Mimi ni mwanaume mwenye bahati

Mimi ni mwanaume mwenye bahati

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,101
Kwanza kabisa wanawake omba omba sijawahi kabisa kuwa kwenye mahusiano nao,unajua kwanini huwa sitongozi kila mwanamke anayepita mbele yangu! Kwanza kabisa najijua mimi ni mwanaume wa aina gani na natakiwa kuwa na mahusiano na wanawake wa aina gani!

Ushawahi kusikia mtu anayekaa masaki anasema kodi ya nyumba ni kubwa?,lakini akitoka mtu anaishi mbagala kwenda kuulizia nyumba masaki atashangaa sana kuhusu bei atasema bei ni kubwa sana na hailipiki!,mwanaume tujifunze kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanawake wa hadhi zetu na tutaacha kulalamika hovyo, wapo wanawake wazuri cheap na pia wapo wanawake wazuri expensive, maisha ni mfumo ule ule mbona ikifika mchana unataka kula chakula hauendi kula hotel ya nyota 5 na badala yake unaenda kwa mama ntilie kula chakula cha buku jero?

Ni kwa sababu unajijua kipato chako! Hauwezi kwenda kwa kutegemea utapata chakula cha buku jero!,lakini wapo pia wanaenda kupata chakula cha mchana kila siku na kwao ni kawaida kwasababu wanamudu gharama!

My brother wapo wanawake wazuri wasiokuwa ombaomba na pia wapo wanawake wazuri walio ombaomba,hapo ni wewe tu kujua unataka wanawake wa aina gani na utatumia mbinu gani kupata kile unachotaka kupata!

Ukiwa unarukia kila Mwanamke kumtongoza unaweza ukakuta unakumbana na aina moja tu ya wanawake ombaomba na ukadhani wanawake wote wapo hivyo!

Nipo kwenye dunia hii hii unaoishi wewe sijawahi kuombwa Elfu 50 na mwanamke!
 
Screenshot_20220212-105107.png
 
Back
Top Bottom