
naomba hizo contacts manake jana ndio ameruhusiwa ila imebidi niseme asiende kwao aje kwangu kwa muda manake nahofia asije akarudi nyuma. sasa ukinipa a way forward itakuwa ni msaada sana. kuhusu kazi sijui kama ataweza kufanya kwasasa manake he is so weak, bado na yuko ndani ya dozi za fungus. sijui kwann napata hofu ya kuruhusu kufanya kazi kwa sasa. naona kama atanyayapaliwa vile. kuna baadhi ya ndugu nao hawajaamini kwamba kabadilika na hawa ndio wanaoniumiza zaidi manake wanaweka kuta kila ninapotaka kupita.
 
Hongera sana swetlo kwa kumrudisha kijana kundini. Napata hasira kujua wanaofanya hivi hawafanywi lolote la maana

swtlo......ukitaka kupata hasira nenda muhimbili kwenye kituo cha waathirika wa dawa za kulevya ama mwananyamala utalia na utataman ukimsikia Kinje ukamkanyage na gari afe. kuna vijana na sasa ni wote wa kike kwa wa kiume yaani maisha yao utalia machozi. wadada wazuri lkn ndo hivyo tena washakua mateja inahuzunisha sana. Tuombee sana watoto wetu kwa kweli
 
Back
Top Bottom