i411
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 906
- 297
Daa huyu mama na watoto wake mpaka nimeshindwa kulala lakini hii ni hali halisi katika vijiji vingi. Nguo nimpaka ccm waje kutoa za kampeni ndo watu wanapata kanga mpya na tishati na kofia. Kwaza huyo mama anaonekana bado msichana mdogo sasa anawatoto watatu. Mungu mkubwa jamani bado yupo gado na labda mwingine mwingine anakuja. Huu ni ukatili aina fulani jamani tufanyeni tuu bidii kila tuwezavyo miaka ijayo matatizo kama haya yapungue hili sio tatizo la ccm tuu jamani hawa ni wenzetu. Kwawale wanojiweza vizuri mwaweza angalau kuchimba visima kule vijijini mlipotoka kidogokidogo tukiwa na moyo wa kujitolea tutafika tuu. Mkienda kwenye kikao cha kuchangia harusi huko huko mnaweka na kamchango cha kusaidia kakijiji fulani twaweza kujikomboa.