Mimi ni mtu wa aina gani

Mimi ni mtu wa aina gani

EL ELYON

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Posts
1,675
Reaction score
2,115
Habari wakuu sana.
Mmebarikiwà sana na Mwenyezi Mungu.

Aisee moja kwa moja kwny hoja mi nna sifa zifuatazo.
  • nikiona mtu ana shida naumia sn mpk machozi hunilenga, mfano mtoto anapigwa au mtu yeyote Yule au nikiona mtu analia kwa uchungu.
  • napenda kukaa kimya nikiwa peke yangu kuliko nikiwa kwenye kundi la watu.
  • urafiki na mtu mpk Mimi niamue na si vinginevyo hata ufanyaje.
  • napenda kuona waliogombana wanapatana na wanafuraha hapo hata tabasamu hunijia.
  • nikipenda mwanamke nimependa kweli sina hulka za michepuko na hii imenipa shida sana.
  • Nina hasira sana yaani nikikosewa huwa nakuwa na hasira sana lakini mgumu kuchukua hatua na mwepesi WA suluhu na yanaisha kabisa.
  • simpendi mtu anifatilie wala afatilie Mambo yangu maana mi ni msiri sana na sina muda na maisha ya mtu.
  • napenda kumkubali mtu kama anakitu kizuri basi lazma nimwambie Yuko vizuri kwenye Jambo Hilo hii imepelekea wengne kunidharau kisa Tu niliwakubali kwenye Jambo Fulani.
  • wakati mwngn simpendi kuongeleshwa nataka nikae kimya Tu no story.
  • nilipata taarifa mtu kanisema kwa uwongo yaani tahakikisha namtafutia target ajae nimchane Sjari umri wake niliwahi mshambulia shangazi yangu kwa uwongo na umbea wake yaani nilimbwatukia live kabisa staki ujinga.
  • nikimchukia mtu huwa kurudi nyuma ni kazi sana.
  • ni mwepesi kukubaliana na matokeo ya Jambo lolote linalonihusu.
Sasa wakuu mnanitafsirije hapo.
 
Nenda google tafuta personality test..kisha jitathimini ...utajua tu..vinginevyo tutakudanganya buree
 
Wewe ni mdhambi mwenye mapungufu mengi kama mimi. Kitakachotuokoa ni kupokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wetu.
 
Back
Top Bottom